Monday, May 11, 2015

WAZIRI MKUU PINDA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Mjane wa baba wa Taifa , Mama Maria Nyerere wakati alipotoa heshima za mwisho kwa mtoto wa Baba wa Taifa, marehemu  John  Nyerere Kushoto ni Makongoro Nyerere na Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Makonda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana naWaziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Jenista Mhagama baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Dodoma  Machi 11, 2015  kwa ajili ya kikao cha Bunge kinachotarajiwa kuanza Machi 12, 2015.  Katikati ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Chiku Galawa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na mzee wa Kihadzabe, Mandona katika maonyesho ya wiki ya Elimu kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Dodoma Mei 11, 1015. Kulia ni Bibi Agnes Israel.  (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

KESI YA MAUAJI YA ALBINO AARON NONGO YAANZA KUSIKILIZWA TENA





 KESI ya mauaji ya Aaron Nongo mwenye ulemavu wa ngozi (albino) imeanza kusikilizwa tena leo hii kwenye Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza baada ya kusimama kwa miezi takriban mitano.
 
Shauri hilo namba 213 la mwaka 2014 liko mbele ya Jaji Robert Makaramba, ambaye ndiyo kwanza ameanza kulisikiliza baada ya jaji wa awali, Ashery Sumari, kupewa uhamisho.
Washtakiwa katika kesi hiyo walikuwa watano, lakini leo hii mahakama imearifiwa kwamba mmoja – Paulo Budeba Genji maarufu kama Lumalija – alifariki dunia Novemba 22, 2014 katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza, Sekou Toure, wakati akiwa mahabusu.

Taarifa hiyo ilitolewa na kiongozi wa mawakili wa upande wa mashtaka, Emil Kiria, ambaye aliiomba mahakama, akirejea Kifungu cha 284 (a) cha Sheria ya Mwenendo wa Makosa ya Jinai, kwamba inapotokea hali kama hiyo mashtaka dhidi ya mtu huyo yanafikia kikomo, ombi ambalo lilikubaliwa na mahakama.

Washtakiwa waliobakia kwenye kesi hiyo ni Chacha Jeremia, Mathew Jeremia Mlimi, Paschal Lugoye Mashiku na Alex Joseph maarufu kama Bugwema Silola Jangalu.
Kesi hiyo ambayo inaendelea tena kesho katika Mahakama Kuu Kanda ya Mwanza, iko katika hatua ya ushahidi ambapo shahidi wa sita wa upande wa mashtaka atatoa ushahidi wake.

Leo hii mashahidi wawili wametoa ushahidi wao na kufanya idadi ya mashahidi waliokwishatoa ushahidi wao kufikia watano mpaka sasa.
Marehemu Nongo aliuawa Juni 26, 2009 majira ya saa tatu usiku akiwa nyumbani kwake Ibanda Relini, jijini Mwanza ambapo wauaji hao walimkata usoni na kisha kumkata miguu yake yote miwili na kutoweka nayo pamoja na meno mawili ya mbele.
 ​

PINDA AFUNGUA KONGAMANO LA LIONS CLUB

  Baadhi ya washiriki wa kongamano la 12 la Lions Club wakimsikiliza Wairi Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipofungua  kongamano hilo kwenye hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam Mei 9, 2015. (picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akihutubia mkutano wakati alipofungua kongamano la 12 la Lions Club kwenye hoteli ya White Sands jijini Dar es salaam  Me 9, 2015. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Sunday, May 10, 2015

WAZIRI MKUU AISHUKURU LIONS CLUB KWA MISAADA YAKE



WAZIRI MKUU Mizengo Pinda ameishukuru taasisi ya Kimataifa ya Lions Club kwa misaada ambayo imekuwa ikiitoa hapa nchini katika nyanja za afya, utunzaji mazingira na uokoaji wakati wa maafa.

Akifungua kongamano la 12 la mwaka linalojumuisha wadau wote wa Lions Club District 411 leo asubuhi (Jumamosi, Mei 9, 2015), Waziri Mkuu alisema anawashukuru wana Lions wote kwani miradi mingi wanayoifanya huwa ni kwa kujitolea tu.

“Serikali itaendelea kushirikiana na taasisi hii kwani kwa sehemu kubwa wanachokifanya ni kile ambacho sisi kama Serikali tulipaswa tukifanye. Wanatoa huduma bure za macho, matibabu ya moyo, wanatoa misaa ya mahema, vyandarua, vyakula pale tunapokumbwa na maafa. Wanafanya kazi nzuri,” alisema.

Akitolea mfano huduma za kijamii kama vile Heart Baby Project, Waziri Mkuu alisema: “Mradi wa Heart Baby Project umedumu kwa miaka karibu 30. Wameshawachukua watoto zaidi ya 3,000 wenye matatizo ya moyo na kuwapeleka India kuwapatia matibabu kwa gharama zao,” alisema.

“Jambo kubwa zaidi la kushukuru ni kwamba asilimia 99.5 ya watoto waliofanyiwa upasuaji, wamepona na hivyo kuweza kuokoa maisha ya watoto wetu,” alisema.

Mapema, akimkaribisha Waziri Mkuu kuzungumza na wajumbe zaidi ya 500 waliohudhuria Kongamano hilo, Mkurugenzi Mkuu wa Lions International, Raju Manwani alisema taasisi hiyo ina wanachama zaidi ya milioni 1.4 duniani waliosambaa katika nchi 210 ambao hufanya kazi kwa kujitolea.

Naye Mwenyekiti wa Lions Multiple Council, Bw. Teja Kalsi alisema wanapojiandaa kuadhimisha miaka 100 ya kuanzishwa kwa Lions Club, wamejiwekea lengo la kuhakikisha wanatoa huduma kwa watu milioni 100 kwa katika Nyanja zao nne kuu. Hivi sasa taasisis hiyo imetimiza mika 98 tangu kuanzishwa kwake.

