Sunday, December 14, 2014

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

Alliance for Change and Transparency
(ACT-TANZANIA)

Mabadiliko na Uwazi
House no. 203, Mpakani A Street, Kijitonyama, P.O. Box 105043, Dar es salaam.
Tel: +255 763 463740 / 715 784670, Email: acttanzania@gmail.com.
All letters to be addressed to the Secretary General
14 Desemba 2014 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI. Ndugu wanahabari, Kama mjuavyo leo ni siku ya uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji katika taifa letu. Chama chetu cha ACT-Tanzania kimeshiriki uchaguzi huo ukiwa ndio uchaguzi wetu wa kwanza kushiriki tangu chama kipate usajili wa kudumu hapo Mei 5, 2014. Chama kimesimamisha wagombea wapatao 2,202 nchi nzima katika mikoa karibu yote ya Tanzania bara ambayo ndiyo inayoshiriki uchaguzi huo. Wakati zoezi hilo likiendelea wakati huu, kama chama tunapenda kusema yafuatayo kuhusiana na uchaguzi huu:
1. Tunapenda kutoa shukrani zetu za dhati kwa watanzania kwa kutupokea na kutukubali na hata kutuwezesha kupata wagombea 2,202. Si jambo la kawaida kwa kwa chama kilichosajiliwa miezi 7 iliyopita kupata idadi hiyo ya wagombea. Miongoni mwa wagombea hao 2,202 tayari chama chetu kimeshapata ushindi kwa mgombea mmoja aliyepita bila kupingwa. Nafurahi kumtangaza Mwenyekiti wa kwanza wa Serikali ya Kitongoji kupitia ACT-Tanzania ambaye ni ndugu Ndugu Justin Kahonga Mwenyekiti wa Serikali ya Kitongoji cha Songambele , Kijiji cha Masigo katika Kata ya Ilela wilayani Mlele Mkoa wa Katavi. Ahsante wananchi wa Songambele kwa kutufanya wa kwanza katika kitongoji chenu. Tunawaahidi utumishi uliotukuka na tutakuwa karibu na mwenyekiti wetu kumshauri, kumwelekeza na kumsaidia kila panapobidi ili awatumikie vema.
2. Tunapenda kueleza masikitiko yetu kwa jinsi uchaguzi huu unavyoendeshwa na wizara ya TAMISEMI. Kumekuwa na matatizo mengi sana hasa mahali ambapo chama chetu kina nguvu na zaidi sana katika maeneo ambayo kuna wagombea wawili tu yaani wa ACT-Tanzania na CCM. Baadhi ya matatizo tuliyoyashuhudia nchi nzima ni kama ifuatavyo:
i. Uchaguzi kuahirishwa maeneo mbalimbali kwa kisingizio cha kukosekana kwa vifaa vya uchaguzi kama karatasi za kupigia kura, nk, majina ya wagombea kuchanganywa na kadhalika. Mfano katika
Alliance for Change and Transparency
(ACT-TANZANIA)
Mabadiliko na Uwazi
House no. 203, Mpakani A Street, Kijitonyama, P.O. Box 105043, Dar es salaam.
Tel: +255 763 463740 / 715 784670, Email: acttanzania@gmail.com.
All letters to be addressed to the Secretary General
wilaya nzima ya Kaliua ambako maeneo mengi wagombea ni wa ACT-Tanzania na CCM tu, uchaguzi umesimama hadi ninapoandika taarifa hii. Maeneo mengi hakuna karatasi za kupigia kura na majina ya wagombea yamechanganywa sana. Jina la Mgombea wa kijiji A linapelekwa Kijiji B. Uchaguzi katika kata ya Vingunguti jimbo la Segerea, wilaya ya Ilala jijini Dar es salaam wilaya ambayo ndipo yalipo makao makuu ya Ofisi ya Waziri Mkuu, wizara ya TAMISEMI, uchaguzi haukufanyika kabisa kwa kisingizio kwamba hakuna karatasi za kupigia kura.
