Thursday, October 18, 2012
MPANGO WA JESHI LA POLISI LA KUWAPIMA WANANCHI KWA HIARI WACHANGAMKIWA
Mganga mkuu wa jeshi la polisi mkoani Kagera Dr. Husein Gamu, ambaye amehamasisha mpango mzima wa kuwapima vipimo vya UKIMWI kwa hiari zoezi hilo lilifanyika eneo la standi kuu ya mabasi iliyoko katika manispaa ya Bukoba na kuhudhuriwa na watu wengi hususani vijana.
Wednesday, October 17, 2012
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI ATEMBELEA BANDARI A BUKOBA NA KEMONDO
Naibu waziri wa uchukuzi Charles Tizeba akitoa maelekezo kwa maofisa wa bandari alipotembelea bandari ya Bukoba.
Meli ya mizigo ikipakia sukari ilikutwa bandari ya Bukoba.
Tibeza akiongea na wasafiri aliowakuta bandarini.
Baadhi ya wasafiri ambao walikutwa kwenye jumba la wageni lililoko bandaria ya Bukoba.
Naibu waziri akiangalia huduma zinazotolewa na meli ya Victoria.
Sehemu ya mandhari ya bandari ya Bukoba.
Naibu waziri akielezwa huduma zinazotolewa na kampuni inayomiliki meli ya Victoria.
Meli kongwe nchini ya victoria ambayo hufanya safari zake kati ya mikoa ya Mwanza na Bukoba, ilikuwa imeegeshwa bandari ya Bukoba, Naibu waziri ameutaka uongozi wa kampuni ya meli kuhakikisha unaweka mazingira mazuri kwa wasafiri ambayo ni pamoja na kuiwekea meli hiyo viyoyozi ili wasafiri waweze kuvuta hewa nzuri na pia waifanyie usafi kwenye maeneo yote.

PINDA JIJINI LONDON
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na mkewe Tunu wakiwa na Mtangazaji wa
Shirika la Habari la Uingereza BBC, Zawadi Machibya (kulia) wakati
alipozungumza na Watanzania waishio Uingereza, kwenye Ubalozi wa
Tanzania uliopo London Oktoba 16, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI MKOANI KAGERA
Mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali mstaafu Fabian Massawe akitoa taarifa kwa naibu waziri wa uchukuzi Charles Tibeza aliyefanya ziara ya siku moja mkoani Kagera.
Baadhi ya viongozi wa serikali na mamlaka ya bandari nchini wakimsikiliza Naibu waziri Tibeza.
Naibu waziri wa uchukuzi akijibu hoja za taarifa iliyotolewa na Massawe mkuu wa mkoa wa Kagera.
Massawe (Kulia) kimsikiliza kwa makini Naibu waziri Tibeza anayefuata ni mjumbe wa sekretarieti ya mkoa wa Kagera Seif Husein na kushoto ni mjumbe mwingine Fikir Kisimba.
Mhandisi wa kampuni ya ukandarasi ya CGG- MECCO JV inayojenga uwanja wa ndege wa Bukoba, Patric Kain akitoa sababu zinazokwamisha ujenzi wa uwanja wa Ndege, mhandisi huyo alishindwa kumpa taarifa sahihi Naibu waziri Tibeza.
Naibu waziri Tibeza akitoa maelekezo kwa kampuni inayofanya ya ujenzi wa uwanja wa Bukoba, waziri huyo alionyeshwa kutoridhishwa na taarifa kasi ya ujenzi wa uwanja huo.
Baadhi ya viongozi wakimsikiliza Naibu waziri Tibeza alipoyembelea uwanja wa ndege wa Bukoba.
Sehemu ya uwanja wa ndege wa Bukoba unaofanyiwa ukarabati.
Massawe akijadiliana jambo na Naibu waziri Tibeza na watendaji wengine walienda kuona hali ya ujenzi wa uwanja wa ndege wa Bukoba.

Tuesday, October 16, 2012
CHIZZA AONYESHA MAKEKE YAKE MKOANI KAGERA
WAZIRI wa ushirika, chakula na masoko Mhandisi Christopher
Chizza amewahimiza viongozi na wanachama wa vyama vya ushirika nchini kushikamana ili waweze kuendeleza na kuviimarisha vyama vya vyao badala ya kujenga dhana ya kuvididimiza.
Mhandisi Chizza aliyasema hayo jana wakati wa kikao chake na
viongozi wa serikali ya mkoa wa Kagera, uongozi wa chama cha ushirika Kagera
(KCU) na waandishi wa habari kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa
Kagera.
Katika kikao hicho alisema migongano zinazojitokeza kati ya baadhi ya wanachama wanaounda vyama ushirika na waliopewa
jukumu la kusimamia na kuongoza vyama vya ushirika kamwe haziwezi kuviimarisha
na kuviendeleza vyama vya ushirika.
