MAKADA wa wanaotarajiwa kupeperusha bendera ya Chama Cha
Mapinduzi(CCM) katika Kaagera kwenye
nafasi yaubunge wamepatikana, katika uchaguzi wa kura za maoni za chama, Balozi
wa Tanzania nchini Ubelgiji, Luxembourg na jumuia ya ulaya, Diodorus Kamala
ameibuka mshindi katika kura za maoni za jimbo la Nkenge.
Dkt. Kamala ameibika mshindi baada ya kuwabwaga kwa kura
nyingi makada watano aliokuwa akichuana nao ambao ni pamoja na Asumpta Mshama aliyekuwa mbunge
wa jimbo hilo, katika jimbo la Muleba Kusini Profesa Anna Tibaijuka ameibuka
mshindi baada ya kumshinda mwenyekiti wa CCM wa wilaya ya Muleba Mhaji Bushako.
Katika mkoa wa Kagera makada wa CCM wengine walioibuka na
ushindi ni pamoja na Jassn Rweikiza aliyembwaga Nazir kalamagi, swahiba mkubwa
wa Edward Lowassa aliyeamia CHADEMA hizi karibuni, Muleba kaskazini, naibu
waziri wa Nishati na Madini, Bw. Mwijage amekuwa mshindi.
Jimbo la Biharamulo Oscar Mkassa , mbunge wa zamani wa jimbo
hilo ameibuka mshindi baada ya kuwashinda aliokuwa akichuana nao ambao ni
pamoja na Anatory Choya, katika jimbo la Bukoba mjini Balozi Khamis Kagasheki ndiye
ameibuka mshindi.
Hatima ya walishinda
katika kupeperusha bendera ya CCM kwenye uchaguzi mkuu utakaofanyika
hivi karibuni itategemea maamuzi ya vikao vya juu ya chama hicho.
No comments:
Post a Comment