ii. Maeneo mengine majina ya wagombea wa ACT-Tanzania hayakuwepo kabisa kwenye karatasi za kupigia kura. Hilo limetokea wilayani Bukombe, hususan Kata ya Runzewe mashariki, Kijiji cha Ikuzi na vitongoji vya Kigoba A na Burumbonga A. Aidha maeneo mbalimbali ya wilaya ya Busega na Kasulu, Wilaya ya Kondoa Kata ya Kisese kijiji cha Disa, Wilaya ya Geita kata ya Nkome kijiji cha Nkome, wilaya ya Mlele Kata ya Inyonga kijiji cha Inyoga, Wilaya ya Kahama kata ya Nyansubi, mtaa wa Nyansubi, Mtaa wa Kilimo B Kata ya Kishiri, wilaya ya Nyamagana, na maeneo mengine mengi, majina ya wagombea wetu wa uenyekiti na wajumbe hayamo kwenye karatasi za kupigia kura kusababisha uchaguzi kuchelewa kuanza ama kuahirishwa kabisa katika maeneo hayo. Hata hivyo Mtendaji wa Kata ya Nkome wilayani Geita amelazimisha uchaguzi uendelee kwa kutumia karatasi ya kura ambayo haina mgombea wa chama chetu kwa madai kwamba eti atatoa uamuzi baadaye.
iii. Wagombea wetu kutokuwa na nembo ya chama mbele ya majina yao. Hilo limeripotiwa maeneo karibu yote katika wilaya ya Ilemela jijini Mwanza, japo nembo tulishampa mkurugenzi wa halmashauri ya manispaa muda mrefu karibu ya siku ya uchaguzi.
iv. Wafuasi wa chama kimoja kutokeza na mapanga na silaha nyingine za jadi kutaka kuvuruga uchaguzi. Katika Mtaa Ihoga Kata ya Maina wilaya ya Nyamagana, ambako kuna wagombea wawili tu wa ACT-Tanzania na CCM, wafuasi wanaosadikiwa kuwa chama kimoja cha upinzani ambacho mgombea wao alienguliwa kwa pingamizi
Alliance for Change and Transparency
(ACT-TANZANIA)
Mabadiliko na Uwazi
House no. 203, Mpakani A Street, Kijitonyama, P.O. Box 105043, Dar es salaam.
Tel: +255 763 463740 / 715 784670, Email: acttanzania@gmail.com.
All letters to be addressed to the Secretary General
wameibuka kwenye kituo cha kupigia kura wakiwa na mapanga na silaha za jadi kwa ajili ya kutaka kuvuruga uchaguzi huo. Tumeripoti kwa mkuu wa polisi wa wilaya na kumtaka kushughulikia tatizo hilo haraka.
Natoa wito kwa wizara ya TAMISEMI kuhakikisha wanawapa maelekezo ya dhati na dharura wasimamizi wote wa uchaguzi kuhakikisha uchaguzi unafuata taratibu. ACT-Tanzania hatutatulia huku tukiona haki yetu ikiminywa kwa kutumia uchaguzi usio huru wala haki. Viongozi wetu wote wa Mikoa, Majimbo, Kata na Matawi wako macho pamoja na wagombea wetu kuhakikisha haki yetu inapatikana. Nawashukuru tena viongozi, wanachama na watanzania kwa ujumla kwa sapoti wanayotupatia. Samson Mwigamba KATIBU MKUU, ACT-TANZANIA.
Alliance for Change and Transparency
(ACT-TANZANIA)
Mabadiliko na Uwazi
House no. 203, Mpakani A Street, Kijitonyama, P.O. Box 105043, Dar es salaam.
Tel: +255 763 463740 / 715 784670, Email: acttanzania@gmail.com.
All letters to be addressed to the Secretary General

No comments:

Post a Comment