Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mara baada ya kurejea nyumbani baada ya ziara ya kikazi mjini Geneva. PICHA NA IKULU
Akiwa Geneva, Rais Kikwete ameongoza
vikao vya Jopo la Kimataifa Linalopendekeza Jinsi Dunia
inavyoweza kukabiliana na majanga yajayo ya magonjwa ya milipuko ambalo kazi yake imeungwa mkono na nchi 21 ambazo
zilichangia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola.
Miongoni
mwa mikutano ambayo Rais Kikwete ameiongoza katika Makao ya Umoja wa Mataifa
(UN) mjini Geneva ni pamoja na yeye na wanajopo wenzake kutoa maelezo kuhusu maendeleo
ya kazi yao kwa nchi ambazo zilichangia mapambano dhidi ya ugonjwa wa Ebola
katika nchi za Guinea, Liberia na Sierra Leone.
Nchi
hizo ambazo zimeunga mkono kazi ya Jopo hili katika mkutano huo ni Venezuela,
Umoja wa Ulaya (EU), Uholanzi, Finland, Shirikisho la Russia (Russian
Federation), Norway, China, Ubelgiji, India, Ujerumani, Marekani, Uswisi,
Canada, Brazil, Denmark, Uingereza, Israel, Benki ya Maendeleo ya Afrika
(AfDB), Umoja wa Afrika (AU), Benki ya Dunia (WB), Jamhuri ya Korea na Japan.
Pamoja
na kwamba wajibu mkuu wa Jopo hili siyo kuchunguza ugonjwa wa Ebola na madhara
yake, bado ugonjwa huo ni msingi mkuu wa kazi ya Jopo hilo ambalo wajibu wake
ni kutumia uzoefu wa Ebola kutoa mapendekezo ya jinsi dunia inavyoweza
kukabiliana na majanga ya magonjwa ya milipuko katika siku zijazo.
Ugonjwa
wa Ebola ambao ulilipuka katika nchi hizo tatu za Afrika Magharibi mwishoni mwa
mwaka 2013 mpaka sasa umeua watu 11,000 katika nchi hizo na kusababisha mshtuko
mkubwa duniani.
Hiyo
ilikuwa mara ya 24 kwa ugonjwa huo kulipuka katika Afrika tokea ulipolipuka kwa
mara ya kwanza mwaka 1976, miaka karibu 40 iliyopita, katika Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo (DRC) wakati huo ikiitwa Zaire.
Hata
hivyo, katika milipuko ya kwanza 23, ugonjwa huo uliua watu wachache zaidi
kuliko mlipuko wa 24.
Jopo
hilo limeambiwa kuwa tofauti na matarajio ya dunia kuwa ugonjwa huo ulikuwa
unamalizika katika nchi hizo hasa katika Liberia, umeanza kupata kasi tena na
nchi hizo tatu zinakisiwa kuwa na wagonjwa karibu 70.
Jopo
hilo lenye Wajumbe sita liliteuliwa Aprili, mwaka huu, na Katibu Mkuu wa Umoja
wa Mataifa, Mheshimiwa Ban Ki Moon na kufanya vikao vyake vya mwanzo Mei, mwaka
huu, katika makao makuu ya UN, mjini New York, Marekani.
Mbali
na kukutana na nchi zilizochangia mapambano dhidi ya Ebola, Rais Kikwete na
Jopo lake limepata nafasi ya kumsikiliza aliyekuwa Mkurugenzi wa Shirika la
Afya Duniani (WHO), Kanda ya Afrika, wakati ugonjwa huo unalipuka Dkt. Luis
Gomes Sambo wa Angola ambaye aliwaeleza wajumbe historia ya ofisi ya kanda hiyo
iliyoko mjini Brazzaville, Jamhuri ya Congo, katika kukabiliana na ugonjwa huo.
Aidha,
Wajumbe wa Jopo wamemsikiliza Mkurugenzi mpya wa Kanda, Dkt. Matshidizo Rebecca
Moeti ambaye amezungumza kwa njia ya mkutanomtandao (teleconference) kutoka
mjini Brazzaville. Dkt. Moeti alianza kazi yake Januari Mosi, mwaka huu, 2015.
Vile
vile, Wajumbe wa Jopo wamesikiliza jitihada za Jamhuri ya Rwanda kukabiliana na
magonjwa ya mlipuko kupitia kwa Waziri wa Afya wa nchi hiyo, Agnes Binagwaho
ambaye naye alizungumza kwa mkutanomtandao kutoka Kigali, Rwanda.
Nje
ya vikao hivyo, Rais Kikwete alikutana na kufanya mazungumzo na Katibu Mkuu
Mstaafu wa UN, Mheshimiwa Kofi Annan. Katika mkutano huo kwenye Hoteli ya
Intercontinental, viongozi hao wawili wamezungumzia masuala mbali mbali ya
kimataifa, ikiwamo hali ya Burundi.
Rais
pia amekutana kwa mazungumzo na Mtendaji Mkuu wa Kituo cha South Centre ambacho
kina makao yake mjini Geneva, Dkt. Martin Kohr. Kituo hicho kilianzishwa chini
ya uongozi wa Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere, kwa nia ya utekelezaji wa Ripoti
ya Kamisheni ya Nchi Zinazoendelea (South-South
Commission), ambayo iliongozwa na Mwalimu.
No comments:
Post a Comment