Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pole Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kufuatia kifo cha
Meja Jenerali Anatory Ruta Kamazima (Mstaafu) aliyefariki jana tarehe 25 Septemba,
2012 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Nimepokea
kwa mshituko na huzuni nyingi habari za kifo cha Meja Jenerali Kamazima, ni
pigo kubwa sana kwa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) na Taifa kwa ujumla” Rais amesema katika
salamu hizo.
Mchana
wa leo Rais ameitembelea familia ya marehemu nyumbani kwao Tegeta kuwafariji
wafiwa.
Marehemu
alizaliwa mwaka 1946 katika kijiji cha Maruku, Mkoani Kagera. Alijiunga na
Jeshi mwaka 1967, mara baada ya kuhitimu Chuo Kikuu mwaka 1966.
Marehemu
Kamazima amesoma kozi mbalimbali za kijeshi hapa nchini na nchi za China,
India, Uingereza na Misri na kulitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
katika ngazi mbalimbali ambapo mwaka 1989, aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Kuzuia Rushwa Tanzania,
hadi alipostaafu Juni 2003.
Rais
amemuelezea marehemu Kamazima kama mzalendo na mtu aliyeipenda na kuitumikia
nchi yake kwa weledi mkubwa, uaminifu na moyo mmoja.
“Nimemfahamu
Marehemu kwa miaka yote ya utumishi wake jeshini na serikalini kama mzalendo,
muaminifu na mwenye moyo wa kulinda nchi yake wakati wote”
amesema “Marehemu Kamazima alikua mtu wa kutumainiwa sana katika nchi yetu na
kamwe hatutamsahau kwa utumishi wake uliotukuka”.
“Tutamkumbuka
na kumuenzi siku zote, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote na tunamuombea
mapumziko mema Marehemu Kamazima. Amina”. Rais ameongeza.
Marehemu ameacha
mjane, watoto na wajukuu.
Imetolewa na:
Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu.
DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment