Tuesday, February 24, 2015
RAIS KIKWETE AMKABIDHI H.H. THE AGA KHAN HATI YA CHUO KIKUU CHA AGA KHAN KILICHOPO DSM
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi Kiongozi wa madhehebu ya
Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana hati ya Chuo Kikuu cha Aga Khan
kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu jijini Dar es
salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsikiliza Kiongozi wa madhehebu ya
Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana akiongea baada ya kumkabidhi hati
ya Chuo Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23,
2015 Ikulu jijini Dar es salaam.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiagana na Kiongozi wa madhehebu ya
Ismailia duniani Mtukufu Aga Khana baada ya kumkabidhi hati ya Chuo
Kikuu cha Aga Khan kilichopo Dar es salaam leo February 23, 2015 Ikulu
jijini Dar es salaam.
Saturday, February 21, 2015
RAIS KIKWETE AWA MWENYEKITI MPYA WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Rais Jakaya Kikwete,Naibu Rais wa Kenya,William Rutto na maafisa
wengine wakiwa kwenye Jengo la mikutano wa kimataifa la Kenyatta
International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya wakati wa kuimba
wimbo wa taifa la Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa
nchi za Afrika Mashariki.
Kutoka kushoto ni mgeni mwalikwa,Rais wa Sudani Kusini,Salva Kiir,Rais
wa Burundi,Pierre Nkurunziza,Rais Jakaya Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru
Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni(Uganda)Rais Paul Kagame(Rwanda)na
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera
wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki.
Rais Jakaya Kikwete(kushoto)akipokea bendera ya Afrika
Mashariki(EAC)kutoka kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara
ya kumkabidhi Uenyekiti wa EAC kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo.20/2/2015
PICHA NA IKULU
wengine wakiwa kwenye Jengo la mikutano wa kimataifa la Kenyatta
International Convention Center(KICC)Nairobi,Kenya wakati wa kuimba
wimbo wa taifa la Tanzania katika mkutano wa kawaida wa 16 wa Wakuu wa
nchi za Afrika Mashariki.
Kutoka kushoto ni mgeni mwalikwa,Rais wa Sudani Kusini,Salva Kiir,Rais
wa Burundi,Pierre Nkurunziza,Rais Jakaya Kikwete(Tanzania),Rais Uhuru
Kenyatta(Kenya)Rais Yoweri Museveni(Uganda)Rais Paul Kagame(Rwanda)na
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC)Dk Richard Sezibera
wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki.
Rais Jakaya Kikwete(kushoto)akipokea bendera ya Afrika
Mashariki(EAC)kutoka kwa Rais wa Kenya,Uhuru Kenyatta ikiwa ni ishara
ya kumkabidhi Uenyekiti wa EAC kwenye mkutano wa kawaida wa 16 wa
Wakuu wa nchi za Afrika Mashariki uliofanyika leo.20/2/2015
PICHA NA IKULU
SERIKALI KUAJIRI WALIMU 35,000 - WAZIRI MKUU
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amesema Serikali imepanga kuajiri walimu
zaidi ya 35,000 kwa ajili ya shule za sekondari ili kukabiliana na
tatizo la uhaba wa walimu nchini.
Ametoa kauli hiyo jana jioni (Alhamisi, Februari 19, 2015) wakati
akizungumza na mamia ya wakazi wa kata ya Kiwere, mara baada ya
kukagua ujenzi wa maabara na kuzindua nyumba nne za walimu kwenye
shule ya sekondari ya Kiwere, tarafa ya Kalenga, wilayani Iringa.
Waziri Mkuu alisema walimu hao watagawanywa kwenye shule kulingana na
mahitaji yaliyokwishawasilishwa na kwamba watakapopata mgao wao hawana
budi kuziangalia kwanza shule zenye miundombinu iliyokamilika kama
ilivyo kwa shule hiyo.
Akifafanua kuhusu kasi ya ujenzi wa maabara Waziri Mkuu alisema: “Mkoa
mzima wa Iringa unahitaji kuwa na maabara 318 na zilizo tayari mpaka
sasa ni 108. Lakini kuna nyingine 141 ambazo zimekwishaanza kujengwa
na zimefikia hatua nzuri. Nimeambiwa katika muda mfupi ujao kutakuwa
na maabara 249 zilizokamilika,” alisema.
“RC inabidi uwasukume watu wako ili hizi 69 ambazo bado hazijaanza
kujengwa zikamilike kabla ya Juni mwaka huu kama ambavyo Mheshimiwa
Rais Jakaya Kikwete alikuwa ameelekeza. Alisema hataongeza tena muda
wa ujenzi,” aliongeza.
Alisema elimu ni sekta ya msingi ambayo Serikali imeamua kuipa umuhimu
wa kipekee na kuiweka katika moja ya maeneo sita muhimu ya kipaumbele
chini ya Mpango wa Matokeo Makubwa ya Haraka (BRN).
Waziri Mkuu aliwataka wanafunzi wa shule hiyo wasome kwa bidii na wawe
wasikivu ili waweze kufanya vizuri zaidi kwenye masomo yao.
