RAIS wa jamhuri ya muungano wa Tanzania, Dkt.Jakaya Kikwete ameuagiza uongozi wa
halmashauri ya manispaa ya Bukoba kuhakikisha unagawa viwanja
kwa wananchi zaidi ya 800 waliokuwa wanadai
viwanja walivyoviomba katika manispaa hiyo mwaka 2003.
Rais Kikwete alitoa agizo hilo wakati akiwahutubia wananchi
wa halmashauri ya manispaa ya Bukoba katika mkutano wa hadhara kwenyeuwanja wa michezo wa
Kaitaba baada ya kupokea taarifa toka mbunge wa jimbo la Bukoba mjini Balozi
Khamis Kagasheki juu ya malalamiko ya wananchi walioomba viwanja katika
manispaa hiyo.
Aliuambia uongozi huo pia kuhakikisha unawarejeshea wananchi
hao fedha walizozitoa wakati wa mchakato wa kuomba viwanja hivyo, ameutaka
uongozi huo kutekeleza haraka mchakato wa kuwapatia viwanja hivyo kwa wananchi
hao.
Aliuambia
uongozi huo utenge viwanja 800 kutoka kwenye viwanja vya mradi vya
upimaji wa viwanja 5,000 ambavyo halmashauri ya manispaa ya Bukoba
imeanza kuviuza kwa wananchi.
Alisema atauelewa uongozi wa manispaa hiyo ikiwa utashidwa
kutekeleza agizo alilolitoa, “lazima haki ya wananchi itendeke,
haki itatendekeka ikiwa manispaa itawapatia wananchi viwanja walivyoviomba
ambavyo hawajapatiwa kwa muda mrefu” aliagiza.
Pia katika mkutano huo aliwaeleza wananchi mradi wa ujenzi wa soko kuu la Bukoba kuwa lazima utekelezwe, Rais huyo aliuagiza
uongozi manispaa kuhakikisha unaandaa maeneo mbadala yatakayotumiwa na
wafanyabiashara watakaohamishwa katika soko hilo la sasa baada ya kuvunjwa
kupisha ujenzi wa soko jipya.
Rais huyo alitoa angalizo kwa uongozi wa manispaa kuhakikisha unatekeleza
ujenzi wa soko jipya kwa kufuata taratibu zote zinazokubalika, aliauagiza pia
kuwashirikisha wananchi katika mchakato mzima wa ujenzi wa soko hilo jipya.
Alisema mradi wa ujenzi wa soko jipya la kisasa unaweza kuwa
kichocheo kikubwa cha maendeleo katika manispaa ya Bukoba, “wananchi wanapenda
maendeleo ni lazima wakubali mradi wa ujenzi wa soko jipya la Bukoba”
alisisitiza.
Rais Kikwete aliwaambia wananchi waachane na malumbano ya
kisiasa kwa kuwa yanakwamisha mambo ya maendeleo, alisema kuwa maendeleo hayaji
mara moja yanataka mchakato, alimaliza kwa kuiwaomba wananchi kuwa kitu kimoja
hasa katika kutekeleza miradi ya maendeleo inayobuniwa.
Kwa
sasa uongozi wa manispaa hiyo unatekeleza mradi wa upimaji na wa
viwanja 5,000 ambavyo tayari imeishaanza kuviuza kwa wananchi, pamoja na
mradi wa upimaji na ugawaji wa viwanja wale walioomba viwanja mwaka
2013 uongozi wa manispaa umewaweka pembeni.