WAZIRI
MKUU Majaliwa Kassim Majaliwa amewataka wafanyakazi wa Ofisi ya Waziri Mkuu
watambue jukumu walilonalo la
kuwahudumia wananchi kutokana na majukumu ya ofisi hiyo ambayo yanagusa maisha
ya kila siku ya Watanzania.
“Ofisi
ya Waziri Mkuu ni kubwa na pana sana na inahusika na shughuli za kila siku za Watanzania.
Kwa hiyo tuna kazi kubwa ya kukidhi matarajio yao,” alisema.
Ametoa
kauli hiyo leo mchana (Jumatatu, Novemba 23, 2015) wakati akizungumza na wakuu
wa taasisi, wakurugenzi na watumishi wa Ofisi ya Waziri Mkuu kwenye mkutano
uliofanyika ofisini kwake, Magogoni, jijini Dar es Salaam. Leo ndiyo ameripoti
kwa mara ya kwanza tangu alipoapishwa Ijumaa iliyopita kwenye Ikulu ya Chamwino,
mkoani Dodoma.
Pamoja
na kazi nyingine tunayo majukumu makubwa ambayo ni udhibiti, usimamizi na
ufuatiliaji wa masuala mbalimbali humu Serikalini. Ninataraji kupata mpango
kazi kutoka kwa Mkuu wa kila idara na kila taasisi zilizo chini
ya Ofisi ya Waziri Mkuu. Nitakwenda pia ofisi za TAMISEMI ili kuweka vipaumbele
vyetu sawa,” alisema.
Aliwataka
watumishi hao wawe tayari kutekeleza kaulimbiu ya ‘Hapa Kazi Tu’ ambayo imekuwa
ikisisitizwa na Rais Dkt. John Pombe Magufuli ili kuweza kumudu kasi ya
utendaji kazi Serikali ambayo anaihimiza hivi sasa.
Alisema
ana imani kuwa watumishi hao watampa ushirikiano kama ambavyo walikuwa wakiutoa
kwa mtangulizi wake, Mhe. Mizengo Pinda ambaye amestaafu hivi karibuni.
(mwisho)
IMETOLEWA
NA:
OFISI
YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,
No comments:
Post a Comment