Mapema, akitoa taarifa mbele ya Waziri Mkuu, Afisa Elimu wa Wilaya ya
Iringa, Bw. Leonard Msigwa alisema ujenzi wa nyumba hizo nne ambazo
zina pande mbili (four duplex houses) umegharimu sh. milioni 323.2.
Alisema nyumba hizo zenye vyumba vitatu vya kulala, sebule na jiko,
zina uwezo wa kubeba familia nane.
Bw. Msigwa alisema ujenzi wa nyumba ulifanywa shirika la DESWOS la
Ujerumani kwa kushirikiana na Halmashauri ya Wilaya ya Iringa pamoja
na wananchi. Pia walisaidiwa kujengewa tenki la maji na mabweni mawili
yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 112 kila moja kwa ajili ya
wasichana.
Akifafanua kuhusu hali ya ujenzi wa maabara, Afisa Elimu huyo alisema
hadi sasa wamekamilisha ujenzi wa vyumba viwili vya Kemia na Baiolojia
lakini bado viko kwenye hatua ya kupaka rangi. Alisema mfumo wa gesi
na maji umekwishafungwa ndani ya vyumba vya maabara.
“Ujenzi wa maabara hadi sasa umekwishagharimu sh. milioni 52.8/- na
katika kipindi cha Februari 2015, tumefanikiwa kutengeneza baadhi ya
samani za maabara yaani meza 24 na stuli 96 zenye thamani ya sh.
8,940,000/-,” alisema.
WAZIRI MKUU ATAKA WATANZANIA WAWE NA HOFU YA MUNGU
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka Watanzania wasikilize na kufuata
mafundisho yanayotolewa na viongozi wa dini ili Tanzania iwe nchi
yenye watu waadilifu na wenye hofu ya Mungu.
Ametoa wito huo leo mchana (Ijumaa, Februari 20, 2015) wakati
akizungumza na maelfu ya waumini na wananchi waliohudhuria ibada ya
mazishi ya Askofu Mstaafu Magnus Mwalunyungu kwenye kanisa la Moyo
Mtakatifu wa Yesu la Tosamaganga, Jimbo Katoliki la Iringa.
“Leo ni siku ya pekee ya kuwasikiliza viongozi wa dini wakituasa
tujiandae kwa maisha baada ya kifo. Tukio hili la leo litupe nguvu ya
kukubali kwamba kifo kipo licha ya kuwa hakizoeleki na kinapotokea
kinaleta simanzi kubwa,” alisema.
“Ninawasihi Watanzania wote tufuate mafundisho yanayotolewa na
viongozi wa dini zetu ili Tanzania iwe na kundi la watu wenye hofu ya
Mungu, waadilifu na wanyofu kama ambavyo mahubiri ya leo
yamesisisitiza,” alisema.
Waziri Mkuu ambaye yuko kwenye ziara ya siku tano ya kikazi mkoani
Iringa, aliamua kusitisha ziara yake siku ya leo ili aweze kushiriki
msiba huo. Pia alitoa salamu za rambirambi kwa niaba ya Rais Jakaya
Kikwete ambaye yuko Kenya kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Jumuiya
ya Afrika Mashariki.
Akitoa mahubiri kwenye ibada hiyo, Askofu Damian Dallu wa Jimbo Kuu
Katoliki la Songea alisema wanadamu wanahangaika na kuogopa kifo kwa
sababu hawajui baada ya kifo maisha yao yatakuwaje.
“Askofu Mwalunyungu ameishi kwa miaka 85 na kati ya hiyo, miaka 55
alikuwa akitumikia kama padre na kwa miaka 22 alimtumikia Mungu aakiwa
Askofu. Na hata baada ya kustaafu aliomba awe Parokopale Kidamalai
ambako alitumikia kwa miaka minne. Maisha yake yanaendana na neno
kutoka kitabu cha hekima kwamba kifo cha mwadilifu ni kupumzika kwa
starehe,” alisema.
Ibada hiyo ya mazishi ilihudhuriwa na Maaskofu wa kanisa katoliki zaidi ya 20.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
IJUMAA, FEBRUARI 20, 2015.
Friday, February 20, 2015
Thursday, February 19, 2015
KIKAO CHA KAWAIDA CHA BARAZA LA MADIWANI KATIKA HALMASHAURI YA MANISPAA YA BUKOBA
Mkuu wa mkoa wa Kagera, Mongella kiongea na madiwani ya manispaa ya Bukoba, alikuwa akitoa ufafanuzi juu ya uamzi wa mkoa kujenga chuo cha VETA katika wilaya ya Bukoba vijijini.
Baadhi ya madiwani wakimsikiliza mkuu wa mkoa.
Diwani wa kata ya Nshanbya,
Baadhi ya wakuu wa idara katika manispaa ya Bukoba walioudhuria kikao hicho.
Mwenyekiti wa CHADEMA katika manispaa ya Bukoba, Victor Sherejei (kulia) na mkuu wa kituo cha polisi kati Halima.
Subscribe to:
Posts (Atom)




