Baadhi ya wafanyabiashara waliokuwa wamepakia mizigo yao ndani meli ya MV
VICTORIA iliyotarajiwa jana
kuondoka bandari ya BUKOBA
kuelekea bandari ya MWANZA
wameandamana hadi ofisi ya mkuu wa wilaya ya BUKOBA kupinga hatua ya mamlaka ya
uthibiti wa usafiri wa maji na nchi kavu (SUMATRA) ya kuzuia safari ya meli
hiyo isiendelee na safari.
Mamlaka hiyo imefikia uamzi wa kuzuia safari hiyo baada ya kubaini matatizo ya kiufundi ya meli
hiyo, imedaiwa meli hiyo iliyotoka bandari ya MWANZA siku ya jumanne na kufika bandari ya BUKOBA jumatano majira
ya saa MOJA na NUSU asubuhi kuwa ilisafiri kwa kutumia injini moja hali ambayo ni hatari kwa usalama
wa abiria na mizigo.
Kufuatia hatua ya
SUMATRA ya ya kuzuia safari ya
meli hiyo baadhi ya wafanyabiashara hasa
waliokuwa wamepakia mizigo inayoharibika haraka ambayo ni pamoja na ndizi mbivu
, maparachichi na mazao mengine hapa
wanalalamika kwa kuiomba serikali iwanusuru kwa kuiruhusu meli hiyo iendelee na
safari ili waweze kuokoa sehemu bidhaa zao ambazo zimeanza kuharibika.
ZIPORAH PANGANI
ambaye ni mkuu wa wilaya ya BUKOBA
anaongea na wafanyabiashara waliofanya mgomo na kuwaeleza namna serikali
itakavyotatua tatizo hilo, ALEX KATAMA ni Meneja wa SUMATRA ambaye anaeleza
sababu za mamlaka hiyo kuzuia meli hiyo, naye MATHEW BAJUMUZI afisa wa shirika la huduma za meli anaeleza
kilichijitokeza, huku JOHN
MONGELLAakisisitiza kwamba serikali ya mkoa wa KAGERA haitaruhusu meli hiyo
hadi ijiridhishe kwa lengo la kulinda usalama wa abiria na mali zao.
Meli hiyo inasadikiwa kuwa ni mbovu na inataka matengenezo makubwa,
katika kipindi cha miezi MITATU imezimika mara TANO ikiwa ndani ya ziwa
VICTORIA wakati ikiendelea n a safari zake.
No comments:
Post a Comment