‘Makala ya Kusisimua yenye matukio yenye hisia nzito.’
Andy Markowitz, Tovuti ya Muziki wa Filamu Music Film Web
‘Tafakari
ya kusisimua ya urafiki usio wa kawaida kati ya Kijana Mtengenezaji wa
filamu na diva wa Zanzibar mzee wa miaka 100 Zanzibar diva’ Garth Cartwright - mwandishi, “More Miles Than Money”Umbali mkubwa kuliko fedha”
‘Uwasilishaji wa wa nyota …iliyofifia na kuifanya ing’are upya’
Martin Mhando, Mkurugenzi ZIFF
Nilimpiga Picha Bi Kidude “I Shot Bi Kidude”, ni
makala mpya ya simulizi iliyotayarishwa na Andy Jones, mtengenezaji wa
filamu wa Uingereza ambayo itahitimisha Tamasha la Filamu la Kimataifa
hapa Zanzibar,. Watazamaji wa Zanzibar watamsikia msimulizi mwenyewe
akisimulia kwa lugha ya Kiswahili ambayo alijifunza kwa muda mfupi
matamshi kwa msaada wa wanamziki Wazanzibari Mim Suleiman na Bwana
Mohammed Issa Matona.
Kwa
kipindi cha zaidi ya miaka minne, kuanzia 2003 mpaka 2006, Andy Jones
alimfuata Bi Kidude alipokuwa akisafiri duniani. Matokeo yake ni
kupokea tuzo ya filamu AS OLD AS MY TONGUE,
ambayo ilionyeshwa kwa mara ya kwanza katika mwaka 2006 na baadaye
iliendelea kuwa kivutio kwenye matamasha ya filamu na muziki duniani
kote..
Baada
ya kutembelea Zanzibar kila mwaka kwa karibu muongo mmoja, Jones
hakuweza tena kumuona Bi Kidude kwa muda wa miaka mitatu. Katika mwezi
Agosti mwaka 2012, taarifa zilifika Uingereza zikieleza kuwa mwanamziki
kinara maarufu Africa Mashariki ametekwa nyara . Haikuchukua muda mrefu
Andy alirudi Zanzibar kupata ukweli wa taarifa .
Wiki
chache tu baada ya kisa hicho kuibuliwa kwa picha zilizopigwa na
Natalie Haarhoff kutoka Afrika ya Kusini , muimbaji mzee sana wa
kimataifa amefariki, akiwa na umri unaosemekana kuwa zaidi ya miaka mia
moja . Jones alikurupuka kutoka nyumbani kwake huko Newcastlena kufika
uwanja wa ndege wa Heathrow dadikia chache kabla ya ndege iliyopangwa
kwenda Nairobi kuondoka. Alifika kwenye mazishi ambayo yalishtua kisiwa
kizima..
“I
SHOT BI KIDUDE, ni simulizi yangu kuhusu mambo yalivyokuwa wakati wa
mwisho wa maisha ya Bi Kidude’ . Kama ilivyo kwenye simulizi nyingine ,
kuna maelezo mbalimbali kuhusu ukweli wa jambo. Kimsingi kuna vitu
vingine ambavo si rahisi kwa mgeni kuvitambua, hata hivyo ninatumaini
kuna vitu vingine haviwezi kufichika machoni . Ninaloona mimi hisia ya
kusherehekea nguvu za muziki na kufanya vitu ambavyo vinatuletea furaha
pale tunapoweza ” Andy Jones anasema.
No comments:
Post a Comment