NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kushirikiana na serikali kimeahidi
kuwachukulia hatua kali za kisheria na kinidhamu viongozi wa kuchaguliwa na
wananchi waliopewa jukumu la kusimamia halmashauri ya manispaa ya BUKOBA na baadhi ya watumishi waliofanya ubadhilifu wa fedha
zilizokuwa zimetengwa kutekeleza miradi
mbalimbali ya maendeleo iliyokuwa imebuniwa katika manispaa hiyo .
Kauli hiyo imetolewa na NAPE NNAUYE, katibu wa siasa itikadi na uenezi wa taifa wa Chama Cha Mapinduzi CCM kwenye hotuba yake aliyoitoa kwenye maalumu mkutano wa hadhara ulifanyika
kwenye uwanja wa uhuru wa kumsimika DEONIZ MALINZI aliyeteuliwa kuwa kamanda wa
jumuia ya vijana katika mkoa wa KAGERA.
Sambamba na kauli hiyo, katibu huyo amemuagiza mkuu wa mkoa
wa KAGERA , JOHN MONGELLA kuhakikisha anatafuta ufumbuzi migogoro iliyochangia kukwamisha miradi ya maendeleo katika manispaa hiyo
iliyochangiwa na hatua ya baadhi ya madiwani kugomea vikao vya baraza kwa zaidi ya
miaka MIWILI jambo lililodumaza
maendeleo ya wananchi.
Katika mkutano huo Balozi KHAMIS KAGASHEKI mbunge wa jimbo la BUKOBA mjini amenusha
kwamba yeye sio chanzo cha migogoro iliyokwamisha utekelezaji wa miradi ya
maendeleo katika manispaa hiyo bali yeye
ni mtetezi wa wananchi, nao makada wa CCM, AMIM
AHMED na PROTACE ISHENGOMA wanaeleza
namna chama hicho kilivyojipanga kuwawezesha vijana kiuchumi huku wakiwahimiza vijana kujiunga na vyama vya akiba na mikopo.
SADIK HASSAN ni mwenyekiti wa VIjana wa CCM wilaya ya NGARA
anayewaleza vijana wajiepushe na udanganyifu unaofanywa na viongozi wa vyama
vya upinzani na kuwataka pia wasikubali
kurubuniwa, huku DIONIZ MALINZI kamanda
wa vijana wa mkoa wa KAGERA akiahidi kuiimarisha jumuia ya vijana katika mkoa
huo.
Mgogoro katika manispaa ya BUKOBA ulikwamisha utekelezaji wa
miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokuwa imebuniwa ambayo ni pamoja na mradi wa
ujenzi wa soko kuu la BUKOBA, upimaji wa viwanja ELFU tano, ujenzi wa standi
kuu ya mabasi eneo la KYAKAILABWA na jingo la kitega uchumi.
Baadhi ya viongozi ambao ni madiwani wakiongozwa na BALOZI
KAGASHEKI walipinga utekelezwaji wa miradi hiyo kwa madai kuwa ilikuwa imeghubikwa
na vitendo vya ubadhilifu hali ambayo iliwagawa madiwani hadi baadhi yao wakafikia
hatua ya kususia bikao.
No comments:
Post a Comment