Wamachinga wakiwa wakiuza bidhaa zao kwenye maeneo waliyoyavamia ya manispaa ya Bukoba.
Eneo lililovamiwa na wamachinga lililo karibu na msikiti wa ijumaa.
Wamachinga wakiuza bidhaa zao kando ya barabara ielekeayo hospitali kuu ya mkoa.
Sunday, September 30, 2012
KALDINARI RUGAMBWA ENZI ZA UHAI WAKE
Mwili wa kaldinari Rugambwa utazikwa rasmi Octoba 6, Mwaka kwenye eneo la kanisa kuu la jimbo la Bukoba ambapo zaidi ya watu 40,000 wanatarajia kuhudhuria mazishi hayo.
UCHAGUZI WA CCM KATAVI
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda ambaye ni Mjumbe wa kamati Kuu ya CCM
akifungua mkutano mkuu wa Uchaguzi wa CCM wilaya za Mlele na Mpanda
mkoani Katavi kwenye Shule ya Sekondari ya Wazazi ya Milala wilayani
Mpanda, Septemba 30,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
RAIS KIKWETE AONANA NA UJUMBE WA MWAPORC IKULU, DAR ES SALAAM
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na ujumbe toka kampuni ya
Mwambani Port and Railway Corridor Company (MWAPORC) uliomtembelea leo
Septemba 29, 2012 Ikulu jijini Dar es salaam kumweleza nia yao ya kutaka
kuwekeza katika sekta ya reli.
Friday, September 28, 2012
Fw RAIS KIKWETE AAGANA NA MABALOZI WA CUBA NA IRAN
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Cuba nchini Tanzania aliyemaliza muda wake Mhe Ernesto Gomes Dias leo Septemba 28, 2012 Ikulu jijini DAr es salaam Dar es salaam.
Thursday, September 27, 2012
CHUO KIKUU cha St. AUGUSTINO CHAZINDUA MWAKA WA MASOMO
Askofu Nestory Timanywa akiendesha ibada ya uzinduzi wa mwaka wa masoko wa chuo cha Mtakatifu Francis Tawi la Bukoba liliko Nkindo.
Baadhi ya wanafunzi wa chuo cha Mtakatifu Francis.
Askofu Nestory Timanywa askofu mkuu wa jimbo la Bukoba akisikiliza mada zilizokuwa zikitolewa na wahadhiri wa chuo kikuu cha mtakatifu Augustino wakati wa uzinduzi wa mwaka wa masomo.
Askofu Kilaini asikiliza mada, kulia ni Profesa Babyegeya na katikati ni padre Mrosso.
RAIS JAKAYA KIKWETE ATUMA SALAMU ZA RAMBIRAMBI ZA KIFO CHA MEJA GENERALI KAMAZIMA
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete amemtumia salamu za pole Mkuu wa Majeshi Jenerali Davis Mwamunyange kufuatia kifo cha
Meja Jenerali Anatory Ruta Kamazima (Mstaafu) aliyefariki jana tarehe 25 Septemba,
2012 katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
“Nimepokea
kwa mshituko na huzuni nyingi habari za kifo cha Meja Jenerali Kamazima, ni
pigo kubwa sana kwa Jeshi la Wananchi wa
Tanzania (JWTZ) na Taifa kwa ujumla” Rais amesema katika
salamu hizo.
Mchana
wa leo Rais ameitembelea familia ya marehemu nyumbani kwao Tegeta kuwafariji
wafiwa.
Marehemu
alizaliwa mwaka 1946 katika kijiji cha Maruku, Mkoani Kagera. Alijiunga na
Jeshi mwaka 1967, mara baada ya kuhitimu Chuo Kikuu mwaka 1966.
Marehemu
Kamazima amesoma kozi mbalimbali za kijeshi hapa nchini na nchi za China,
India, Uingereza na Misri na kulitumikia Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ)
katika ngazi mbalimbali ambapo mwaka 1989, aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Kuzuia Rushwa Tanzania,
hadi alipostaafu Juni 2003.
Rais
amemuelezea marehemu Kamazima kama mzalendo na mtu aliyeipenda na kuitumikia
nchi yake kwa weledi mkubwa, uaminifu na moyo mmoja.