“Uanachama ndiyo nguzo yetu kuu lakini pia tuna shauku ya kutimiza watu milioni 100 waliopata huduma zetu katika nyanja za vijana, afya na hasa huduma ya macho, utunzaji wa mazingira na kuwalisha wenye njaa. Tujielekeze huko ili tutimize kaulimbiu yetu isemayo palipo na uhitaji, mwana-lion yupo (Where there’s a need, there’s a lion),” alisema.

Kongamano hilo limehudhuriwa na washiriki kutoka Kenya, Uganda, Ethiopia, Seychelles, Sudan Kusini, India na wenyeji Tanzania.



IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,

Friday, May 08, 2015

WATANZANIA WEKEZENI KWENYE VIWANDA - PINDA



WAZIRI MKUU, Mizengo Pinda amewataka Watanzania wenye uwezo wa kifedha waangalie uwezekano wa kuanzisha viwanda hapa nchini badala ya kuendelea kuwa wachuuzi wa kuagiza bidhaa kutoka nje ya nchi na kuziuza hapa nchini.

Ametoa wito huo jana jioni (Jumatano, Mei 6, 2015) baada ya kutembelea maonyesho ya biashara ya Syria yanayoendelea kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na baadhi ya mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Tanzania pamoja na wafanyabiashara kadhaa, Waziri Mkuu Pinda alisema mtindo unaoendelea wa kuuza mazao ghafi nje ya nchi hauisaidii Tanzania kama nchi na badala yake unanemeesha viwanda na uchumi wa nchi zinazonunua mazao hayo.

“Watazania lazima wajiulize hivi bidhaa zote wanazoagiza kutoka nje ya nchi haziwezi kabisa kuzalishwa hapa nchini ili kupunguza matumizi mkubwa ya fedha za kigeni, kukuza uchumi na kuongeza ajira?,” alihoji Waziri Mkuu.

Alisema wakati umefika sasa wa Tanzania kufikiria kuanzisha mpango mahsusi wa kulinda viwanda vya ndani kwa kuweka vivutio vitakavyowashawishi wawekezaji na wafanyabiashara wa ndani na nje ya nchi kuanzisha viwanda vitakavyotumia malighafi inayozalishwa hapa nchini hatua ambayo itawafanya wafanyabiashara wasiende nje kununua bidhaa ambazo zinaweza kuzalishwa hapa nchini.

Mapema, Balozi wa Syria nchini, Mhe. Abdulmounem Annan alimweleza Waziri Mkuu kuwa nchi yake inavyo viwanda vya nguo za pamba zaidi ya 100 na pamba ghafi yote inayotumika kwenye viwanda hivyo inalimwa nchini humo.

Balozi Anan alisema yuko tayari kuandaa utaratibu utakaowawezesha wafanyabiashara, wawekezaji na viongozi wa Serikali kwenda Syria ili kukutana na wenzao kwa lengo la kujifunza na kuwashawishi waje kuwekeza Tanzania kwenye viwanda vya nguo na vya kusindika vyakula.

(mwisho)

IMETOLEWA NA
OFISI YA WAZIRI MKUU,
2 MTAA WA MAGOGONI,

Thursday, May 07, 2015

UTEKSELEZWAJI WA MRADI WA MAJI KATIKA MANISPAA YA BUKOBA UNAOGHARAMIWA NA SERIKALI YA UFARANA NA YA TANZANIA WENYE THAMANI ZAIDI YA BILIONI 31 UTAKUWA NA UWEZO WA KUZALISHA LITA MILIONI 18

Sehemu ya utekelezwaji wa mradi, hili ni eneo ambalo linajengwa tanki la kuhifadhi  maji toka kwenye chanzo cha maji cha ziwa Victoria na kuyasambaza kwenye matenki ya Kashura na Ibula, tanki hili limejengwa eneo la Bunena.
Matenki madogo ya kuchuja maji.

Baadhi ya wasimamizi wa mradi wakiwa pamoja na mmiliki wa mtandao huu ambaye ni pia ni mwakilishi wa clouds Tv na Redio Kagera, Audax Mutiganzi wa pili kutoka kushoto, Wa kwanza kushoto ni mhandisi Thomas George meneja wa kampuni inayofanya ukandarasi ya TECHNO FAB toka nchini India, wa pili toka kulia ni Mhandisi Fortunatus Kasimbi ambaye ni mwakilishi wa kampuni inayosimamia mradi huo ya GWK Consult ya nchini Ujerumani.

Mhandisi Kasimbi akielezea jambo wakati akionyesha eneo la chanzo  chanzo cha maji cha mradi huo


Mhandisi George akielezea namna maji yatavyochujwa wakati akionyesha chumba ambacho zitafungwa mashine za kuchuja maji.



Huu ndio mtamba utakaoongoza machine zote za kuchunja, kusukuma na kusambaza maji kwenye matenki, mtambo huu ni wa kielekronic pia utatumika kujua habari za matatizo ya kiufundi kwenye mitambo.
Wahandisi, Thomas na Kasimbi wakijadili jambo, walikuwa ndani ya chumba cha mtambo maalumu wa kuendesha mashine.


Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya maji katika mji wa Bukoba (BUWASA) akielezea hali ya upatikanaji wa maji hatika mji huo, anasema kuwa mahitaji ya maji katika mji wa Bukoba ni lita milioni 14 kwa siku wakati uzalishaji wa maji kwa sasa ni lita milioni 8 kwa siku, anasema kuwa mradi huo utasaidia kupunguza mahitaji ya maji katika mji huo.