Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza katika kikao kati ya ujumbe wa
Tanzania na ujumbe wa Polanda aulioongozwa na Rais Mstaafu wa nchi hiyo
Lech Walesa (kushoto) katika hafla ya utiaji saini makubaliaono ya
mkopo nafuu ambapo Tanzania itapokea matrekta kutoka Poland
yatakayounganishwa na SUMA JKT hapa nchini. Utiaji saini huo ulifanyika
kwenye Makao Makuu ya JKT Mlalakuwa jijini Dar es slaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Rais mstaafu wa Poland, Lech Walesa
(kulia kwake) wakiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa Tanzania na
Poland ulioshiriki katika mazungumzo na utiaji saini makubaliano ya
mkopo nafuu ambapo Tanzania itapokea matreta na maghala kutoka poland .
Utiaji saini huo ulifanyika kwenye makao makuu ya JKT, Mlalakuwa jijini
Dar es slaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Rais Mstaafu wa Poland, Lech
Walesa (kulia) baada ya kushuhudia utiaji saini wa makubaliano ya
mkopo nafuu wa matrekta na magahala ya nafaka kutoka Poland kwenye mako
Makuu ya JKT, Mlalakuwa jijini Dar es slaam.
No comments:
Post a Comment