-Awafunga watumishi
Yanga: Aagiza Polisi ‘Marafiki’ kuwakomesha
Baada ya kumtimua kocha Mkuu wa timu yake na baada ya
kubwaga chini sekretariati ya klabu hiyo, Mwenyekiti wa Klabu ya Young Africans
Sports Club (Yanga) Bw. Yusuf manji, ameamua kuwafanyizia baadhi ya waliokuwa
watumishi wa Klabu hiyo akiwemo Beno Njovu, Katibu Mkuu aliyepita.
Wakandamize haswa
Kulingana na mawasiliano yaliyonaswa na makachero wetu kati
ya Mwenyekiti huyo na viongozi wa juu wa Klabu hiyo, Manji amewapa maelekezo
wanasheria wake na Sekretariati ya sasa kuwafungulia mashtaka Sekretariati
iliyopita kwa madai ya
ufujaji pesa, huku akiwataka viongozi hao kutumia ‘marafiki’ zao
waliooko katika jeshi la polisi ‘kuhakikisha wanashugulikiwa’
Katika mawasiliano hao kupitia email ya tarehe 22 Desemba ,
Manji pia anamwagiza mtu aliyetambulika kuwa mhasibu anayaenda kwa jina la Amit kugaramia ‘maagizo
hayo yote’, na kumpa taarifa kila siku.
Vyombo vya habari
kutumika
Manji pia ameagiza
wafanyakazi hao wazamani ‘wachafuliwe’ kupitia kampeni kali magazetini, huku
akielekeza ‘Press Release’ yenye saini yake itolewe ikionesha ‘masikitiko
yake’.
Adhabu mbele, hukumu
nyuma
Huku akitoa maagizo wafanyakazi hao washugulikiwe ipasavyo
na polisi ‘marafiki’ zake, Bwana Manji ametupilia mbali haki za wafanyakazi hao
kusikilizwa kukiwa hakuna uchunguzi wowote uliokwishafanyika kuhusu madai yake
dhidi ya watumishi hao zaidi ya hisia zake mwenyewe na Sekretariati mpya
inayotekeleza kila alitakalo bila kuhoji.
Maagizo yazua mpasuko ndani ya kamati tendaji
Kufuatia maagizo ya Manji, mmoja wa watumishi wapya
aliyetambulika kama Frank Chacha alitekeleza maamuzi hayo ambayo mwenyekiti
huyo alikuwa amesema hayapingiki wala hayahojiki kwa email yake, huku
wakifungua kesi katika kituo cha Polisi kati Dar es salaam na kufanikiwa kuweka
wafanyakazi wawili ndani huku wakiendelea kumuwinda Beno Njovu
Lakini masaa machache baada ya hatua hizo, kuna dalili kuwa
baadhi ya viongozi ndani ya klabu hiyo wanapinga vikali hatua hizo za Manji na
wametishia ‘kuaachia’ ngazi.
Mpasuko huo ndani ya Yanga umedhihirishwa na email kutoka
kwa Bwana Omar, Mkurugenzi mpya wa Fedha na Utawala akimjulisha Manji kuwa jana
Jumanne, baada ya kutekeleza maagizo ya Mwenyekiti huyo alipokea simu kutoka
kwa Isaac Chanji, mjumbe wa Kamati
Tendaji akitishia kuwa hatua ambazo
zilikuwa zimeshachukuliwa zilikuwa za hatari kwa Klabu hiyo na kuwa yeye Chanji
na wajumbe wengine wengelazimika kuwaachia akina Omari na Chacha timu hiyo.
Maswali tata
Kufuatia hatua hii ya Manji mtu unaweza kujiuliza maswali
kadhaa:
1. Je
kwa nini Yanga inakuwa na kesi kila wakati? Gharama za kesi hizi, ambazo
nyingine siyo za lazima, si mzigo usiokuwa na faida kwa Yanga? Mara wachezaji,
makocha, na Sekretariati za nyuma.
2. Ni
dhahiri kuwa hata kama kesi hii ya sasa ina msingi wowote, basi uchunguzi
ungetangulia. Lakini, labda kwa jeuri ya hela, Manji ameshawahukumu watumishi
wale na ni wazi kuwa yuko tayari hata kupindisha sheria ili afikie lengo lake.
3. Lengo
la Manji hasa ni nini? Anajaribu kuwaadhibisha hawa watumishi kweli au ni
kujenga hoja za Mkutano Mkuu wa Klabu hiyo unaotegemewa kufanyika Januari 2015
kwa kujenga mazingira ya kuwasahaulisha wanachama wa Yanga baadhi ya ahadi alizotoa na ambazo hadi sasa bado ni
ahadi hewa tu?
No comments:
Post a Comment