Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Afrika ya Kusini leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Afrika ya Kusini leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation). Kutoka kulia ni Mwenyeiti wa Chama cha Wataalam Watanzania waishio Afrika Kusini, Dkt Hamza Mokiwa, Mwenyekiti wa Tanzania Women in Gauteng (TWIGA), Mama Scholastica Kimario, Rais Kikwete, Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Mhe Radhia Msuya, Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Afrika ya Kusini Bw. Deusdedit Rugaiganisa na Bw. David Mataluma, mratibu wa Vijana katika Jumuiya ya Watanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiomndoka leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation)
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika
Kusini Mhe. Radhia Msuya leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya
Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano
wa siku moja wa Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya
Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC Organ Troika on Politics, Defence and
Security Cooperation)
PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment