Baadhi ya wajumbe wa bodi ya KCU, kushoto, Bw. Baruti na Kulia ni Alexanda Ngalinda, makamu Mwenyekiti.
Mwenyekiti wa bodi ya KCU, John Binunshu kushoto na meneja mkuu wa Vedasto Ngaiza wakiteta jambo.
Baadhi ya wajumbe wa mkutano mkuu wanaowawakilisha wakulima.
Chama kikuu cha ushirika cha Kagera kimeitisha mkutano mkuu kujadili namna ya kukinusuru kufuatia kuporiomoka kwa bei ya ununuzi wa kahawa kwenye soko la dunia, mkutano huo ulikuwa na lengo la kuwaomba wajumbe kuipa baraka bodi ya chama hicho ili ikubali kuidhinisha kiasi cha shilingi bilioni 1.8 il.i zisaidie kufufua msimu wa ununuzi wa kahawa ulikuwa umesimama baada ya chama hicho kukubwa na ukata.
Wednesday, October 23, 2013
Monday, October 21, 2013
UGONJWA WA MNYAUKO WA MIGOMBA WAITESA KAGERA
TUNAPOONGELEA
mikoa ambayo imekumbana na majanga mengi hapa nchini Tanzania ambayo
yameleta athari nyingi za kijamii na kiuchumi hatupaswi kuusahau mkoa wa
Kagera.
Mkoa
wa Kagera ambao umepakana na nchi za Rwanda, Uganda na Burundi umekuwa chimbuko
la majanga mengi yanayojitokeza hapa nchini ambayo uanzia nchi jirani na
hatimaye kusambaa nchini kote.
Tunaposema
tunapoongelea suala la majanga hatupaswi kuusahau ugonjwa wa UKIMWI ambao kwa Tanzania
ulijitokeza kwa mara ya Kwanza mkoani Kagera kabla ya kusambaa nchini kote,
ulitokea nchini Uganda.
Janga la UKIMWI lilitokea nchini Uganda na
hatimaye likatinga mkoani Kagera, ugonjwa wa UKIMWI ulipoingia mkoani Kagera
kwa mara ya Kwanza ulikuwa ukiitwa jina la ‘Juliana’ .
Jina
la juliana lilitokana na mashati yaliyokuwa yamechorwa nembo ya ndege mgogoni
na kifuani yaliyokuwa yakiingizwa kwa njia ya magendo na wafanyabiashara
watanzania waliokuwa wakifanya biashara na waganda maeneo ya Rukunyu.
Janga jingine lililoukumba mkoa wa
kagera ni lile la uvamizi uliofanywa na Rais wa zamani wa Uganda Nduli Idd Amin
mwaka 1979, uvamizi huo ulileta madhara makubwa ambayo ni pamoja na vifo vya
watu wengi pia ulichangia kudumaza maendeleo ya uchumi na kijamii nchini
Tanzania.
Mbali na majanga yote hayo sasa kuna janga
jingine jipya lililojitokeza mkoani humo ambalo limeanza kuonyesha athari
nyingi ambazo ni pamoja na kiuchumi na kijamii, janga hilo sio jingine bali ni la
ugonjwa wa mnyauko wa migomba unaojulikana kwa jina maarufu kwa jina la
unyanjano.
Ugonjwa wa mnyauko umeanza kuhatarisha
usalama wa zao la ndizi ambalo ndilo zao kuu la chakula na biashara katika mkoa humo
hii inafutia hatua ya ugonjwa huo kusambaa kwa kasi ya ajabu.
Kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa unyanjano
uzalishaji wa ndizi mkoani Kagera umekuwa ukipungua kila kunapokucha, migomba
mingi mkoani humo imeathirika sana na ugonjwa huo ambao unaonekana kuwa
tishio.
Mkoani Kagera wilaya ambazo
zimeathirika zaidi kufuatia kuzuka kwa ugonjwa wa unyanjano ni pamoja na
wilaya ya Muleba, Kyerwa, Karagwe, wilaya hizi ndizo uzalisha ndizi kwa wingi ambazo uuzwa
kwenye magulio na masoko mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera, maeneo ya
mikoa mingine iliyoko hapa nchini na nje ya nchi.
Mtafiti mkuu wa chuo vha utafiti wa mazao cha maruku
Innocent Ndyetabula anaelezea athari zinazochangiwa na ugonjwa vwa mnyauko,
anasema kufuatia kuzuka kwa ugonjwa huo hali ya upatikanaji wa ndizi
kwenye masoko na magulio umekuwa mdogo sana.
