Wanachama na wapenzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wametakiwa kudumisha umoja na mshikamano miongoni mwao badala kuendekeza tabia ya inayokigharimu chama hicho kwa sasa inayofanywa na baadhi wanachama wa chama hicho ya kutafunana wenyewe kwa wenyewe.
Wito huo umetolewa leo na IDD ALI AME ambaye katibu wa CCM mkoani Kagera wakati wa kikao cha kutathimini na kujadili masuala ya maendeleo katika wilaya ya MULEBA kilichoandaliwa na PROFESA ANNA TIBAIJUKA, mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa (NEC) na mbunge jimbo la MULEBA KUSINI kilichofanyika kwenye jengo la taasisi ya KAJUMULO ambacho kiliwashirikisha viongozi wa chama hicho kuanzia ngazi ya mashina hadi wilaya.
AME amesema ikiwa wanachama wa CCM wataendekeza tabia ya kutafunana wenyewe kwa wenyewe wataleta mpasuko ndani ya chama hali itakayovipa nafasi vyama vya upinzani ya kushinda chaguzi mbalimbali jambo litakalochangia kukichimbia chama hicho kaburi.
Kwa upande wao , DEOGRATIAS RUTAGUMWA, katibu wa CCM wa mkoa wa KILIMANJARO na DIDAS ZIMBIILE , katibu wa jumuia ya umoja wa vijana mkoani KAGERA wanawashauri wananchi wilayani MULEBA kuzipuuza kauli zinazotolewa na wapinzani, Naye PROFESA ANNA TIBAIJUKA anaeleza mikakati yake na namna masuala ya kuendeleza elimu yalivyomgharimu, huku ERNESTINA RICHARD, katibu wa wazazi wa mkoa wa KAGERA anawaomba wananchi wawe na imani na PROFESA TIBAIJUKA.
Profesa Tibaijuka amewaahidi wananchi kuwa ataendelea kutetea nafasi yake ya ubunge pamoja na kuwajibishwa na kufuatia tuhuma za fedha alizozipata toka kwa RUGEMALILA.
No comments:
Post a Comment