Msajili wa mashirika
yasiyo ya kiserikali hapa nchini MICHAEL KATEMBA ameiagiza mitandao yote
ya wilaya inayoyaunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani KAGERA
kuhakikisha inafanya uchaguzi ndani ya kipindi cha miezi MITATU kuanzia sasa
ili iweze kupata wawakilishi watakaoshiriki katika zoezi la kuwachagua viongozi
wapya wataoongoza mtandao unaoyaunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani
humo (KANGONET).
Ametoa agizo hilo leo
wakati wa kikao kilichowashirikisha wawakilishi wa mitandao inayoyaunganisha
mashirika yasiyo ya kisekari toka katika wilaya zote zilizoko mkoani KAGERA
kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya BUKOBA kilichokuwa na
lengo la kumaliza mgogoro uliopo kati ya mitandao ya wilaya mkoani humo na
uongozi wa sasa wa KANGONET.
Agizo alilolitoa KATEMBA
limekuja baada ya kuelezwa na washiriki wa kikao hicho chanzo cha mgogoro
ilioko kati ya uongozi wa sasa wa KANGONET na mitandao ya wilaya
inayoyaunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani KAGERA.
Katika kikao hicho
wawakilishi wa mitandao ya wilaya kwa nyakati tofauti walimweleza , KATEMBA kuwa
mgogoro ulipo kati ya mitandao wilaya na
KANGONET kwamba unachangiwa
na tabia ya baadhi ya viongozi wa sasa ya
kutaka kujinufaisha kupitia katika mtandao
huo na kutokataka kuitisha mikutano na uchaguzi
kwa muda mrefu.
Kwa upande wake
Mwenyekiti wa KANGONET na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilokuwa la
kiserikali (KADETFU) linalotuhumiwa kupora majukumu ya KAGONET, YUSTO MCHURUZA,
katika kikao hicho amesema shirika lake la KADETFU kuwa halina mahusiano na mtandao wa KANGONET
katika utendaji wake wa kazi, amesema mambo yanayoifanya KANGONET ishindwe
kuitisha mkutano wa uchaguzi kuwa ni pamoja na ukata unaokabili mtandao huo.
No comments:
Post a Comment