Tuesday, December 17, 2013

MANISPAA YA BUKOBA YAENDELEA KUWAKA MOTO

Hii inafuatia hatua ya baadhi ya madiwani wanaoongozwa na waziri wa maliasili na utalii, Balozi Khamis Kagasheki wanaotaka kumg'oa madarakani mstahiki Meya wa manispaa ya Bukoba, Anatory Amani ya kuandika barua ya kutokuwa na imani ya ofisi ya mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali ambayo iliwasilishwa kwa mkurugenzi mtendaji wa manispaa hiyo.

Kwa mujibu taarifa madiwani hao wanadai kuwa mkaguzi huyo wa hesabu za serikali anachelesha kusoma taarifa ya tuhuma za matumizi mabaya ya madaraka zinazomkabili kwa lewngo la kumlinda, madiwani hao chini ya mwavuli wa Balozi Kagasheki wameishaunda mikakati ya mikali ya kumg'oa Meya huyo hata kama mapungufu ya tuhuma zinazoelekezwa kwake hazitabainika.

PINDA AWEKA JIIWE LA MSINGI LA UJENZI WA BARABARA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kiweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya  Jendelecheju- Kaebona na Koani- Jumbi mkoa wa Kusini  Unguja Desemba 17, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu

Monday, December 16, 2013

Jaribio la mapinduzi latibuliwa Sudan.K


Rais Kiir anasema jaribio la mapinduzi lilipangwa na Riek Machar aliyekuwa makamu wake wa Rais
Rais wa Sudan Kusini Salva Kiir, anasema vikosi vyake vimefanikiwa kutibua jaribio la mapinduzi, baada ya usiku mzima wa mapigano katika mji mkuu wa nchi hiyo Juba.
Bw. Kiir, anayetoka katika kabila kubwa zaidi la wa Dinka amewatupia lawama wanajeshi wanaomtii aliyekuwa makamu wake Riek Machar, anayetoka katika kabila dogo la Nuer.
Aidha Kiir ametangaza amri ya kutotembea usiku mjini Juba na kusema serikali sasa inaudhibiti mji huo.
Makundi hasimu ya wanajeshi walipigana vikali kwa saa kadhaa na kuna ripoti za kuwepo majeruhi maelfu wakiripotiwa kukimbilia usalama wao.
Milio ya risasi sasa inaripotiwa kupungua. Kumekuwa na hali tete ya kisiasa nchini Sudan Kusini tangu mwezi Julai wakati Rais Kiir alipovunja na kuwafuta kazi mawaziri wote katika baraza lake akiwemo Makamu wa Rais Bw.Machar.

TAARIFA YA KUTATUA MGOGORO YAHAIRISHWA

Mkaguzi wa hesabu za serikali ameahirisha kwa muda kutoa taarifa ya juu tuhuma ya matumizi mabaya ya madaraka iliyokuwa imeelekezwa kwa mstahiki Meya wa manispaa ya Bukoba, Khamis Kagasheki iliyoelekezwa kwake na baadhi ya madiwani wanaompinga wanaoongizwa na waziri wa maliasili na utalii, Balozi Khamis Kagasheki.

Mkaguzi huyo wa serikali alikuwa atoe taarifa hiyo desemba 16, mwaka huu, taarifa hiyo ilikuwa itolewe na mkaguzu huyo kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Kagera.

Taarifa za kuhairishwa kwa utolewaji wa taarifa hiyo zilipatikana siku ya jumapili, kabla ya hapo  madiwani wote walikuwa wameishapatiwa barua za kuhudhuria kikao hicho maalumu kilichokuwa kimeandaliwa na ofisi za mkaguzi huyo.

Taarifa zinadai kuwa mkaguzi huyo ameaahirisha zoezi la kutoa taarifa hiyo kufuatia majukumu yaliyomkabili, hata hiyo uamzi wa kuhairisha kikao hicho umewakatisha tamaa baadgi ya wananchi katika manispaa ya Bukoba, wananchi walikuwa na shauku kubwa ya kusikia mgogoro unahitimishwa ili masuala ya maendeleo yaliyokwama katika manispaa hiyo yaendelee kutekelezwa, ambayo ni pamoja na ujenzi wa soko kuu la Bukoba na standi kuu ya mabasi.

Taarifa ambazo zimepatikana zinadai kuwa mkaguzi huyo ameahidi kutoa taarifa wakati wowote bila kueleza taarifa hiyo itatolewa siku gani.

WANAOCHANGIA KUUENEZA UGONJWA WA UNYANJANO KUKIONA CHA MOTO

 Baadhi ya waandishi wa habari mkoani Kagera wakibadilishana mawazo.
 Ndizi ambayo haijakumbana na ugonjwa wa mnyauko maarufu kwa jina la unyanjano.
 Migomba ambayo haijaathirika.
 Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe, wa pili toka kulia akiwa na baadhi ya watafiti wa kituo cha utafiti wa mazao cha Maruku.

 Mkuu wa mkoa wa Kagera, Kanali Mstaafu Fabian Massawe ameziagiza halmashauri za wilaya na manispaa katika mkoa wa Kagera kutunga sheria ndogo ndogo zitakazowabana wakulima wanaochangia kueneza ugonjwa wa unyanjano.

Ametoa agizo hilo mara baada ya kutembelea shamba la mkulima bora wa ndizi lililopo eneo la mwanzo mgumu katika wilaya ya Misenyi, amesema ugonjwa wa unyanjano unathibitiwa, amewaambia wakulima watumie mbinu bora za kilimo za kuuzuia ugonjwa huo unaoenea kwa kasi katika maeneo mbalimbali mkoani Kagera.

Amewaambia viongozi kuanzia ngazi ya kata hadi mkoa kuwafikisha mahakamani wakulima wote ambao watakuta migomba yao imeathirika, pia ameahidi kuwawajibisha watendaji wote wa serikali ambao watashindwa kusimamia zoezi la kuthibiti uginjwa wa mnyauko.
Baadhi ya watafiti, kulia Bw. Sayi Bulili na kushoto nbi Bw. Leonard Mkandala.

MATUKIO YA PICHA ZA BUNGE NA KAMATI KUU

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na  Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, bungeni mjini Dodoma  Desemba  13, 2013.

 Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji na Uwezeshaji, Dr. Mary Nagu (kushoto) na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta (kulia) wakiteta na Mbunge wa Same Mashariki, Anne Kilango Malecela, bungeni mjini Dodoma Desemba 13, 2013. (Picha a na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua  Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM, mjini Dodoma Desemba 13, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)