NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA +255 784 939 586
Jeshi la polisi mkoani KAGERA limefanikiwa kudhibiti vitendo vya uharifu vya utekaji wa magari vilivyokuwa vimekiri mkoani humo katika maeneo ya pori la KIMISI lililoko wilayani BIHARAMULO na pori la KASINDAGA lililoko wilayani NGARA vilivvyokuwa vikifanywa na watu wanaosadikiwa toka nchi jirani.
Akizungumza wakati wa sherehe iliyoandaliwa na jeshi hilo kwa lengo la kukaribisha mwaka 2014 na kukaribishwa mwaka 2015,Kamishina msaidizi HENRY MWAIBAMBE, kamanda wa jeshi la polisi mkoani KAGERA, amesema matukio ya uharifu ya vitendo vya utekaji wa magari kwenye mapori hayo kwa mwaka 2013 kwamba yalikuwa SABA wakati katika mwaka 2014 hakuna tukio lolote lililotokea.
Aidha, kamanda huyo amewataka maofisa wa jeshi la polisi kufanya kazi kwa weredi zaidi ili jeshi hilo katika mkoa huo liweze kutimiza malengo yake ya kuzuia uharifu kwa asilimia kubwa na pia kutoa wito kwa wanasiasa, naye Mkuu wa kikosi cha kutuliza ghasia mkoani Kagera ,mrakibu mwandamizi JEMSI WEKWE anawahimiza maofisa wa jeshi hilo kuzingatia maelekezo ya viongozi wao, huku WINSTON KABANTEGA mwenyekiti wa kamati ya usalama barabarani ya mkoa wa KAGERA akiitoa ushauri utakaoiwezesha mikoa mingine kupunguza ajali.
Kwa mjujibu wa takwimu mkoa wa Kagera kwa mwaka 2014 umefanikiwa kudhibigti ajali za barabarani kwa asilimia THEMANINI na TISA ukilinganisha na mwaka 2013, katika mkoa huo matukio ya uharifu yaliyoongezeka kidogo katika mwaka 2014 ni pamoja na ya ubakaji, wananchi kujichukulia sheria mkononi, pia katika mkoa huo matukio ya ujambazi wa kutumia silaha kwa mwaka 2014 yamethibitiwa kwa zaidi ya asilimia AROBAINI na TANO.
Katika sherehe hiyo maofisa wa jeshi la polisi na wadau wa jeshi hilo hapa wanaonyesha umahili wao katika kusakata wimbo wa mwana muziki maarufu kanda bongoman.
No comments:
Post a Comment