DAR ES SALAAM, Tanzania, July 28, 2015/ -- Tanzania
ina fursa nyingi ambazo bado hazijatumika. Kwa mujibu wa Benki ya
Dunia, uchumi unategemewa kukua kwa wastani wa asilimia7.2 mwaka huu na
uwekezaji wa serikali kwa kiasi kikubwa katika mkongo wa taifa unaongeza
biashara na upatikanaji wa teknolojia kwa raia ili kujenga fursa za
kusonga mbele kwenye teknolojia zetu. Pamoja na kuibuka kwa teknolojia
nyingi zisizokuwa na mpangilio, hatua hii imewekwa kwa ajili ya
kuongezeka kwa fursa nyingi. Haya ni maoni ya Jane Canny, Afisa
Uendeshaji Mkuu katika Kampuni la Business Connexion.
Kampuni
ya business Connexion Tanzania imekuwa ikifanya kazi tangu mwaka
2000,lengo lake kubwa hasa ni kujikita katika huduma za kifedha,
mawasiliano ya simu, nishati na madini na sekta ya umma. Kupitia
matumizi bunifu ya teknolojia na ushirikiano wetu na UmojaSwitch
Consortium, Tunatoa huduma ya upatikanaji wa miundombinu ya malipo iliyo
salama katika benki 28 na mashine za ATM 200 nchini Tanzania.
Miundombinu hii imeunganishwa na swichi tano za malipo ndani ya Afrika
Mashariki ili kuruhusu miamala ya kimataifa, makampuni makubwa matatu ya
mitandao ya simu ili kuwezesha malipo ya simu na taasisi mbalimbali za
serikali katika kuwezesha makusanyo ya malipo ya kielektroniki.
Muunganiko
wa vitu hivi vinavyotengeneza mtandao unabadili namna ya uendeshaji wa
biashara kwa kasi kubwa," anasema Canny. "Kama wateja watakuwa
wameunganishwa zaidi, mahitaji yao yanabadilika na mashirika kwani
yanapaswa kubadilika kama teknolojia na namna tunavyoitumia inabadilika,
au wanakutana na kile kilichoachwa nyuma na washindani wao.
Anaongeza
kuwa, pia kuna miradi kadhaa inayoendelea ya kuunganisha Manispaa na
hospitali nchini kote ili kuwezesha makusanyo ya malipo ya
kielektroniki. ”Huu ni mfano mkubwa ambapo teknolojia imekuwa ikitumiwa
kufanya maisha ya watumiaji yawe rahisi zaidi," anasema Canny. "Na kama
teknolojia inaendelea kukua, ndivyo jinsi ambavyo wateja wataingiliana
na watoa huduma wao. Kwa mfano,Katika miaka mitano ijayo kitengo cha
mawasiliano cha karibu au kitengo cha teknolojia cha mawasiliano kilicho
karibu kitatumika nchini kote ili kuwezesha malipo ya rejareja kupitia
simu ya mkononi. Pia tunatengeneza kiunga muhimu cha kwenye simu
kinachohusiana na benki katika intaneti, ambacho kitakuwa kinaratibiwa
katika kituo chetu cha data hapa nchini.
Canny
anasema muungano uliopendekezwa na Telkom hautarajiwi kuwa na athari
yoyote juu ya uendeshaji nchini na kampuni bado linabaki likijikita
katika soko la Tanzania. Bila kujali matokeo ya muungano uliopendekezwa,
ni biashara kama kawaida kwetu. Lengo letu kubwa ni kuhakikisha
tunaendelea kutoa suluhisho zenye ubunifu kwa wateja wetu. Tutaendelea
kuwekeza katika miundombinu ya huduma za ubadilishaji wa kifedha ili
kulinda nafasi yetu katika soko la huduma za kifedha, "anasema. "Kituo
chetu cha data nchini,ambacho kinaratibu moja ya suluhisho kubwa za
makampuni ya mawasiliano ya simu, na huduma za kufufua data pia
zinaendelea kukua.
Canny
anaamini muungano huu uliopendekezwa unaenda sambamba na mwenendo wa
kimataifa ambapo kampuni za mawasiliano ya simu na huduma za TEHAMA
zinaungana. Inatuwezesha kuinua miundombinu ya mawasiliano ya Telkom na
kutoa ufumbuzi kwa wateja wetu unaokuwa na mwisho. Wakati Telkom
haijaanza uendeshaji wake nchini Tanzania, kwa sasa unasehemu kidogo
nchini. Hii ni pamoja na mkakati wao wa ushirikiano wa kuunganisha na
uwekezaji wa miundombinu ya mawasiliano chini ya bahari kote Afrika,
bila shaka kutafaidisha wateja wetu, "anahitimisha.
No comments:
Post a Comment