Saturday, February 14, 2015

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KASHAI HATARINI KUKUMBANA NA MLIPUKO


NA AUDAX MUTIGANZ
BUKOBA

Halmashauri ya manispaa ya BUKOBA imeshauriwa  kufanya utaratibu wa kuliondoa  DAMPO liliko karibu kabisa na shule ya msingi  ya KASHAI ambalo ni makusanyo maalumu  ya taka zinazotoka ndani ya soko kuu la kata ya KASHAI ili wawaepushe wanafunzi katika shule hiyo na  magonjwa ya mlipuko pamoja na baadhi ya wanaofanyabiashara karibu na DAMPO hilo.

Baadhi  ya wananchi walioongea na  CLOUDS wamesema DAMPO kuwa DAMPO hilo linaharatisha uhai wa wananfunzi katika shule ya KASHAI na baadhi ya wananyabiashara wanaotumia maeneo yanayozunguka DAMPO hilo kuendesha shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato.

Wananchi hao wamesema  jambo linalohatarisha zaidi uhai wa wanafunzi ni maji ya machafu  yanayojichuja kwenye taka zinazorundikwa  kwenye  DAMPO hilo ambayo hutililika hadi kwenye maji  ya  mto ulioko karibu na eneo ya shule hiyo, maji ya  mto huo  wanafunzi katika shule hiyo huyatumia kwa matumizi  mbalimbali, hapa  baadhi ya wananchi  wanavyoeleza madhara ya uwepo na DAMPO hilo.


ERNEST BYANGWAMU ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya KASHAI anayekiri  kwamba  uwepo wa DAMPO hilo namna  unavyowaathiri wanafunzi katika shule hiyo hasa nyakati za mvua.


Kwa upande wake, CHIBUNU LUKIKO ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Manispaa ya BUKOBA,  amesema kuwa manispaa hiyo iko katika mchakato wa kuliondoa DAMPO hilo,  akizungumza kwa njia ya simu amesema  kwa sasa inatafuta eneo mbadala.


No comments:

Post a Comment