Thursday, January 24, 2013

KILIMO CHA MPUNGA

Watoto  wa kijiji cha Luchili wilayani Sengerema wakiandaa shamba kwa jili ya kupanda mpunga Januari 22, 2013. Zao la Mpunga  hivi sasa linalimwa na wananchi wengi wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga kwa ajili ya chakula na Biashara. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS KIKWETE NCHINI UFARANSA

 
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa zawadi  Rais wa Seneti ya Ufaransa Mhe Jean Pierre Bel, alipotembelea makao makuu yake jijini Paris.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Rais wa Seneti ya Ufaransa Mhe Jean Pierre Bel, alipotembelea makao makuu yake jijini Paris.

Wednesday, January 23, 2013

MANGULA ASHINDWA KUMNUSURU MEYA WA MANISPAA YA BUKOBA ANATORY AMANI, MKAKATI WA KUMUENGUA WABAKIA PALEPALE

MAKAMU Mwenyekiti  wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula ameshindwa kumunusuru Meya wa manispaa ya Bukoba, Anatory Amani asienguliwe na madiwani wanaotaka kumpigia kura za kutokuwa na imani naye kulingana na utendaji wake wa kazi.

Pamoja na ushawishi mkubwa alioufanyaMangula wa kutaka kumnusuru Meya huyo  madiwani hao wameonekana kushirikia msimamo wao wa kutaka Meya huyo aachie ngazi.

Madiwani hao walionyesha msimamo wao wakati wa kikao cha dharula cha halmashauri ya kuu ya Bukoba kilichofanyika kwenye ukumbi wa mtakakatifu Francis uliko katika manispaa ya Bukoba.

Kwa mujibu wa taarifa zilizotoka ndani ya kikao hicho kilichomalizika majira ya saa 9.00 leo baadhi ya madiwani  na wajumbe wa halmashauri kuu ya Bukoba  walimkataa waziwazi  Mstahiki meya Amani kwa kuonyesha vielelezo mbele ya Philip Mangula.

Wajumbe wa halmashauri hiyo kuu walikataa uamzi wa Philip Mangula aliyetaka tume maalumu iundwe ya kuchunguza tuhuma zinazomkabili mstahiki Meya huyo.

Walimweleza Mangula kuwa kama anataka kuunda tume ya kuchinguza tuhuma zinazomkabili Amani kuwa ni lazima ahakikishe Meya huyo anaachia ofisi ili apishe uchunguzi.

Baadhi ya wajumbe wa kikao hicho walimweleza Mangula kuwa mambo anayoyafanya yanalenga kuifilisi Halmashauri ya manispaa ya Bukoba, kwa nyakati tofauti wameonyesha kutoridhishwa na matumizi ya mamilioni ya pesa yanayofanywa na meya huyo na mikataba  ya miradi anayoibuni katika manispaa hiyo.

Wamemweleza Mangula kuwa hawamtakio Meya huyo na ndio maana wanataka kumpigia kura za kutokuwa na imani naye, katika hali isiyo ya kawaida madiwani hao walikataa kutii maelekezo yaliyotolewa Mangula.

Mangula aliwataka madiwani wote 8 wa CCM  waliosaini waraka wa kutaka Meya apigiwe kura za kutokuwa na imani naye waondoe saini zao kwenye waraka huo la sivyo wangenyanganywa uanachama, madiwani hao walikataa maelekezo hayo.

Mangula aliwatishia madiwani hao kuwa madiwani ambao walisaini waraka huo ambao wangekataa kuondoa saini zao kuwa chama hicho kingewanyanganya kadi za uanachama.

Habari ambazo gazetib hili limezipata ni kwamba mchakato wa kikao cha baraza la madiwani kitakachojadili hatima ya Mstahiki Meya Amani  kitafanyika januari, 28 mwaka huu.

Meya huyo anakabiliwa na tuhuma ya kuingia mikataba mibovu wa miradi ya ujenzi wa soko kuu la Bukoba, upimaji wa viwanja, ujenzi wa jengo la kitega uchumi, Meya huyo amekuwa akituhumiwa kwa kufanya mambo kwa usiri mkubwa.

MAOFISA WA JESHI LA POLISI KAGERA AMBO NI WAKAGUZI WA TARAFA WAKABIDHIWA PIKIPIKI

 Kamanda wa jeshi la polisi mkoani Kagera, Philip Kalangi akiongea na baadhi ya maofisa wa jeshi la polisi kagera wakaguzi wa tarafa ambao wamekabidhiwa pikipiki kwa ajili ya kuhubiri dhana ya polisi jamii.
 Sehemu ya pikipiki zilizogagwiwa.
 Kamanda Kalangi akiwasha moja ya pikipiki alizozigawa.
 Maofisa wa jeshi la polisi wakizipasha moto pikipiki hizo.

Mkaguzi wa tarafa ya Nshamba na Kamachumu, inspecta msaidizi, Faustina Mwakapangala akitoa neno la shukrani kwa niaba ya waliokabidhiwa pikipiki.

WASHIKA DAU WA HABARI KAGERA WAKIBURUDIKA

Baadhi ya waandishi wa habari wakiburudika kwenye miti iliyoko nyuma ya jengo la Chama Cha Mapinduzi la mkoa wa Kagera lililoko katika manispaa ya Bukoba, kutoka kushoto ni Antidius Kalunde (Tanzania Daima), Audax Mutiganzi (Clouds Television) , mdau wa habari kagera, kutoka kulia ni Charles Mwebeya (Tanzania Broadcasting Corporation) na Angela Sebastian (Uhuru/ Mzalendo).

MBIVU AU MBICHI KATI YA BALOZI KHAMIS KAGASHEKI NA MEYA WA MANISPAA ANATORY AMANI

 Na Mwandishi wetu

LEO ndio siku itakayotoa hatima ya mgogoro ulipo kati ya Balozi Kagasheki ambaye ni mbunge wa jimbo la Bukoba mjini na Anatory Amani ambaye ni mstahiki meya wa manispaa ya Bukoba.

Halmashauri kuu ya wilaya aya Bukoba mjini (CCM) itakaa kikao cha dharura kitakachofanyika kwenye ukumbi wa mtakatifu Francis chenye lengo la kujadili hatima ya Meya Amani, katika kikao wajumbe wa halmashauri kuu ya wilaya ya Bukoba watapiga kura za kumkubali au kumkataa Meya Anatory Amani.

Umazi wa kutaka kumg'oa Meya madaraka unadaiwa kufuatia hatua yake ya kutaka kutekeleza miradi ya maendeleo ndani ya manispaa hiyo kwa maslahi yake binafsi.

Kikao hicho kitahudhuliwa na makamu mwenyekiti wa Chama  Cha Mapinbduzi taifa, Philip Magula ambaye ameishawasili mkoani Kagera tangu jana, katika hali ambayo sio ya kawaida pande zote zinazopingana kila moja ilikuwa ikitamba kuibuka mshindi katika sakata hilo.