Tuesday, July 23, 2013

NAIBU WAZIRI AKUTANA NA WATENDAJI WA TANESCO KAGERA

 Mwenyekiti wa bodi ya TANESCO, Robert Mboma (kushoto) akiongea na watendaji wa shirika hilo wa mkoa wa Kagera.
 Baadhi ya watendaji wa TANESCO.




 Naibu waziri wa nishati na madini, George Simbachawene akiongea na watumishi wa TANESCO, kushoto ni Meneja mwandamizi wa shirika hilo wa kanda ya ziwa Joyce Ngahyoma.

MKUU WA MKOA WA KAGERA KANLI MSTAAF FABIAN MASSAWE AKIZUNGUMZA NA WANA HABARI

 
HALI YA MAANDALIZI YA MAADHIMISHO YA MASHUJAA KITAIFA JULAI 25, 2013 NA ZIARA YA MHESHIMIWA              RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA      TANZANIA           
MKOANI KAGERA

Ndugu Wananchi, kama ambavyo nimewahi kuwajulisha mara nyingi kupitia vyombo vyetu vya habari juu ya Mkoa wetu wa Kagera kupewa heshima kubwa ya kuandaa maadhimisho ya Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa kitaifa mwaka 2013, leo napenda kuwajulisha juu ya maandalizi ya maadhimisho hayo ambayo yataadhimishwa tarehe 25/07/2013 hapa mkoani kwetu katika Wilaya ya Muleba katika Kambi ya Jeshi la Wananchi Kaboya. Pia nawajulisha kuwa maadhimisho hayo yataambatana na ziara ya kikazi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkoa wa Kagera.

MAADHIMISHO YA MASHUJAA MWAKA 2013
Ndugu Wananchi, Maandalizi ya maadhimisho ya Siku ya Kumbumbu ya Mashujaa mkoani Kagera yanaendelea vizuri kamati mbalimbali za maandalizi zinatekeleza majukumu yake ya mwisho ili kufanikisha maadhimisho siku ya Alhamisi ya wiki hii tarehe 25 Julai, 2013. Kamati zinazoandaa maadhimisho hayo   ni Kamati ya Mapokezi, Usafiri na Malazi; Kamati ya Ujenzi Uwanja na Mapambo; Kamati ya Chakula na Afya; Kamati ya Ulinzi na Usalama; na Kamati ya Burudani, Habari na Uhamasishaji.

Ndugu wananchi, Kwa kiwango kikubwa maandalizi yote yamekamilika na tunatarajia kuanzia leo kupokea wageni kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya mkoa, pia nje ya nchi watakaohudhuria maadhimisho hayo.
Mkoa wetu umejipanga vizuri kuwapokea wageni wote watakofika mkoani hapa kwa ukarimu na bashasha kubwa.

Wajibu wa Wananchi
Ndugu wananchi, Napenda kutumia fursa hii kuwaomba kuwa wakarimu kwa wageni wetu  wote tunaowatarajia kuanzia leo  kwa kutekeleza majukumu yenu kama  Wanakagera kama ifuatavyo;
Ø Kila mwananchi kuhakikisha maeneo yake na mazingira yanayomzunguka yanaendelea kuwa katika hali ya usafi kama utamaduni wetu. Pia kumwajibisha mtu yeyote atakaeonekana anachafua mazingira yetu. Hili ni jukumu la kila mwananchi.
Ø Kila mwananchi kushiriki kikamilifu katika kuadhimisha Siku yenyewe ya Kumbukumbu ya Mashujaa tarehe 25 Julai, 2013   huko Kaboya Wilayani Muleba.  Kwani hatuna budi kuwakumbuka Mashujaa wetu kwa sababu ya historia ya mkoa wetu kushiriki katika vita ya kumwondoa adui aliyekuwa amevamia nchi yetu kupitia ardhi ya mkoa huu mwaka 1978 hadi 1979.
Ø Kila mwananchi kuhakikisha anaitunza amani na utulivu kama destuli ya mkoa wetu kwa wakati wote wageni wetu watakapokuwepo hapa mkoani na baada ya maadhimisho ya Mashujaa. Aidha, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa imejipanga vizuri kuhakikisha  amani na utulivu vinatawala wakati wote. Kwa mwananchi yeyote atakayeona viashiria vya uvunjifu wa amani atoe taarifa mara moja ili taarifa hizo zifanyiwe kazi mara moja.