Ndyetabula anasema kwa sasa kwenye magulio na
masoko mbalimbali yaliyoko mkoania Kagera bei ya ununuzi wa ndizi ni wastani wa
bei kati ya shilingi kati ya 13,000 hadi
30,000.
Anasema kabla ya kuzuka kwa ugonjwa wa mnyauko
wa migomba bei ya ununuzi wa ndizi kwenye masoko na magulio ilikuwa na wastani
wa bei kati ya shilingi 2,500 hadi 8,000 kwenye masoko na magulio na wastani
wa bei kati ya shilingi 1,000 hadi 4,000 toka kwenye mashamba ya wakulima.
Anaendelea kusema kuwa upanda kwa bei ya
ununuzi wa ndizi kwenye masoko na magulio umewafanya wakazi wa mkoa wa Kagera
waliokuwa wanaona ndizi kama chakula chao kikuu waione ndizi sawa na mama mkwe
, kwa sasa ni wahaya wachache wanaoweza kumudu bei ya sasa ya ununuzi wa
ndizi.
Ndyetabula anasema ugonjwa wa mnyauko
umewafanya wahaya wabadili fikira zao, kwa sasa wahaya wanaona vyakula
vyote vinavyoonekana mbele yao bila kufanya uchambuzi, wahaya sasa wanakula
wali, ugali na vyakula vingine ambavyo walikuwa hawavitumii hapo awali.
PROFESA TIBAIJUKA ZIARANI MULEBA KATIKA JIMBO LAKE LA KUSINI
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Profesa Anna Tibaijuka
ambaye pia ni Mbunge wa Muleba Kusini na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa
CCM yuko katika ziara ya kiaina jimboni kwake. Akidai kwamba hataki
kuwasumbua wananchi kwa matayarisho ya ujio wake, anaingia katika kijiji
kimoja baada ya kingine na kukutana na wananchi kwa matembezi ndani ya
kijiji ili ajithibitishie kwa macho kero na changamoto hizo na
kuzitafutia ufumbuzi.
Jumapili tarehe 19 oktoba ametembelea kijiji cha Bihanga kata ya Burungura na kushuhudia shule ya msingi yenye madarasa manne yaliyoezekwa kwa nyasi. Wanafunzi walimueleza adha kubwa wanayoipata wakati wa mvua. Utoro katika shule hiyo ni mkubwa kwa sababu ya mazingira mabaya. Akakaa na viongozi wa kijiji na wananchi na kuamua kuweka nguvu pamoja kujenga madarasa 4 kabla ya mwisho wa mwaka. Amesema atarejea kwenye uzinduzi wa madarasa hayo mwezi Januari.
Katika kijiji cha Kiga kata ya Rulanda Profesa Tibaijuka alipokelewa na Mwenyekiti wa Kijiji Ndugu Masud Ibrahim. Aliandamana na wanawake vijana na watoto ambao katika mda mfupi walijitokeza kwa wingi kumlaki mara baada ya kusikia ujio wake, kuteka maji katika chemchem pekee ya Nyakashengya inayotegemewa na kijiji hicho. Profesa aliteka dumu la maji kwa bibi kizee mmoja mama Mwajabu ambaye hajiwezi tena.
Kwa mila na desturi mwanamke huwezi kwenda mtoni ukarejea nyumbani bila maji kuwasaidia wasiojiweza! Hiyo ni kupoteza wakati? Profesa Anna alishuhudia uharibifu mkubwa wa chanzo hicho na ufugaji holela wa mifugo inayotoka vijiji jirani ikiwa mali ya wafugaji wakubwa.
Aidha Mwenyekiti na wanawake walimuonyesha kwa uchungu mashamba yao ya mihogo yaliyoharibiwa kabisa na makundi ya ng'ombe hao. Kijiji hicho zamani kilikuwa kinazalisha mihogo kwa biashara lakini sasa hawana hata ya kula wao wenyewe kwa sababu ya uharibifu wa mifugo.
Profesa Tibaijuka aliahidi kuleta mainjinia kuboresha chanzo cha maji na kutenga sehemu ya kuteka maji, kunywesha mifugo na kufua nguo. Kwa kuwa tayari kijiji kina mpango wa matumizi bora ya ardhi alitoa Shs laki tano kwa vijana kuunda kikosi cha ulinzi wa mashamba. Wanawake walidai wanaogopa kwenda kulima kwa sababu wanafukuzwa na kupigwa na wachungaji hao.
