Sunday, August 30, 2015

Gesi nyingi yagunduliwa Misri


shughuli za kuchimba gesi  mwambao wa Misri

Kampuni ya mafuta ya Utaliana, Eni, inasema imegundua katika mwambao wa Misri, moja kati ya visima vikubwa kabisa duniani vya gesi.
Kampuni hiyo imesema kisima hicho kiitwacho Zohr, kiko mita 1,500 chini ya bahari, na inakisiwa kuwa kina mita za mjazo bilioni 850 za gesi.
Mkurugenzi mkuu wa Eni amesema kisima hicho kipya kinaweza kuwa mmoja kati ya ugunduzi mkubwa kabisa wa gesi duniani na kitasaidia kukidhi mahitaji ya gesi ya Misri kwa miongo kadha ijayo.
Kampuni ya Eni ya Utaliana, ambayo ina haki kamili ya kuchimba kisima hicho, ni kampuni kubwa kabisa ya kigeni Afrika katika sekta ya mafuta na gesi.

No comments:

Post a Comment