NA MHARIRI
AUDAX MUTIGANZI +255 784 939 586/ 753 844 995
Mahakama kuu kanda ya BUKOBA imezindua kikao vya mahakama ya
rufaa ambapo mashauri mbalimbali ISHIRINI na SITA yatasikilizwa huku mengine yakitolewa maamuz na jopo la majaji wa mahakama hiyo,
uzinduzi wa vikao hivyo umefanyika leo kwenye viwanja vya mahakama hiyo iliyoko
katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba.
Uzinduzi huo ulienda sambamba na gwaride maalumu lililoandaliwa na kikosi
cha jeshi la polisi cha kutuliza ghasia lililokaguliwa na jaji EDWARD RUTAKANGWA ambaye ni mwenyekiti
wa majaji watakaosikiliza mashauri yote
yatakayoletwa mbele ya mahakama ya rufaa
uliudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali walioongozwa na mkuu wa mkoa wa
KAGERA JOHN MONGELLA..
Akitoa wakati wa
uzinduzi huo ,CHARLES MAGESSA ambaye msajili
wa mahakama kuu kanda ya BUKOBA amesema sambamba
na kikao vya mahakama hiyo ya rufani pia mahakama kuu kanda ya BUKOBA itakuwa kikao kitakachoanza leo katika vituo viwili ambavyo alivitaja kuwa ni
pamoja na BUKOBA na BIHARAMULO ambapo jumla
ua mashauri ISHIRINI na SABA yatasikilizwa.
Aidha , msajili huyo amesema mahakama hiyo imeandaa vikao
hivyo kwa washirikisha wadau wakuu wa mahakama hiyo ambao aliwataja kuwa ni
pamoja na jeshi la polisi na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, MAGESSA
amesema asilimia kubwa ya wakaotoa ushahidi unaohusiana na mashauri
yatakayosikilizwa kwamba wanaonyesha mwitikioa mzuri.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliohudhulia uzinduzi wa
vikao hivyo wameshukuru hatua ya serikali ya kusogeza huduma mahakama ya rufani
katika mkoa wa KAGERA, kwa nyakati tofauti wamesema kuwa uwepo wa Mahakama ya
rufani katika mkoa wa KAGERA utawapa nafasi kubwa ya kutetea haki zao ambazo
wakati mwingine walikuwa wakipokonywa walikuwa wakifuiata huduma ya mahakama ya
rufani mkoani MWANZA.
Kabla ya serikali
kusogeza huduma ya mahakama ya rufani mkoani
KAGERA mwaka jana, wananchi walikuwa wakisafiri hadi mkoani MWANZA kusikiliza mashauri yao, hali hiyo
ilikuwa ikiwapa wakati mgumu wananchi hao
hasa wenye kipato kidogo wakatii
mwingine walikuwa wakilazimika kupoteza haki yao, wengi walikuwa wakishindwa kumudu
gharama za usafiri na malazi.
No comments:
Post a Comment