Waziri Tibaijuka aliagiza kuwa mifugo yote itakayokutwa katika mashamba ikamatwe na kupelekwa kwa Mkuu wa Wilaya kwa sababu wananchi walidai hawana imani na polisi.
Akipita ndani ya kijiji alitembelea yatima 2 waliomaliza darasa la saba na kujitolea kuwalipia karo wakifaulu kwenda sekondari. Aidha alitoa mchango wa kujenga darasa moja la sekondari ya Rulanda, kuezeka madarasa mawili shule ya msingi ya kijiji jirani cha Nyabule ambayo imekwama mda mrefu.
Alitoa mchango wa laki mbili na nusu kwa vikundi 4 vya wanawake ili waboreshe mtaji wao. Katika mkutano wa hadhara uliotawaliwa na ngoma hoihoi na vifijo kumpokea mbunge wao, Profesa Anna aliwaasa vijana kuwa na nidhamu na kutodanganywa na wapiga porojo na kejeli bila matendo yoyote.
Alisema vijana watambue kuwa tofauti za itikadi hazitakiwi kuleta uhasama na vurugu. Akawaeleza kuwa watambue kuwa nguvu na jeuri ya ngumi inatokana na utofauti wa vidole! Je kama vyote vingelikuwa saizi moja ngumi ingekuwa na nguvu gani? Kwa mantiki hiyo kila mmoja wetu ana mchango mkubwa katika kuleta maendeleo awe mke awe mume, awe CCM au Chadema au CUF.
Cha msingi ni kauli na hoja zake. Aliwaambia vijana wapime akili ya mtu kwa kauli na kazi zake. Mtu asiye na heshima hawezi kuleta maendeleo yoyote. Na Kiongozi anayesubiri utawala kwanza ndiyo ashughulikie matatizo ya wananchi ana faida gani?
Alisema vijana wasiyumbishwe wachambue mambo na waone nani wa kuwaongoza. CCM ina mengi ya kurekebisha lakini pia imefanya mengi. Umati ulimshangaa kwa busara na uelewa wake wa mambo na kumsikiliza kwa makini. Kero ya wanyama waharibifu wa mazao nyani tumbili na viboko alisema atazitafutia ufumbuzi haraka iwezekanavyo. Sherehe ilimalizika kwa chakula cha pamoja.
Awali Katika kata ya Gwanseli Profesa Tibaijuka alisali misa ya jumapili katika Kanisa la Kilutheri KKKT la ilemera ambapo Alitembelea shule ya ufundi yenye uwezo wa kuwafundisha wanafunzi 22 kwa mwaka vijana 10 wanajifunza useremala na wasichana 12 ushonaji na elimu ya nyumbani. Wote ni yatima na wanafadhiliwa na Swedeni. Profesa Tibaijuka alichanga lhaki mbili na nusu kuwasaidia. Aidha alitembelea dispensari ya Ilemera na kushuhudia wagonjwa kupungua baada ya mlipuko wa malaria wilayani muleba kuthibitiwa.

Zitto aenda Uswiss na Uingereza kuhusu utoroshaji wa fedha
Shirika la Kimataifa la Mtandao wa Ulaya wa Madeni
na Maendeleo, European Network on Debt
and Development (Eurodad) watafanya ziara ya kiuchunguzi kuhusu
masuala ya uwazi katika kodi katika nchi za Ulaya kuanzia tarehe 20 Oktoba
mpaka tarehe 5 Novemba mwaka 2013. Uchunguzi huo utaendeshwa na wataalamu
waliobobea wa masuala ya kodi na maendeleo. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu
za Serikali wa Bunge la Tanzania Zitto Zuberi Kabwe ameteuliwa kuongoza Jopo la
uchunguzi huo.
Eurodad ni Mtandao wa Mashirika yasiyo ya
kiserikali yapatayo 48 kutoka nchi 19 za Ulaya ambayo yanajihusisha na masuala
ya kufutia madeni nchi zilizoendelea, misaada yenye maana na kodi za haki.
Mashirika haya yamekuwa kwenye kampeni ya kupinga utoroshwaji wa fedha kupitia
ukwepaji kodi unaofanywa na mashirika ya kimataifa kwa nchi zinazoendelea.
