NA AUDAX MUTIGANZI
MULEBA
Mbunge wa jimbo la MULEBA kusini PROFESA ANNA TIBAIJUKA ameshauriwa wananchi katika jimbo hilo kuwapuuza wanaochanganya masuala ya siasa na masuala ya maendeleo hasa wale wanaobeza mambo yanayobuniwa na viongozi yenye lengo la kuboresha maisha hali zao za maisha.
PROFESA TIBAIJUKA ametoa ushauri huo wakati semina ya siku MOJA iliyofanyika kwenye ukumbi wa jengo la taasisi ya KAJUMULO ulioko wilayani MULEBA ambayo iliandaliwa na mbunge huyo kwa wafanyabiashara na wakulima wa zao la ndizi katika jimbo la hilo ambayo ilikuwa na lengo la kujadili mikakati ya kuhakikisha zao hilo linakuwa na soko la uhakika.
Mbunge huyo ambaye alikuwa waziri wa ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi amesema masuala ya maendeleo hayaendani na itikadi za kisiasa, amewakemea wanaodhani kwamba kwa sasa amejikita katika masuala ya kuwaletea maendeleo wananchi kwa lengo la kujiongezea umaarufu.
INSERT No.1……Profesa Anna Tibaijuka……Mbunge wa Muleba kusini
ELIUD ISHABAKAKI, GIBSON MUGANYIZI, SIMON MBALULA na STEVEN ANGELICUS ni miongoni mwa wafanyabiashara na wakulima wa ndizi walioudhuria semina hiyo wanaoeleza hali ya soko la ndizi, changamoto wanazokabiliana nazo na pia wanatoa ushauri kwa serikali, huku EDMUND KATANGAYO akiwahimiza wananchi katika jimbo kubuni fursa mbalimbali zinazoweza kuwaondoa katika wimbi la umaskini.
No comments:
Post a Comment