Tuesday, May 21, 2013

WABUNGE WA CCM WAKUTANA NA RAIS KIKWETE




Mei 19, 2013 Chama Cha Mapinduzi kilifanya kikao cha siku moja na wabunge wanaotokana na CCM, kikao hicho kilifanyika mjini Dodoma ambapo pamoja na viongozi wengine wa juu wa CCM kikao hicho kilihudhuriwa pia na Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete.

Kikao hicho kilikuwa na lengo la wabunge wa CCM na viongozi wa CCM wakiongozwa na Mwenyekiti wa Taifa wa CCM ambaye pia ni Rais na mtekelezaji mkuu wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kubadilishana uzoefu wa namna ilani ilivyotekelezwa hasa kwenye majimbo kwa kipindi cha nusu ya muhula wa miaka mitano. Baada ya kubadilishana mawazo uliwekwa mwelekeo wa namna bora ya kutekeleza ilani na ahadi mbalimbali kwa kipindi kilichobaki.

Kwahiyo kwa kifupi lengo la kikao hicho ilikuwa ni kutathimini utekelezaji wa ilani majimboni na kuangalia namna bora ya kuweka msukumo mpya na mkubwa zaidi kwa kipindi kilichobaki cha utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya CCM kwa 2010/2015, lengo likiwa kuhakikisha ilani na ahadi za CCM na wagombea wake zinatekelezwa kwa kiwango kikubwa.

Hata hivyo baada ya semina hiyo baadhi ya vyombo vya habari vimenukuu kauli inayodaiwa kutolewa na Mwenyekiti wa CCM Dr. Jakaya Kikwete kuwa ameruhusu wanaokusudia kuomba ridhaa ya CCM kugombea Urais wa 2015 kufanya kampeni.

CCM imesikitishwa na nukuu hiyo ya kupotosha ukweli wa kilichojadiliwa na hivyo tumelazimika kutoa ukweli wa kilichojiri na kujadiliwa. Ni kweli kuwa mjadala juu ya watu mbalimbali wanaotajwa au wanaojitaja kuwa na nia ya kugombea nafasi mbalimbali hasa udiwani, ubunge na Urais ulikuwepo na ulikuwa mkali.

Hata hivyo hitimisho la kikao na majumuisho ya Mwenyekiti wa CCM Taifa lilikuwa ni kukemea kwa nguvu zote pirika hizo na uvunjifu huu wa makusudi wa kanuni za Chama chetu ambazo kimsingi pirika hizi zinakigawa Chama na kuvuruga mshikamano na umoja ndani ya Chama.

Nasisitiza nukuu hiyo ya baadhi ya vyombo vya habari si sahihi na ni ya kupotosha ukweli. Inaelekea kuna kikundi cha watu wanamgombea wao wa kuchonga ambaye bila shaka anapungukiwa na sifa, hivyo wanajaribu kumuongezea sifa kwa kumlisha Mwenyekiti maneno na kuwaapa baadhi ya waandishi, uhuni huo haukubaliki.

CCM ina kanuni na taratibu zake zinazoisimamia na kuiongoza katika kufanya shughuli zake mbalimbali zikiwemo za mchakato wa kuwapata wagombea wake katika ngazi mbalimbali kuanzia shina hadi taifa.

Kanuni hizo ni pamoja na kanuni za Uteuzi wa wagombea wa CCM kuingia katika vyombo vya dola toleo la Februari, 2010 na Kanuni za uchaguzi wa CCM, toleo la 2012.

Katika Kanuni za Uchaguzi wa CCM Toleo la 2012 kanuni za jumla Ibara ya 33 inazungumzia Miiko ya kuzingatiwa wakati wa shughuli za uteuzi na uchaguzi. nanukuu“ Maadili na nidhamu ya chama katika kusimamia na kutekeleza shughuli za uchaguzi wa chama lazima kuzingatiwa na wale wote wanaohusika. Hivyo yawapasa kuelewa na kutambua kuwa;-

(1). “….wanachama wenye nia ya kugombea hawaruhusiwi kufanya kampeni ya aina yoyote kabla ya majina yao kuteuliwa na kikao kinachohusika”.

(4). “Ni mwiko kwa kiongozi au mwanachama yeyote wa CCM kuunda vikundi visivyo rasmi ndani ya chama, au kushiriki katika kampeni za uchaguzi za chini chini kinyume na ratiba ya uchaguzi na taratibu rasmi zilizowekwa”.

Ibara hiyo ya 33 kifungu kidogo cha 1 na 4 vinaweka wazi msimamo wa kikanuni wa Chama. Hivyo basi kwa mujibu wa kanuni za Uteuzi wa wagombea wa CCM kuingia katika vyombo vya dola toleo la Februari, 2010 na Kanuni za uchaguzi wa CCM, toleo la 2012 na kwa mujibu wa maagizo yaliyotolewa na kupokelewa kwenye kikao cha Mwenyekiti wa CCM Taifa na wabunge wa CCM mjini Dodoma tarehe 19/05/2013;

Ni marufuku kwa mwanachama yeyote wa CCM anayetaka kuomba CCM impe nafasi ya kugombea kwenye uchaguzi wa dola kujipitishapitisha na kuita wapiga kura na kukutana nao kinyume na kanuni za Chama. Hatua kali zitachukuliwa kwa mwana CCM yeyote atakaye kiuka agizo hili.

Lakini pia ni marufuku kwa viongozi na watendaji wa Chama kujihusisha na kuwakusanyia wapiga kura watu hao wenye nia ya kugombea kupitia CCM kwenye uchaguzi wa dola. Hatua kali zitachukuliwa dhidi ya viongozi na watendaji wote watakao kiuka agizo hili la Chama.

Tunawataka wote wenye nia, viongozi na watendaji wa CCM kuzingatia agizo hili, ili tusije laumiana mbele ya safari.



Imetolewa na;-



Nape Moses Nnauye
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi

MEYA WA MANIPAA YA BUKOBA AENDELEA KUANDAMWA



WAKATI baadhi ya madiwani wa halmashauri ya manispaa wanajiandaa kwenda mjini Dodoma kumuona waziri  mkuu Mizengo Pinda kwa lengo la kumshtaki mstahiki meya wa manispaa hiyo, Anatory Amani  nao baadhi ya wanachama wa Chama Cha Mapinduzi  (CCM) katika manispaa hiyo wameandaa mpango  kurudisha kadi za uanachama wa chama hicho kufuatia  kukerwa na kauli zinazotolewa na meya huyo mara kwa mara.

Wanachama hao wamedai kuwa meya huyo anatakiwa kujiuzulu kwa kuwa miradi yote ya maendeleo ambayo ni pamoja na ujenzi wa soko jipya na upimaji wa viwanja 5,000 kuwa anaibuni kwa maslahi yake binafsi.

Kwa nyakati tofauti wamesema kuwa wamekasirishwa na kauli zake alizozitoa wakati wa kikao cha baraza la madiwani kilichofanyika siku ya ijumaa iliyopita ya kutumia lugha ya matusi, na pia kuuelea umma kuwa mgogoro kati yak e na wananchi na baadhi ya madiwani wanaompinga umeisha.

Katika kikao hicho Amani aliwambia madiwani kuwa ameishakutana na waziri mkuu hivyo tume iliyoundwa kumchunguza haikubaini tuhuma yoyote inayomkabili.

Meya huyo alichowashangaza wananchi katika kikao hicho alisema ujenzi wa soko jipya la Bukoba utaendelea kama kawaida, walisema kauli aliyoitoa inaingili uhuru wa mahakama kwa kuwa wafanyabiashara ndani ya soko hilo walishafungua kesi ambayo inaendelea kusikilizwa na Mahakama kuu.

KAMATI KUU YA CHAMA CHA MAPINDUZI

 Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Shamsi Vuai Nahodha na Jenista Mhagama (kushoto) wakimsikiliza Mwenyekiti wa CCM. Rais  Jakaya Kikwete wakati  alipofungua mkutano wa Kamati Kuu ya CCm kwenye  ukumbi wa White House (CCM) mjini Dodoma May 21 2013 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akifungua Mkutano wa Kamati Kuu ya CCM kwenye ukumbi wa White House (CCM mjini Dodoma Maya 21, 2013. Kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa CCM , Zanzibar, Dr. Ali Mohamed Shien na Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Monday, May 20, 2013

FBI mourns loss of agents in hostage rescue training



The FBI is mourning the deaths of two special agents killed Friday during a training exercise off the coast of Virginia Beach, Virginia.
The agents, Christopher Lorek and Stephen Shaw, were assigned to the FBI's Critical Incident Response Group. The FBI said the cause of the incident is under review.
"We mourn the loss of two brave and courageous men," FBI Director Robert S. Mueller said in a statement issued Sunday.
"Like all who serve on the Hostage Rescue Team, they accept the highest risk each and every day, when training and on operational missions, to keep our nation safe. Our hearts are with their wives, children, and other loved ones who feel their loss most deeply. And they will always be part of the FBI Family."
A law enforcement official said the agents were killed while training to use a rope for landing on a ship from a helicopter.
The official said the helicopter encountered weather difficulties and the agents fell into the water rather than making a landing on the ship. The official believed winds were a factor but did not know if it was raining at the time.
The official said the agents died as a result of the impact rather than drowning.
The accident took place about 12 nautical miles off shore, the official said.
Special Agent Lorek, age 41, joined the FBI in 1996. He is survived by his wife and two daughters, ages 11 and 8. Special Agent Shaw, 40, joined the FBI in 2005 and is survived by his wife; a daughter, age 3; and a son, age 1.
The Hostage Rescue Team is part of the Tactical Support Branch of the FBI's Critical Incident Response Group. It is based at the FBI Academy in Quantico, Virginia.

MAZISHI YA MWANDISHI MAARUFU WA VITABU YAANZA



Mazishi ya mwandishi maarufu wa riwaya wa Nigeria, Chinua Achebe, yameanza katika mji wa Ogidi, kusini-mashariki mwa nchi ambako ndiko alikotoka.
Chinua Achebe
Maziko yanaendelea kwa juma zima, kumkumbuka na kusherehekea maisha ya mmoja kati ya waandishi maarufu kabisa wa Afrika.
Bwana Achebe alifariki mwezi March akiwa na umri wa miaka 82.
Kongamano la waandishi, mihadhara ya wasomi na kanivali ni baadhi ya matukio katika mazishi ya wiki moja ya mwandishi Chinua Achebe.
Shughuli zitakuwa nyingi katika mji wa Ogidi alikozaliwa kusini-mashariki mwa Nigeria.
Wageni kutoka pembe zote za dunia wanatarajiwa kutoa heshima zao za mwisho kwa yule waliyemwita baba wa fasihi ya kisasa ya Afrika.
Bwana Achebe aliwakosoa viongozi wa Nigeria, hata hivo wanasiasa wengi maarufu wanatarajiwa kuhudhuria matanga yake.
Maziko yatafuata taratibu za Kikristo na utamaduni wa kabila lake la Igbo.
Chinua Achebe alikuwa maarufu kwa mtindo wake wa uandishi ambao umefuata mila ya kutoa hadithi ya kabila lake la Igbo.
Kitabu cha Chinua Achebe Things Fall Apart kimetafsiriwa katika lugha zaidi ya 50.

Rais Kikwete aongoza waombolezaji katika mazishi ya Mzee Ally Kleist Sykes

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali, Rais wastaafu Alhaji Ali Hassan Mwinyi na Mzee Benjamin William Mkapa, Waziri Mkuu Mstaafu Dkt Salim Ahmed Salim, Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kianana wakiungana na mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Mzee Ally Kleist Sykes, mmoja wa waasisi wa chama cha TANU, leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2013
Jakaya Mrisho Kikwet akiongoza mamia ya waombolezaji katika mazishi ya Mzee Ally Kleist Sykes, mmoja wa waasisi wa chama cha TANU, leo katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2013


PICHA NA IKULU