Zitto amekuwa mmoja wa wabunge wanaosimamia hoja ya kutaka Watanzania
waliotorosha fedha kwenda nje warejeshe na kufunguliwa mashtaka. Mwaka 2012
aliwasilisha hoja binafsi Bungeni na kupitishwa kuwa Azimio la Bunge ya kutaka
uchunguzi kuhusu utoroshwaji wa fedha na kufichwa nje kama Uswiss. Kikosi Kazi
cha Serikali kutekeleza Azimio hilo la Bunge kinatarajia kuwasilisha taarifa
yake katika Mkutano wa Kumi na Sita wa Bunge. Siku ya Jumatatu tarehe 21 Oktoba
Zitto atakutana na Waziri wa Fedha wa Uswiss na maafisa wa mabenki na asasi
zisizo za kiserikali zilizopo jijini Geneva. Pia Zitto atahudhuria mkutano wa
Kamati ya Kodi ya Umoja wa Mataifa katika kampeni ya kubadili mfumo wa kodi za
kimataifa ili kuzuia unyonyaji wa nchi za Kiafrika unaofanywa na Makampuni
makubwa ya Kimataifa.
Baada ya Geneva Zitto atatembelea nchi za
Luxembourg na Brussels kabla ya kwenda Norway ambapo atamalizia ziara yake kwa
Jopo la Wataalamu wa masuala ya kodi na Maendeleo kuandika taarifa maalumu
yenye mapendekezo kuhusu kuzuia utoroshaji wa fedha kutoka Afrika.
Zitto atakwenda jijini London kutoa mada kuhusu
masuala ya kodi za kimataifa katika mkutano wa Uwazi (Open Government
Partnership). Mwenyekiti wa PAC Tanzania atafanya mazungumzo na Mwenyekiti wa
PAC Uingereza Bi Margaret Eve Hodge, Lady Hodge MBE, PC, MP kuhusu masuala mbalimbali ya ushirikiano wa
mabunge mawili na kuendeleza wito wake kwa makampuni ya kimataifa kulipa kodi
zao barani Afrika na kuacha tabia ya kutumia ‘Tax Havens’ kukwepa kodi na
kufukarisha nchi za Kiafrika.
Zitto invited to annual
OGP Summit
The Kigoma North Member of Parliament and Chairman
of the Public Accounts Committee (PAC), Hon Zitto Kabwe has been invited for
the annual Open Government Partnership (OGP) Forum which kicks off in London at
the end of the month.
The OGP Summit is a chance to promote tax and
illicit issues to new audiences, to encourage new commitments in country action
plans.
Hon Zitto, who also serves as Deputy Leader of
Official Opposition in the Parliament, will serve in the panel which will
discuss tax and illicit flows, which is among themes to be deliberated during
the summit.
The OGP is a global platform for domestic reformers
committed to making their governments more open, accountable, and responsive to
citizens. Tanzania is among countries which have signed its membership to the
OGP.
Hon Zitto has great interest on tax avoidance
through illicit transfers and last year he tabled private motions which lead to
the adoption of a Parliament Resolution compelling the government to
investigate a number of individuals who have illicitly stashed billions of
dollars abroad.
The fact finding mission will see its members
interact with UN Tax Committee, OECD, EU as well as key European governments.
They will visit a number of European cities namely Geneva, Paris, Luxembourg,
Brussels and Oslo.
Ends
Issued
by;
Parliamentary
Office of Hon. Zitto Kabwe MP
Dar es
Salaam
October
19, 2013
HUAWEI KUNUFAISHA SEKONDARI 150 ZA TANZANIA *Yachangia dola za marekani 155,000 kwa shule aliyosoma Waziri Mkuu
KAMPUNI ya Huawei ya China ina mpango wa kuzisaidia shule za sekondari 150
nchini Tanzania ili ziwe zikipata mafunzo kwa njia ya mtandao wa mawasiliano (E-Education)
kama njia ya kukabiliana na uhaba wa walimu na vitabu vya masomo.
Hayo yameelezwa jana (Jumapili, Oktoba 20, 2013) na Rais wa Kampuni hiyo, Bw. William
Xu alipofanya mazungumzo na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye makao makuu yao jijini
Shenzhen, China.
Alisema walipokea maombi ya Serikali ili kuona jinsi
mkongo wa mawasiliano ya Taifa (NCITBB) utakavyoweza kuinua kiwango cha elimu
ya watoto wa Kitanzania kwa kiasi kikubwa. Kampuni ya Huawei ndiyo iliyojejenga
mkongo huo.
