VIONGOZI wa vyama
vingine vya ushirika vilivyoko hapa nchini wametakiwa kuja mkoani Kagera
kujifunza namma chama cha ushirika cha Kagera (KCU)kinavyoendesha
shughuli zake ili waweze kupata elimu ya itakayowasaidi kuimarisha vyama
vyao vya ushirika.
Kauli hiyo
imetolewa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Rais Jakaya
Kikwete mara kuzindua jesho la kitega uchumi lililojengwa na chama cha
ushirika cha Kagera (KCU) liliko mtaa wa one way jana.
Rais Kikwete
alisema chama cha ushirika Kagera ni moja ya vyama vya ushirika nchini
ambavyo vimeimarika zaidi na vyenye uwezo mkubwa ukilinanisha na vyama
vingine vya ushirika vilivyoko hapa nchini.
Alisema kuimarisha kwa chama hicho kunatokana na mikakati mizuri inayopangwa na viongozi wa chama hicho yenye lengo la kuiimarisha hasa kwa kikijengea uwezo zaidi.
"KCU ni chama cha ushirika ambacho ni imara kisichoteteleka na chenye mafanikio mazuri viongozi wa vyama vya ushirika ni lazima waje kupata elimu ya namna ya kuendesha vyama vyao" alisema Rais huyo.
Alisema kuimarisha kwa chama hicho kunatokana na mikakati mizuri inayopangwa na viongozi wa chama hicho yenye lengo la kuiimarisha hasa kwa kikijengea uwezo zaidi.
"KCU ni chama cha ushirika ambacho ni imara kisichoteteleka na chenye mafanikio mazuri viongozi wa vyama vya ushirika ni lazima waje kupata elimu ya namna ya kuendesha vyama vyao" alisema Rais huyo.
Alisema vyama vya ushirika
vinapoimarika vinawanufaisha zaidi wakulima kwa kuwa vinakuwa na uwezo
mkuba wa kukusanya mazao toka kwa wakulima na kuwalipa kwa wakati,
aliendelea kusema kwa vyama vya ushirika kamwe haviwezi kuimarika bila
kuwa na nguzo.
Rais huyo alisema nguzo kuu ya
inayiviimarisha vyama vya ushirika ni vitega uchumi, alisema vitega
uchumi vinaviwezesha vyama vya ushirika kupata mikopo toka kwenye
taasisi za kifedha.
"Nimefurahia taarifa
niliyopokea toka KCU inapendeza,nimefurahishwa na idadi ya vitega
uchumi vikubwa inavyovimiliki ambavyo vinaweza kuipa dhamana popote
duniani, naomba uongozi wa KCU uendelee kubuni mambo makuba zaidi"
alisema.
Alisema serikali kila mara
imekuwa ikipata mzigo mkubwa wa kuvinasua vyama vya ushirika kwa
kuvilipa madeni, amesema hali hiyo ni mbaya sana kwa kuwa inaitia
serikali hasara kubwa.
Rais Kikwete alisema sasa ni
wakati wa vyama vya ushirika kijiendesha bila kutegemea ruzuku toka
serikalini, utegemezi huo unawadidimiza wakulima kwa kuwa vinakuwa
havina uhakika wa kukusanya mazao toka kwao na kuwalipa kwa wakati.
No comments:
Post a Comment