Wajibu wa Vyombo vya Habari
Ndugu Wananchi, Vyombo vyetu vya habari vina wajibu wa kuhakikisha vinaendelea kutoa taarifa mbalimbali kwa wananchi kuhusu Maadhimisho ya Mashujaa kama ambavyo vimekuwa vikifanya kuanzia mwezi Mei, 2013.

Aidha, nawaombeni Waandishi, Wahariri na Wamiliki wa vyombo vya habari kutumia fursa hii kuutangaza mkoa wetu wa Kagera katika sekta mbalimbali za uwekezaji na fursa mbalimbali zinazopatikana katika mkoa wetu.
Vilevile nawaombeni Wamiliki wa vyombo vya habari hasa redio zetu za jamii  kutoa muda wa kutosha  katika vituo vyenu vya redio kurusha habari na matukio ya Kumbukumbu za Mashujaa papo kwa papo  (live coverage) siku ya maadhimisho ili wananchi ambao hawatapata muda wa kufika Kaboya wazipate habari hizo kupitia redio zetu za Jamii.

ZIARA YA MHE. RAIS MKOANI KAGERA
Ndugu Wananchi, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ndiye atakayekuwa mgeni Rasmi Katika Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mashujaa tarehe 25 Julai, 2013. Pia Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anatarajia kufanya ziara ya kikazi katika mkoa wetu wa Kagera.

Ndugu Wananchi, Katika ziara hiyo Mheshimiwa Rais Kikwete anatarajia kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo katika mkoa wetu kama ifuatavyo:
§  Kuweka jiwe la msingi katika ukarabati na upanuzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.
§  Kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa barabara ya kiwango cha lami ya Kagoma - Rusahunga
§  Kuweka jiwe la msingi barabara ya kiwango cha lami Kyaka hadi Bugene
§  Kufungua Jengo la Mahakama Kuu Kanda ya Bukoba.
§  Kufungua jengo la kitega uchumi la Chama Kikuu cha Ushirika (KCU Ltd)
§  Kuzindua mradi wa maji Muleba
§  Kuzindua kivuko kipya Rusumo  (Ngara) 
§  Kuzindua mradi wa usambazaji umeme vijijini Nyaishozi (Karagwe)
§  Kuzindua Wilaya Mpya ya Kyerwa

Ndugu Wananchi, Vilevile Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ataongea na wananchi kupitia mikutano mbalimbali ya hadhara katika Wilaya zetu ndani ya mkoa.

Ndugu Wananchi, nawaombeni kujitokeza kuanzia tarehe 24/07/2013 uwanja wa ndege wa Bukoba ili kumpokea Mheshimiwa Rais, pia atakapokuwa anafanya ziara katika Wilaya zetu tujitokeze kwa wingi kumsikiliza.

Mwisho; Nawatakia ushiriki mzuri katika kuadhimisha Siku ya Kumbukumbu ya Mashujaa na mapokezi mazuri ya wageni wetu hasa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Kagera: Amani na Maendeleo.
Amani na Maendeleo; Kagera.

Imetolewa na: Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe
Mkuu wa Mkoa
                             KAGERA



RAIS KIKWETENCHINI AFRIKA YA KUSINI

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijibu maswali toka kwa wanahabari wakati wa mkutano wa pamoja na waandishi wa habari mara baada ya mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation) katika jumba la wageni wa Rais la Sefako Makgatho jijini Pretoria, Afrika Kusini,  Jumamosi usiku. Kutoka kulia ni Rais wa Afrika Kusini Mhe Jacob Zuma, Rais wa Msumbiji ambaye pia ni mwenyekiti wa SADC Mhe  Armando Guebuza, Katibu Mtendajji wa SADC Dkt  Tomaz Augusto Salomão na Waziri wa Mambo ya Nje wa Namibia Netumbo Nandi-Ndaitwah