Alisema kwa kuanzia mradi huo utazihusu shule 50 ambapo
shule mbili kutoka kila mkoa zitaunganishwa kwenye mtandao saa zote (ziko
online) zikiwa na madarasa ya kujifunzia teknolojia mpya (multimedia
classrooms), maabara ya kompyuta (computer lab), projekta, mafunzo ya kwenye mtandao
yanayofundishwa kwa njia ya video, (Online video teaching) na (online
applications).
“Shule nyingine 100 zimekwishaainishwa lakini zenyewe zitakuwa
zikipata mafunzo offline (hazitakuwa mtandaoni moja kwa moja), bali katika
awanu ya pili zinaweza kuunganishwa na kuwa online kutegemea na upatikanaji wa
intaneti na kasi yake,” alisema.
Alisema shule hizi zitakuwa zikipokea mawasiliano kutoka
kituo chao kikuu ambacho kimejengwa Dakawa, Morogoro.
Vilevile Bw. Xu alimkabidhi Waziri Mkuu hati ya makabidhiano
ya msaada wa dola za marekani 155,000 kwa ajili ya ujenzi wa ujenzi wa madarasa
mawili na vifaa vya komputa kwa shule ya msingi Kibaoni ambayo alisoma Waziri
Mkuu iliyoko wilayani Mlele, Katavi.
Akitangaza matumizi ya msaada huo, mtaalamu kutoka
kampuni ya Huawei, Bw. Moses Hella alisema msaada huo utatumika kujenga madarasa
mawili moja likiwa computer lab na jingine ni darasa la kujifunzia teknolojia
mpya (multimedia classroom), kompyuta 50, laptop tano kwa ajili ya walimu, Huawei
tablets 100 na audio system.
Kwa upande wake, Waziri Mku aliishukuru kampuni hiyo kwa kukubali
kutumia teknolojia yake katika kuendeleza elimu nchini kwa kuanzisha mfumo wa E-Education kwenye shule 50 kwa wakati
mmoja.
Aliishukuru pia kampuni hiyo kwa
kukisaidia Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Nelson Mandela cha Arusha na
kuongeza kuwa angependa kuona chuo hicho
kinakuwa cha mfano katika maeneo ya utafiti na teknolojia ya mawasiliano barani
Afrika.
Kuhusu msaada kwa shule ya msingi
Kibaoni, Waziri Mkuu aliwashukuru kwa kumuunga mkono katika kampeni yake ya
kuhakikisha amefanya kitu kuisaidia shule hiyo ambayo alisoma kati ya mwaka
1957 na 1960.
“Ninawashukuru sana kwa msaada huu.
Niliahidi kwamba kabla sijaondoka madarakani nataka nifanye jambo la ukumbusho
kwa manufaa ya jamii ya eneo lile. Kwa kweli nawashukuru sana kwa kutupatia
msaada huu naamini kuwa shule hii sasa ni ya kisasa na wanafunzi wake watakuwa na
elimu ya teknohama na siyo wa BBC (born before computers) kama mimi.
Alisema ataikabidhi hati hiyo kwa
viongozi wa Halmashauri yake ili watunze kwenye rekodi zao.
Shule ya msingi Kibaoni aliyosoma imechakaa,
eneo ilipo ni dogo sana na haifai kwa ukarabati. Ili kukamilisha azma yake, Waziri Mkuu aliomba Halmashauri ya Wilaya ya
Mlele itafute eneo jipya ili ujenzi wa shule hiyo ukikamilika, wanafunzi
walioko katika shule hiyo wahamie kwenye shule mpya. Hadi sasa madarasa 12
yamekwishajengwa na kuezekwa.
Waziri Mkuu ambaye yuko katika siku ya sita ya ziara yake
ya kikazi ya siku tisa kwa mwaliko wa Serikali ya China leo asubuhi amewasili
Chengdu ambako atakuwa na mikutano mbalimbali.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
JUMATATU, OKTOBA 21, 2013
WAZIRI MKUU PINDA NCHINI CHINA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu (kushoto) wakisalimiana na
viongozi baada ya kuwasili kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa
Chengdu Shuangliu nchini China wakiwa katika ziara ya kakazi nchini humo
Oktoba 21, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu
Waziri Mkuu, Mkuu, Mizengo PInda akiondoka katika NYumba ya wageni ya Wozhou, Shenzhen tayari kwa safari ya kwenda Chendu akiwa katika ziara ya kikazi nchini China Oktoba 21, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Subscribe to:
Posts (Atom)