Na. Mwandishi Wetu
Tume ya Rais ya Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza itakusanya taarifa na kupokea
malalamiko yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili Nchini
mikoa ya Mikoa ya Arusha, Manyara, Tabora, Singida na Dodoma.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa tarehe 24 Desemba, 2014 na Katibu wa Tume hiyo,
Bw.Frederick Manyanda, Tume inatarajiwa kuendelea na zoezi la kukusanya maoni na
taarifa kuanzia tarehe 5 Januari , 2015 mpaka tarehe 21 Januari,2015
katika maeneo mbalimbali ya kanda ya Kaskazini na Kati Nchini.
Katika
kutekeleza jukumu hilo, Bw. Manyanda ameeleza kuwa, Tume itatembelea Mkoa wa Tabora tarehe 4 Januari 2015 mpaka tarehe
8 Januari 2015 na itakuwa Mkoa wa Singida tarehe 9 Januari,2015 mpaka tarehe 10 Januari,2015.
Aidha Tume
itatembelea Mkoa wa Dodoma tarehe 11
Januari, 2015 mpaka tarehe 12 Januari 2015. Vilevile, Wakili Manyanda ameeleza
kuwa Tume itakusanya maoni Mkoa wa Manyara
kuanzia tarehe 13 Januari, 2015 mpaka
tarehe 16 Januari, 2015 na Tume itakuwa Mkoa wa Arusha tarehe 16 Januari 2015 mpaka tarehe 19 Januari,2015.
Mpaka sasa
Tume ya Rais ya Operesheni Tokomeza imefanikiwa kukusanya taarifa na kupokea malamiko
yaliyotokana na utekelezaji wa Operesheni Tokomeza katika mikoa kumi na tano
(15) ya Tanzania Bara ambayo ni Kigoma, Katavi, Rukwa, Mbeya Kagera, Geita, Shinyanga, Simiyu, Mwanza
Mara,Lindi,Mtwara,Ruvuma,Iringa, Morogoro.
Pamoja na
mikutano hiyo, Bw. Manyanda ametumia fursa hiyo kuwakumbusha na kuwaomba
wananchi na watanzania wa maeneo husika kuendelea kutuma taarifa na malalamiko
kuhusu utekelezaji wa Operesheni Tokomeza kwa njia ya barua, simu na barua pepe
ambapo ameeleza kuwa wananchi wanaweza kutuma barua kwa Katibu wa Tume, Tume ya
Uchunguzi wa Operesheni Tokomeza Ujangili, SLP
9050, Dar es Salaam na barua pepe kwenda opereshenitokomeza@agctz.go.tz.Aidha, wananchi wa maeneo husika wanaweza kutuma ujumbe mfupi wa maandishi kwa namba za simu za Tigo: 0714 826826; Vodacom: 0767 826826; Airtel:
0787 826826; na Zantel: 0773 826826.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment