Na Audax Mutiganzi,Bukoba +255 784 939 586
Sasa kumekucha, asiye na mwana aeleke jiwe, nimeanza makala
yangu hii kwa kutanguliza usemi huu hii
ni kwa kuwa tunatarajia kuona mengi
kufuatia mchauano mkali unaoanza wa
kuwapata wale wataopeperusha bendera za Chama Cha Mapinduzi (CCM) wakati wa uchaguzi mkuu utakaofanyika nchini
kote mwezi Octoba, mwaka huu katika ngazi za udiwani na ubunge.
Mchuano uliopo sasa ni baina
ya wale wanaotaka kuendeleza
juhudi za kutetea viti vyao vya ubunge na udiwani wanavyovishikilia kwa sasa kwa nguvu zote na wale wanaovikodolea macho
viti hivyo baada ya kuonyesha nia ya
kutaka kuviwania.
Hali hii inawachanganya sana wale ambao wanafanya kila njia
ya kutetea viti vyao kwa mara nyingine tena, ninachikielewa kiongozi ambaye
alitekeleza ahadi yake vizuri baada ya kupewa ridhaa ya uongozi na wananchi
hapaswi kuwa na wasiwasi hata wakijitokeza watu zaidi ya 1000 wanaotaka
kuchuana naye.
Ninachokielewa mimi na kukifikiri pia ni kwamba kiongozi anayepaswa
kuwa na wasiwasi pale anapojitokeza mtu anayetangaza nia ya kuchuana naye ni
yule aliyeshindwa kuwatumukia wananchi vizuri hasa kwa kukwamisha maendeleo yao
kwa maslahi yake binafsi bila kutanguliza maslahi ya wananchi.
Tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu tumeanza kuona mengi na tutaendelea
kuona mengi, hii ni kwa sababu kuna baadhi ya viongozi wanaotaka kulinda viti vyao kwa kutumia mbinu
ya kuwajenga hofu wale wamaowahisi wanataka kutangaza nia ya kuchuana nao.
Baadhi ya viongozi wamekuwa na kawaida ya kutumia maneno
makali wanapokuwa kwenye majukwaa, wengine wanathubutu kusema kuwa
watahakikisha wanawapasua vifua au
kuwavunja meno wale wote watakaojitokeza kuchuana nao, kauli hizi mara kwa mara
zimekuwa zikitafsiriwa vibaya na wananchi.
Mara nyingi binadamu huwa hawapendi kukubali matokeo na lazima
tuelewe kuwa kila siku sio siku ya jumapili, ninachotaka
kukielezea inapotokea ukapingwa tena wa mtu wako karibu au yule ambaye mnazaliwa tumbo moja ni lazima ujie kwamba kuna tatizo kwa maana
hiyo ni lazima ujitathimini ili uweze
kupata majibu ya haraka, kama unadhamilia kufanya jambo ama urudi nyuma au
usonge mbele.
Ninachokielewa nafasi za uongozi hasa zile zinazopatikana
kwa ridhaa ya wananchi hazipatikani kwa njia iliyorahisi, hapa naongelea nafasi
ya ubunge ambayo inaliliwa na watu wengi, nafasi hii sio ya kung’ang’ania, kwa
kuwa sio ajira rasmi na wala sio nafasi za urithi kwa kuwa inatokana na matakwa
ya wananchi.
Jambo linalowashangaza wananchi walio wengi ni pale
wanapomuona mbunge anamjengea chuki mtu yoyote anayejitokeza kumnyanganya tonge
mdomoni, inashangaza pale unapomuona mbunge na kwa kushirikiana na wapambe wake
wanapofikia hatua ya ya kuwatolea vitisho baadhi ya watu wanaotangaza nia ya
kuwania viti vya ubunge.
Ninachoshangaa ni kauli za baadhi ya wabunge ambao kawaida
yao uchaguliwa na wananchi kwa kutumia nguvu kubwa pale wanapotamba na
kuwaeleza wananchi kuwa hakuna mtu yoyote ambaye anaweza kupambana nao huku
akielewa wazi kwamba nafasi zao ya ubunge ziko rehani.
Katika karne ya sasa wananchi hawadanganyiki tena, hii kwa
sababu wanajua kuchambua mchele na pumba, ninachotaka kukisema ni kwamba
wananchi walio wengi sasa hawadanganywi, wanatambua haki yao hasa kwa kuwapigia
kura wabunge wanaofaa tofauti na zamani ambapo walikuwa wakichagua wabunge kwa kuongwa pombe, sukari na vijipesa vidogo.
Kwa maana hiyo mbunge anapochaguliwa anapaswa kuwajibika zaidi hasa
kwa kutetea maslahi ya waliomchagua, pale anaposhindwa kuwajibika vizuri na
akagundua mvuto wake kwa wananchi unafifia hapaswi kulazimisha hivyo hana budi
kuachia ngazi na kuwaachia wengine uwanja ili wapate nafasi ya kujimwaga,
habari ndoo hiyo, kugang’ania hakuna maana.
Katika mkoa wa Kagera ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)
baadhi ya makada wa chama hicho wameanza kuonyesha nia yao ya kushiriki kwenye
kura za maoni kuwania nafasi ya ubunge kupitia katika chama hicho.
Baadhi ya makada wa CCM ambao wameonyesha nia ya kuwania
nafasi ya ubunge kupitia katika chama hicho ni pamoja na Julius Rugemalila, Dr.
Mazima, Dr Diodorus Kamala na Kyombo wanaotaka kushiriki kwenye kura za maoni
kwa lengo la kumg’oa mbunge wa jimbo la Misenyi Asumpta Mshama.
Tukienda katika jimbo la Karagwe tunamkuta Karim Amri AmirI
anayetaka kuchuaa na mbunge wa sasa wa jimbo hiloGozibert Brandes, na katika
jimbo la Ngara tunamkuta Willison
Gashaza anayetaka kuwania nafasi ya ubunge kupitia CCM kwa lengo la kumg’oa
Ntukamazina na tukienda katika jimbo la Bukoba vijijini tunamkuta Nazir Kalamagi
anayetaka kuwania kiti cha ubunge kinachoshikililiwa na Jasson Rweikiza.
Katika jimbo la Bukoba mjini
Mwalimu George Joseph Lubaiyuka ni miongoni mwa makada wa CCM ambao
wameishaonyesha nia ya kutaka kuwania kiti cha ubunge kinachoshikiliwa na
mbunge wa sasa katika jimbo hilo Balozi Khamis Kagasheki kupitia chama hicho.
Mtangaza nia huyo ni katibu wa uchumi na fedha katika wilaya
ya Bukoba mjini, pia ni kada wa CCM wa muda mrefu na ambaye amewahi kushika
nyazifa mbalimbali ndani ya chama
hicho, baadhi ya nyazifa hizo ni pamoja
na mjumbe wa halmashauri kuu CCM wilaya ya Bukoba mjini na mkoa wa Kagera.
Nyazifa nyingine ndani ya Chama hicho mjumbe wa kamati ya
siasa ya wilaya ya Bukoba mjini na mjumbe wa mkutano mkuu wa taifa, nyazifa
ambazo aliwahi kuzishika ni pamoja na kuwa mjumbe wa kamati ya utekelezaji wa
jumuia ya wazazi wa wilaya ya Nyamagana iliyoko mkoani Mwanza, mjumbe wa kamati
tendaji wa jumuia ya wazazi na katibu elimu na uchumi na malezi wa kata ya
Pamba jijini Mwanza.
Mwalimu Lubeiyuka ni mtumishi wa serikali, ni afisa elimu
vifaa na takwimu katika halamashauri ya willaya ya Misenyi, mwalimu huyo ni
msomi mwenye shahada ya uzamili ya elimu katika masaula ya utawala, mipango na
sera ‘masters’.
Kwa sasa anaendelea kusoma shahada ya kwanza ya sheria
kupitia chuo kikuu huria nchini, mwalimu ambaye amewahi kushika nyazifa nyingi
za uongozi ambazo ni pamoja na urais wa serikali ya wanafunzi wa chuo kikuu
huria kituo cha Kagera, mjumbe wa kamati ya ushauri ya chuo kikuu huria na
waziri wa elimu wa chuo kikuu taifa.
Akitangaza vipaumbele vyake baada ya kuonyesha nia yake
Lubeiyuka anasema akibahatika kuwa mbunge wa jimbo la Bukoba mjini atahakikisha
anavunja makundi yanayochangia migogoro inayokwamisha maendeleo katika jimbo
hilo.
Amesema migogoro katika jimbo hilo katika manispaa hiyo
inayokwamisha maendeleo kuwa inachangiwa na baadhi ya wanaotaka kugang’ania
nafasi za uongozi kwa hisia kwamba wanaobuni mipango ya maendeleo
watanyang’anya tonge mdomoni.
Lubeiyuka anasema kuwa hakuna kiongozi yoyote anayeweza
kuleta maendeleo kwa juhudi zake binafsi, anasema maendeleo yanaletwa na juhudi
ya pamoja, “ukiona mtu anataka kuwaletea maendeleo wananchi maendeleo kwa
kutumia juhudi zake binafsi ujue huyo anataka kuwaweka mfukoni mwake” anasema.
Akizungumzia suala la elimu amnasema kuwa katika jimbo la
Bukoba mjini akiwa mbunge atahakikisha anachagua shule 2 za sekondari za kata,
anasema katika shule hizxo kwa kushirikiana na wadau atahakikisha anajenga
vyumba vya madarasa ya kidato cha tano na sita.
Anasema atafanya hivyo ili kuwaongezea nafasi wanafunzi
katika jimbo hilo wanaofaulu vizuri masomo yao ya kidato cha nne na kukosa
nafasi ya kujiunga na kidato cha tano kutokana na uchache wa shule za sekondari
za serikali zilizoko hapa nchini.
Lubeiyuka anasema iwapo atakuwa mbunge wa jimbo la Bukoba
mjini pia anatarajia kuanzisha mfuko wa jimbo. Anasema mfuko huo utawahudumia
zaidi watoto wanaofaulu wanaofaulu vizuri masomo yao ya elimu ya msingi ambao
wazazi wao wana uwezo mdogo kiuchumi.
Katika hatua nyingine amesema mfuko huo utasadia kuboresha
mazingira mazuri ya walimu ambapo utakuwa ukitumika kutoa zawadi kwa walimu
ambao wanafunzi wao wanafnya vizuri na utatumika kufanya kazi ya kuwazadia
wanafunzi wanaofaulu vizuri.
Mtangaza nia huyo huyo ameahidi kufanya mkakati wa
kutengeneza ajira zisizo rasmi kwa vijana zitakazowawezesha kujiajiri wenyewe
badala ya kuwa tegemezi ndani ya jamii, amesema vijana wanatengenezewa ajira
wanakuwa wanajiepusha na vitendo vinavyojiingiza ambavyo ni pamoja na uzuruuaji.
Anasema katiia jimbo la Bukoba mjini vijana wamesahalika
kabisa na ndio maana wakati mwingine unakuta wanashabikia vyama vya upinzani
ambavyo haviwezi kuwapa manufaa, anaendelea kusema kuwa katika kutengeneza
ajira ya vijana kuwa atashirikiana na wadau mbalimbali.
