Thursday, October 29, 2015

Safari za ndege za shirika zaanza kuelekea kituo cha 13 katika Afrika Mashariki


Dubai, Muungano wa Falme za Kiarabu. 25 Oktoba 2015 / -- Ndege ya Safari ya uzinduzi ya FZ665 ya flydubai imetua jana kwenye mji mkuu wa Eritrea, Asmara. Huku ikitua katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Asmara, maafisa wakuu wa Eritrea wakiongozwa naTesfaslassieBerhane, Waziri wa Usafiri na Mawasiliano, AskaluMenkorios, Waziri wa Utalii na PaulosKahsai, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Safari za Ndege aliukaribisha ujumbe wa flydubai ukiongozwa na SudhirSreedharan, Kaimu rais Mkuu, timu ya Kibiashara (GCC, Bara hindi, Afrika) na wanachama wakuu wa usimamizi wa shirika hili la ndege.
 
Ghaith Al Ghaith, Afisa mkuu wa flydubai alisema, “Kuongezwa kwa Asmara kwenye mfumo wetu unaonyesha kujitolea kwetu katika kuimarisha uunganishaji wa safari za ndege hadi Dubai ambao unahusisha vituo 67 ambavyo hapo awali havikuwa na uunganishaji wa safari za ndege za moja kwa moja hadi Dubai au vilivyokosa kuhudumiwa ipaswavyo hapo awali. Mji mkuu wa Eritrea umefanyika kituo chetu cha 13 cha Afrika Mashariki.”
Asmara ndicho kituo cha 17 ambacho flydubai ilitangaza mwaka huu na shirika la ndege lenyewe hivi majuzi limezindua safari hadi Burundi, Rwanda, Somaliland, Tanzania na Uganda.
 
Sudhir Sreedharan Kaimu Rais Mkuu, Kibiashara (GCC, Bara Hindi, Africa), flydubai alisema: “Kwa nyongeza ya safari nne kwa wiki hadi Asmara, tunawapa abiria kutoka Afrika Mashariki na muunganisho wa moja kwa moja hadi Dubai. Wakati abiria wanapochagua flydubai watafurahia huduma zetu za usafiri zinazoweza kugharamikika, zisizo na usumbufu, na zenye kutegemewa, ujuzi wa safari ya kutamanika ndani ya ndegena Kitengo chetu cha Kibiashara kilicho halisi.”
Abiria wa kitengo cha Biashara wanaweza kufurahia kiti cha kujitulizia chenye nafasi tele, chaguo la mlo kutoka kwa orodha ya vyakula vya kiwango vya kimataifa, ukaguzi wa mizigo kwa ukarimu na uharakishaji kupitia kwa forodha na kwa walinda usalama. Kwa ziada, abiria wa Kitengo cha Kibiashara wana ufikiaji wa manyumba ya mapokezi ya kibiashara kote kwenye mfumona timu ya Kibiashara iliyotengwa kwa masaa 24 ya kusaidia ununuzi wa nafasi za usafiri na kushughulikia maswali kote safarini.
 
Abiria wanaosafiri kwenye Kitengo cha Uchumi wanaweza kufurahia mitambo ya utumbuizaji ya ndani ya ndege iliyowekewa zaidi ya masaa 1,300 ya yaliyomo, ikijumuisha sinema, michezo na magazeti. Sehemu ya ndani ya ndege ya Boeing Sky hupunguza uchovu nadari ya kufungia mizigo yenye nafasi kuhakikisha safari ya kutamanika. Abiria wa Kitengo cha Uchumi wanaufikiaji wa vyakula kadha moto na baridi vinavyopatikana kwa kujinunulia ndani ya ndege na za kuagiza awali.

No comments:

Post a Comment