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Afrika ya Kusini leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation)
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja  na viongozi wa Jumuiya za Watanzania waishio Afrika ya Kusini leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation). Kutoka kulia ni Mwenyeiti wa Chama cha Wataalam Watanzania waishio Afrika Kusini, Dkt Hamza Mokiwa, Mwenyekiti wa Tanzania Women in Gauteng (TWIGA), Mama Scholastica Kimario, Rais Kikwete, Balozi wa Tanzania nchini Afrika ya Kusini Mhe Radhia Msuya, Kaimu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania waishio Afrika ya Kusini Bw. Deusdedit Rugaiganisa na Bw. David Mataluma, mratibu wa Vijana katika Jumuiya ya Watanzania.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiomndoka  leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation)
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Balozi wa Tanzania nchini Afrika Kusini Mhe. Radhia Msuya  leo Julai 21, 2013 jijini Pretoria, Afrika ya Kusini, muda mfupi kabla ya kurejea nyumbani baada ya kuhudhuria mkutano wa siku moja wa  Kamati ya Troika ya Siasa na Usalama ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika  (SADC Organ Troika on Politics, Defence and Security Cooperation)
PICHA NA IKULU

Wednesday, July 17, 2013

Vita vinaendelea kati ya waasi na jeshi Goma



Wapiganaji wa M23
Vita vikali vinaendelea katika wanajeshi serikali na waasi karibu na Goma, Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Msemaji wa wapiganaji wa waasi wa M23 ameiambia BBC kuwa ndege za kivita za serikali zimefanya mashambulio ya anga katika maeneo yao usiku ya kuamkia leo.
Umoja wa Mataifa kwa upande wake umesema uko tayari kutumia nguvu, kuwalinda raia ikiwa wapiganaji hao wa M23 wataingia mjini Goma.
Mapigano hayo yanatokea, huku jeshi la Umoja wa Mataifa litakalojumuisha wanajeshi elfu tatu likijiandaa kwenda eneo hilo kuwapokonya silaha wapiganaji wa waasi.
Mwaka uliopita waasi hao walijiondoa kutoka mji huo baada ya kuuteka kwa muda.
Mazungumzo ya amani kati ya wasi hao na wawakilishi wa serikali nchini Uganda yamekwama.
Raia wakikimbia mapigano Karibu na Goma
Wakati huo huo, Mashirika ya kutoka misaada ya Kibinadam yamesema kuwa zaidi ya wakimbizi elfu sabini raia wa Congo wamekimbilia nchi jirani ya Uganda, kukwepa mapigano Mashariki mwa Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.
Wapiganaji wa waasi wa Uganda nchini Congo, Allied Democratic Forces walishambulia mji wa Kamango na kusababisha mapigano makali kati yao na jeshi la serikali.
Mji huo kwa sasa unathibitiwa na jeshi la serikali.
Mwandishi wa BBC, Mark Doyle anasema mapigano hayo yanaashiria kibarua kigumu kinachoikabili jeshi la Umoja wa Mataifa litakalohusika na shughuli ya kuwapokonya wapiganaji wa waasi silaha katika eneo hilo.
Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa mjini Goma wamewekwa katika hali ya tahadhari huku mapigano hayo yakiendelea, karibu na mji huo muhimu ambao pia ni mji mkuu wa mkoa wa Kivu ya Kaskazini.

Bashir arejea nyumbani kutoka Nigeria



Omar al-Bashir akiwa kwenye mkutano wa AU
Rais wa Sudan Omar al-Bashir, ameondoka nchini Nigeria baada ya makundi ya kutetea haki za kibinadam kwenda mahakamani, kushinikiza serikali kumkamata kuhusiana na tuhuma za uhalifu wa kivita.
Afisa mmoja wa kibalozi, katika ubalozi wa Sudan nchini Nigeria, amesema rais Bashir, alirejea nyumbani Jumatatu jioni kabla ya kumalizika kwa mkutano wa Muungano wa Afrika ambao alikuwa akihudhuria.
Afisa huyo amesema, rais huyo alikuwa na majukumu mengine ambayo yalikuwa yakimsubiri nyumbani na amekanusha madai kuwa aliondoka kwa sababu ya kuongezeka kwa shinikizo za kukamatwa kwake.
Mahakama ya kimataifa ya Jinai ICC, inamtuhumu Rais Bashir kwa kuhusika na mauaji ya halaiki katika eneo la Darfur nchini Sudan.
Muungano wa Afrika umetoa wito kwa wanachama wake kutotekeleza agizo la mahakama ya ICC ya kumkamata rais huyo wa Sudan.
Viongozi hao wa AU wanasema mahakama hiyo ya ICC imekuwa ikiwalenga viongozi wa nchi za Kiafrika pekee.
Bwana Bashir alikuwa Nigeria kwa mkutano ulioandaliwa na muungano wa Afrika kuhusu afya unaokamailika baadaye leo.
Ubalozi wa Sudan umesema kuwa aliondoka kwa sababu ya majukumu mengine.
Mahakama ya kimataifa ya ICC ilitoa kibali cha kumkamata Bashir mwaka 2009, baada ya kumtuhumu kwa kufanya mauaji ya halaiki wakati wa vita vilivyodumu mwongo mmoja katika jimbo la Darfur.
Sudan haitambui mahakama ya ICC na inaituhumu kwa kuwa chombo cha nchi za kimataifa kutumiwa kukandamiza nchi za Afrika huku Muungano wa Ulaya ukitoa wito kwa nchi za Afrika kutomkamata Bashir.
Aidha Bashir alitarajiwa kutoa hotuba kwenye mkutano huo mjini Abuja, Jumatatu kulingana na vyombo vya habari nchini humo.
Lakini alipoitwa kutoa hotuba yake hakuwepo kwenye ukumbi.
Bashir alipokelewa na gwaride la jeshi Nigeria, alipowasili mjini Abuja Jumamosi. Mkutano huo unatafuta mbinu za kupambana zaidi na magonjwa ya Kifua kikuu, Ukimwi na Malaria.
Viongozi kutoka nchi nane za Afrika wanahudhuria mkutano huo.
Msemaji wa rais wa Nigeria,Reuben Abati, aliambia shirika la habari la AP kuwa Bashir alikuwa mjini Abuja kwa mwaliko wa muungano wa AU wala sio Nigeria.

MSAJILI AIAGIZA MITANDAO KAGERA KUFANYA UCHAGUZI


Msajili wa mashirika yasiyo ya kiserikali hapa nchini MICHAEL  KATEMBA ameiagiza mitandao yote ya wilaya inayoyaunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani KAGERA kuhakikisha inafanya uchaguzi ndani ya kipindi cha miezi MITATU kuanzia sasa ili iweze kupata wawakilishi watakaoshiriki katika zoezi la kuwachagua viongozi wapya wataoongoza mtandao unaoyaunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali mkoani humo (KANGONET).

Ametoa agizo hilo leo wakati wa kikao kilichowashirikisha wawakilishi wa mitandao inayoyaunganisha mashirika yasiyo ya kisekari toka katika wilaya zote zilizoko mkoani KAGERA kilichofanyika kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya BUKOBA kilichokuwa na lengo la kumaliza mgogoro uliopo kati ya mitandao ya wilaya mkoani humo na uongozi wa sasa wa KANGONET.

Agizo alilolitoa KATEMBA limekuja baada ya kuelezwa na washiriki wa kikao hicho chanzo cha mgogoro ilioko kati ya uongozi wa sasa wa KANGONET na mitandao ya wilaya inayoyaunganisha mashirika yasiyo ya kiserikali  mkoani KAGERA.

Katika kikao hicho wawakilishi wa mitandao ya wilaya kwa nyakati tofauti walimweleza , KATEMBA kuwa  mgogoro ulipo kati ya mitandao wilaya na  KANGONET  kwamba  unachangiwa na tabia  ya baadhi ya viongozi wa sasa ya  kutaka kujinufaisha kupitia katika mtandao huo na  kutokataka kuitisha mikutano na uchaguzi kwa muda mrefu.


Kwa upande wake Mwenyekiti wa KANGONET na mkurugenzi mtendaji wa shirika lisilokuwa la kiserikali (KADETFU) linalotuhumiwa kupora majukumu ya KAGONET, YUSTO MCHURUZA, katika kikao hicho amesema shirika lake la KADETFU kuwa  halina mahusiano na mtandao wa KANGONET katika utendaji wake wa kazi, amesema mambo yanayoifanya KANGONET ishindwe kuitisha mkutano wa uchaguzi kuwa ni pamoja na ukata unaokabili mtandao huo.