Katibu wa uchumi na fedha wa Bukoba mjini, Mwalimu George
Rubeiuyuka aliyetangaza mapema nia yake ya kuwania kiti cha ubunge katika jimbo la Bukoba mjini kwa tiketi ya Chama Cha
Mapinduzi (CCM) jana (jumatano) amekuwa kada wa kwanza kuchukua fomu ya kwania
kiti cha ubunge wa jimbo hilo.
Mwalimu George ambaye nia afisa elimu vifaa na takwimu wa
wilaya ya Misenyi amechukua fomu hiyo majira ya saa 4.30 toka kwa katibu
msaidizi wa Bukoba mjini Abdul Kambuga huku akiwa ameongozana na wafuasi wachache wa
chama hicho.
Kada huyo wa CCM muda mfupi baada ya kuchukua fomu hiyo alisikika akisema kuwa hakuwania nafasi hiyo ya
ubunge wa jimbo la Bukoba mjini inayoshikiliwa na Balozi Khamis Kagasheki inayonyemelewa na makada wengine wa chama hicho kwa ushabiki.
Amesema anawania nafasi hiyo kwa dhati kwa kuwa uzoefu wa kuwaongoza
wananchi anao, uwezo wa kuwatumikia
anao, uwezo wa kukitetea chama anao na sababu nia na madhumuni ya kuwania
nafasi ya ubunge katika jimbo la Bukoba mjini anayo.
Mwalimu Rubeiyuka amesema kwa sasa ni mapema kutaja
vipaumbele vyake kwa kuwa vipaumbele
vyake vitaendana sambamba na ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 205 itayotolewa
na chama hicho.
Allichokiahidi ni kuwatumikia wananchi kwa nguvu zote, pia
amesema kuwa iwapo atachaguliwa atahakikisha anaondoa makundi yanayodumaza
maendeleo katika manispaa ya Bukoba, amesema makundi ndio chanzo cha migogoro
inayokwamisha maendeleo katika manispaa ya Bukoba.
Amewaomba wanachama wa CCM wammchague ili aweze kupeperusha
bendera ya chama hicho kikongwe nchini
kwa kuwa anao uwezo mkubwa wa kukabiliana na wawakilishi wa vyama vya
watakaoteuliwa kuwania nafasi ya ubunge ndani katika jimbo la Bukoba mjini.
Kinyanganyiro cha kumpata mwakilishi atakayepeperusha
bendera ya CCM katika jimbo la Bukoba mjini kina
ushindani mkubwa, ushindani huo unadhihirishwa na hatua ya makada wengi wa
chama hicho kujitokeza kwa wingi kuwania kiti cha ubunge katika jimbo hilo.
Baadhi ya makada ambao wanatarajia kuchukua fomu kwa lengo la kushiriki
kwenye kura za maoni za CCM ni pamoja na Meya wa zamani Anatory Amani ambaye ni
hasimu mkubwa wa mbunge wa sasa Balozi Kagasheki, Samweli Rugemalila na Joseph
Mujuni Kataraiya hali hii tofauti na vipindi vilivyopita ambapo Balozi Kagasheki
alikuwa akipita bila kupingwa.
No comments:
Post a Comment