Wednesday, July 17, 2013

Vita vinaendelea kati ya waasi na jeshi Goma



Wapiganaji wa M23
Vita vikali vinaendelea katika wanajeshi serikali na waasi karibu na Goma, Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Msemaji wa wapiganaji wa waasi wa M23 ameiambia BBC kuwa ndege za kivita za serikali zimefanya mashambulio ya anga katika maeneo yao usiku ya kuamkia leo.
Umoja wa Mataifa kwa upande wake umesema uko tayari kutumia nguvu, kuwalinda raia ikiwa wapiganaji hao wa M23 wataingia mjini Goma.
Mapigano hayo yanatokea, huku jeshi la Umoja wa Mataifa litakalojumuisha wanajeshi elfu tatu likijiandaa kwenda eneo hilo kuwapokonya silaha wapiganaji wa waasi.
Mwaka uliopita waasi hao walijiondoa kutoka mji huo baada ya kuuteka kwa muda.
Mazungumzo ya amani kati ya wasi hao na wawakilishi wa serikali nchini Uganda yamekwama.
Raia wakikimbia mapigano Karibu na Goma
Wakati huo huo, Mashirika ya kutoka misaada ya Kibinadam yamesema kuwa zaidi ya wakimbizi elfu sabini raia wa Congo wamekimbilia nchi jirani ya Uganda, kukwepa mapigano Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wapiganaji wa waasi wa Uganda nchini Congo, Allied Democratic Forces walishambulia mji wa Kamango na kusababisha mapigano makali kati yao na jeshi la serikali.
Mji huo kwa sasa unathibitiwa na jeshi la serikali.
Mwandishi wa BBC, Mark Doyle anasema mapigano hayo yanaashiria kibarua kigumu kinachoikabili jeshi la Umoja wa Mataifa litakalohusika na shughuli ya kuwapokonya wapiganaji wa waasi silaha katika eneo hilo.
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa mjini Goma wamewekwa katika hali ya tahadhari huku mapigano hayo yakiendelea, karibu na mji huo muhimu ambao pia ni mji mkuu wa mkoa wa Kivu ya Kaskazini.

No comments:

Post a Comment