“Nimemfahamu
Marehemu kwa miaka yote ya utumishi wake jeshini na serikalini kama mzalendo,
muaminifu na mwenye moyo wa kulinda nchi yake wakati wote”
amesema “Marehemu Kamazima alikua mtu wa kutumainiwa sana katika nchi yetu na
kamwe hatutamsahau kwa utumishi wake uliotukuka”.
“Tutamkumbuka
na kumuenzi siku zote, tunamshukuru Mwenyezi Mungu kwa yote na tunamuombea
mapumziko mema Marehemu Kamazima. Amina”. Rais ameongeza.
Marehemu ameacha
mjane, watoto na wajukuu.
Imetolewa na:
Premi
Kibanga,
Mwandishi
wa Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu.
DAR ES SALAAM
RAIS KIKWETE AOMBOLEZA KIFO CHA MKURUGENZI MKUU WA KWANZA WA TAKUKURU, MEJA JENERALI (mstaafu) ANATOLI KAMAZIMA
Rais na Amiri Jeshi
Mkuu Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pole kwa mjane na ndugu wa wa Meja Jenerali
Mstaafu Anatoli Kamazima leo nyumbani
kwa marehemu Tegeta, Dar es salaam. Marehemu Kamazima, ambaye amefariki dunia usiku
wa kuamkia leo Jumatano ya Tarehe 26
Septemba, 2012 utokana na mshtuko wa moyo, alikuwa Mkurugenzi Mkuu wa kwanza wa
Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini TAKUKURU.
PINDA AAGANA NA BALOZI WA CUBA
Waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na Balozi wa Cuba nchini, Ernesto
Gomez Diaz ambaye alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijiniDar es salaam
kuaga , Septemba 26, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
UZINDUZI WA TIGO MAMA AFRIKA SARAKASI WAFANA JIJINI DAR...!!!
Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Leonard Thadeo akizungumza machache katika ufunguzi wa maonyesho ya Tigo Mama AfriKa sarakasi yanayoendelea katika ukumbi wa ukumbi wa Mancom ndani ya Centre New World Cinema Mwenge. Maonyesho hayo yanaendelea mpaka ifikapo Oktoba 4, 2012.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Tigo Tanzania Diego Gutierrez akieleza machache kwa wageni waliokuwa wamefika katika maonyesho hayo.
Mkurugenzi wa Mancom Centre, Constantine Magavilla akiwakaribisha na kuwashukuru wageni waliokuwa wamefika katika uzinduzi wa Tigo Mama Afrika Sarakari.
Moja ya michezo iliyovutia katika Tigo Mama Africa Circus inayoendelea katika ukumbi wa Mancom ndani ya Centre New World Cinema Mwenge.
Huyu kijana anauwezo wa kuendesha baiskeli ya tairi moja.
... ilikuwa ni maajabu na kweli.
Kijana mwingine alionyesha umahili wake ni huyu kama vile unavyomuona.
Michezo ya kamba nayo ilikuwa ya kuvutia.
Mchezo mwingine ulikuwa niwa kurushiana vikapu ya kutimia miguu.
Vijana wakionyesha uhodari wao wa kupaa juu.
Vijana wakiaga mara baada ya onyesho kumalizika.
Wanamuziki wa Bendi ya Inafrika nao wakiaga, kazi yao kubwa ilikuwa ni kusherehesha wakati vijana wakiendelea na onyesho.
Umati mkubwa wa watu uliojitokeza katika maonyesho hayo.
watu walipata fulsa ya kubadilisha mawili matatu. Picha zote na Cathbert Angelo Kajuna wa www.kajunason.blogspot.com
Tuesday, September 25, 2012
KIKAO CHA KAMATI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua kikao cha Kamati Kuu ya
CCM kwenye ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM mjini Dodoma
Septemba 24, 2012. Kushoto ni Rais wa Zamnzibar, Dkt. Ali Mohamed
Shein, Kulia ni Makamu mwenyekiti wa CCM (Bara) Pius Msekwa na wapili
kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Wilson Mkama. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu)
Monday, September 24, 2012
Morning Jogging In Mbeya City!
Maggid,
Subscribe to:
Posts (Atom)