Alisema kuwa duniani kote migongano ndio huwa chanzo cha
kudidimiza vyama vya ushirika, Chizza alisema ili vyama vya ushirika viweze
kuimarika na kuendelea ni lazima wana
ushirika wapendane, waaminiane na waheshimiane, “hizi ndio nguzo kuu zinazoimarisha ushirika”alisema
kwa msisitizo.
“Ndugu zangu viongozi wa KCU ninapokea barua rundo
zinazowatuhumu, nyingine zinazoelea masuala ya ubadhilifu na barua hizi zinaandikwa
na wanaushirika wenu, ila taarifa mliyonipa ya utendaji wa kazi naiona iko wazi
na inaelezea hali halisi ya utendaji kazi mzuri wa KCU, sasa sielewi hizi barua
zinaashiria kitu gani” alisema kwa msangao.
Aliuagiza uongozi wa KCU kuwawajibisha watendaji ndani ya
ushirika huo wanawaona wanajihusisha na masuala ya ubadhilifu wa mali ya
wakulima, alisema yoyote wanayemuona anajihusisha na masuala ya ubadilifu
wasiishie kumfukuza tu bali wamfikishe mahakamani ili sheria ichukue mkondo
wake.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa KCU, John Binunshu katika
taarifa yake kwa waziri huyo aliiomba serikali isitoe vibali vya kununua kahawa moja kwa moja toka kwa
wakulima kwa makampuni makubwa ambayo
ununua kahawa inayakusanywa na vyama vya ushirika moja kwa moja mnadani.
Binunshu alisema kuwa hali ya serikali kutoa vibali kwa
makampuni hayo makubwa inadhoofisha vyama vya ushirika kwa kuwa yanachangia
mnada wa kahawa kuchelewa, alisema minada ya kahawa inapochelewa vyama vya
ushirika vinakosa fedha za kuwalipa wakulima hivyo vinalazimika kununua kahawa
kwa mkopo.
Akitoa ufafanuzi juu ya kwa nini baadhi ya wanunuzi wa
kahawa wananunua kahawa kwa bei kubwa alisema, wanaonunua kahawa kwa bei kubwa
ni wale wanaonunua kahawa bila kutumia minzani, aliendelea kuwa wanunuzi hao
wananunua kahawa kwa ujazo badala ya kilo jambo ambalo linawapunja wakulima.
Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi. Ziporah Pangani alikiri kuwepo
kwa magendo ya kahawa, alisema kamati yake ya ulinzi na usalama
inalishughulikia suala hilo, alimaliza kwa kusema kuwa kamati yake imeshakamata
magari yaliyokuwa yanavusha kahawa kwa njia ya magendo na kufilisi kahawa hiyo.
MKUU WA MKOA KAGERA AMUUMBUA MBUNGE WA JIMBO LA NKENGE
Huyu ndiye mbunge wa jimbo la Nkenge Asumpta Mshama.
MKUU wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe amepinga
vikali ushauri uliotolewa mbunge wa jimbo
la Nkenge Asumpta Mshama wa kuiomba
serikali iwaruhusu wakulima wao wenyewe wajitafitie masoko wa kahawa
wanayoizalisha ndani na nje ya nchi.
Massawe amesema kamwe biashara ya kahawa haitakuwa huria
hivyo wakulima wataendelea na utaratibu uliowekwa na serikali wa kuuza kahawa
yao kwenye vyama vya ushirika na makampuni ya yaliyosajiliwa kisheria
yanayofanya kazi ya kununua kahawa toka kwao.
Mkuu huyo wa mkoa alitoa kauli hiyo wakati wa kikao cha
kamati ya ushauri ya mkoa wa Kagera kilichofanyika jana kwenye ukumbi wa mkuu
wa mkoa uliko kwenye manispaa ya Bukoba.
Alisema kuwa wakulima wanapouza kahawa kwa njia isiyo rasmi
wanakuwa wanaikosesha serikali mapato , “halmashauri za wilaya na manispaa huwa
zinanufaika na mauzo ya kahawa kwa kupata ushuru tukiruhusu biashara huria ya
kahawa tutakuwa tuaziua halmashauri za wilaya na manispaa” alisema Massawe.
“Sikubaliani na kauli ya mhemimiwa mbunge biashara ya kahawa
kamwe haitakuwa huria, na mimi naahidi titaendelea kuwashughulikia kikamilifu
wale wote wanajihusisha biashara ya magendo ya kahawa, ni lazima tuunusuru
uchumi wetu” alisema huku akishangiliwa.
Massawe alisema kamwe hatamfumbia macho mtu yoyote atakayejihusha
na magendo ya kahawa’ “Nitamshughulikia mtu yoyote bila kuangalia sura yake,
kabila na nafasi yake aliyonayo ndani ya jamii” alisema.
Aliwataka viongozi wote washirikiane ili wawezer kuwathibiti
wale wote wanajihusisha na magendo ya kahawa, alisema magendo ya kahawa
inavidhoofisha vyama vya ushirika na wakulima wanaouza kahawa yao kwa njia ya
magendo, “wakulima wanaouza kahawa kwa njia ya magendo wanapunjwa sana” alimaliza
kusema.
Subscribe to:
Posts (Atom)