Lubeiyuka anasema ni vigumu kabisa mtu kutengeneza ajira ya
vijana kwa kutumia fedha ya mtu binafsi anayoitoa toka mfukoni, anasema kutengeneza ajira ya vijana
kunahitaji nguvu ya pamoja, anaendelea kusema mtu anayetengeneza ajira kwa vijana
kwa kutumia fedha yake ya mfukoni anakuwa anatengeneza chuki kwa kuwa ajira ya
fedha ya mfukoni haiwezi kumfikia kila kijana kwa maana hiyo ni lazima itolewe
kwa ubaguzi.
Ameahidi kuimarisha mshikamano ndani ya CCM, na pia ameahidi
kushirikiana na viongozi wa chama hicho katika suala zima la kutoa maamuzi
yanayohusiana na masuala ya maendeleo yanayogusa maslahi ya wananchi, anasema
yeye atakuwa na tofauti na wabunge wengine.
Mtangaza nia huyo anasema atahakikisha anatafuta ufumbuzi wa
migogoro ambayo imeikumba manispaa ya Bukoba ambayo imekwamisha miradi
mbalimbali ya maendeleo iliyokuwa inagusa maslahi ya wananchi ambayo ni pamoja
na ujenzi wa soko kuu la Bukoba, ujenzi wa standi kuu ya mabasi ya Kyakailabwa
na upimaji wa viwanja wa viwanja 5,000.
Anasema endapo akichaguliwa hataendekeza majungu, atakuwa na
chuki na hatatukana watu ,badala yake atafanya kazi ya kuwatumikia wananchi kwa
uaminifu na kwa uadilifu mkubwa hadi pale atakapowavusha,. “uwezo wa kuongoza
ninao, nia ya kuongoza ninayo na karama ya kuongoza ninayo na sina doa lolote”
anasema.
Lubeiyuka anasema kamwe hatatoa ahadi ambayo atashindwa kuitekeleza
sambamba na wabunge ambao wamepita katika jimbo la Bukoba mjini ambao
walishindwa kutimiza ahadi zao,anasema
hakuna mtu anayeweza kutamba kuwa jimbo hili amelitoa mbali, “ jimbo
hili lilikuwepo na wabunge wengi wamepita na wamefanya mengi, anayetamba kuwa
jimbo amelitoa mbali anawadanganya wananchi kwa lengo la kujitafutia
umaarufu”anasema.
Anasema siasa za
kuwalaghai wananchi kwa kitu wanachokiona kwa macho zimepitwa na wakati,
mtu mwenye nia ya kuwatumia wananchi ni
lazima atangulize ukweli ili wananchi waupime na wautolee maamuzi, “nafasi ya
ubunge haitaki majaribio” anamaliza.
Baadhi ya wananchi walioongea juu ya mtangaza nia huyo wanasema,
anafaa kuwania kito cha ubunge katika jimbo la Bukoba mjini kwa kuwa ni msomi
mzuri, mtu mwenye uelewa na mchapakazi, Idrisa Bingileki ni mkazi wa kata ya
Kashai ambaye anasema mtangaza nia huyo ndiye chaguo la wengi kulingana na hali
ya upinzani toka kwenye vyama vingine vya siasa.
Bingileki anasema jimbo la Bukoba mjini linahitaji mgombea
mwenye mvuto kama Lubeiyuka, anasema Mwalimu huyo anapendwa na lika zote,”
tumechoka na siasa za matusi zinazotolewa na baadhi ya viongozi tunaowachagua,
nafasi za ubunge sio za urithi sasa ni wakati wa kufanya mabadiliko” anasema.
“Hatudanganywi tena huu ni wakati wa kuchambua pumba na
mchele, nawashauri CCM wasifanye kosa, wakiamuangusha Mwalimu Lubeiyuka
watakuwa wanafanya kosa kubwa ambalo watalijutia, vijana wana usongo mkubwa na
wana siri kubwa wamepania kufanya maajabu katika uchaguzi wao, chonde… chonde
msituletee mgombea ambaye hauziki” anamaliza.