NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA
Kamati ya huduma ya afya ya msingi katika mkoa wa KAGERA imefanya kikao cha
dharura kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati mbalimbali yenye lengo la kupunguza
vifo vya watoto wachanga chini ya umri
wa miaka MITANO na wakina mama wajawazito.
Kikao hicho kimefanyika wilayani KARAGWE kwenye ukumbi wa hoteli ya kanisa la kiinjili la
KIRUTHERI diosisi ya KARAGWE iliyoko
katika mji wa mdogo wa KAYANGA chini ya
mkuu wa mkoa wa KAGERA, JOHN MONGELLA.
Katika kikao hicho kilichohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali katika ngazi zote, mkuu huyo wa mkoa amewaagiza wakuu wa wilaya mkoa humo katika kila vikao wanavyoviandaa vya kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo kuweka ajenda ya namna ya kudhibiti vya vifo vya watoto wachanga chini ya miaka MITANO na wakina mama wajawazito.
DKT THOMAS RUTACHUNZIBWA ni mganga mkuu wa mkoa wa KAGERA na
NEEMA KYAMBA mratibu wa huduma ya watoto na wakina mama wajawazito katika mkoa huo ni maofisa wa afya
wanaoeleza hali ya sasa ya vifo vya watoto na wakina mama.
Kwa upande wake GRANDIOSA
TIBAIJUKA ambaye ni meneja taaluma wa
mradi wa JHPIEGO unaofadhiliwa na seriikali ya MAREKANI anaishauri jamii kuchangia huduma ya afya ili
iweze kupata matibabu sahihi badala ya kutegemea sana misaada toka kwa serikalini
na wafadhili, DALI RWEGASIRA mkuu wa wilaya ya KARAGWE na DENIS
MBEO mkuu wa wa wilaya ya BIHARAMULO ni miongoni mwa wakuu wa wilaya wanaoeleza
mikakati yao ya namna ya kuthibiti vifo
vya wakina mama na watoto kwa kuwahamasisha wananchi wajiunge na mfuko wa afya ya jamii.
Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa michache hapa nchini
ambazo inafanya mikakati mikubwa ya kuhakikisha vifo vya wakina mama wajawazito
na watoto cinini ya miaka MITANO vinabaki kwenye vitabu vya historia, mkakati
wa mkoa huo ni kuihamasisha jamii namna ya kujiepusha na vifo hivyo kuanzia
ngazi ya vijiji, mtaa na vitongoji.
No comments:
Post a Comment