Tuesday, February 17, 2015

WALIOFANYA UBADHILIFU WA UTEKELEZAJI WA MIRADI KATIKA MANISPAA YA BUKOBA KUKIONA CHA MOTO




 
NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA
 
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kushirikiana na serikali kimeahidi kuwachukulia hatua kali za kisheria na kinidhamu viongozi wa kuchaguliwa na wananchi waliopewa jukumu la kusimamia   halmashauri ya manispaa ya BUKOBA  na baadhi ya watumishi waliofanya  ubadhilifu wa  fedha  zilizokuwa zimetengwa  kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokuwa imebuniwa katika manispaa hiyo .
 
Kauli hiyo imetolewa na NAPE NNAUYE,  katibu wa siasa itikadi na uenezi wa  taifa wa Chama Cha Mapinduzi CCM  kwenye hotuba yake aliyoitoa  kwenye maalumu mkutano wa hadhara ulifanyika kwenye uwanja wa uhuru wa kumsimika  DEONIZ MALINZI aliyeteuliwa kuwa kamanda wa jumuia ya  vijana  katika  mkoa wa KAGERA.
 
Sambamba na kauli hiyo, katibu huyo amemuagiza mkuu wa mkoa wa KAGERA , JOHN MONGELLA kuhakikisha anatafuta ufumbuzi  migogoro iliyochangia kukwamisha  miradi ya maendeleo katika manispaa hiyo iliyochangiwa na hatua ya baadhi ya  madiwani kugomea vikao vya baraza kwa zaidi ya miaka MIWILI jambo  lililodumaza maendeleo ya wananchi.
 

 
Katika mkutano huo Balozi KHAMIS KAGASHEKI  mbunge wa jimbo la BUKOBA mjini amenusha kwamba yeye sio chanzo cha migogoro iliyokwamisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo  katika manispaa hiyo bali yeye ni mtetezi wa wananchi, nao makada wa CCM,  AMIM  AHMED na PROTACE ISHENGOMA wanaeleza  namna chama hicho kilivyojipanga kuwawezesha vijana  kiuchumi huku wakiwahimiza  vijana kujiunga na vyama vya akiba na mikopo.
 

 
SADIK HASSAN ni mwenyekiti wa VIjana wa CCM wilaya ya NGARA anayewaleza vijana wajiepushe na udanganyifu unaofanywa na viongozi wa vyama vya upinzani  na kuwataka pia wasikubali kurubuniwa,  huku DIONIZ MALINZI kamanda wa vijana wa mkoa wa KAGERA akiahidi kuiimarisha jumuia ya vijana katika mkoa huo.
 

 
Mgogoro katika manispaa ya BUKOBA ulikwamisha utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo iliyokuwa imebuniwa ambayo ni pamoja na mradi wa ujenzi wa soko kuu la BUKOBA, upimaji wa viwanja ELFU tano, ujenzi wa standi kuu ya mabasi eneo la KYAKAILABWA na jingo la kitega uchumi.
 
Baadhi ya viongozi ambao ni madiwani wakiongozwa na BALOZI KAGASHEKI walipinga utekelezwaji wa miradi hiyo kwa madai kuwa ilikuwa imeghubikwa na vitendo vya ubadhilifu hali ambayo iliwagawa madiwani hadi baadhi yao wakafikia hatua ya kususia bikao.


Monday, February 16, 2015

PINDA AKAGUA DAWATI LA BEI NAFUU NA IMARA


Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua dawati  lenye ubora uliothibitishwa na Shirika la Viwango Tanzania lililouiniwa na kutengenezwa na Kampuni ya EDOSAMA HARDWARE ya jijini Dar es salaam, ofisini kwake Februari 16, 2015. Dawati hilo linalotengenezwa kwa mbao laini ambazo zimebanwa  bila kutumia misumari linakadiriwa kugharimu sh. 80,000/=. Wengine pichani  kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Eric Shigogo, Mkuu wa Idara ya Mikopo ya Benki ya TIB, Masanja Kungu, Ofisa Mazingira, Daniel Kapakala na Mkurugrnzi Msaidizi wa Kampuni hiyo,Edward Saguda. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Saturday, February 14, 2015

WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI KASHAI HATARINI KUKUMBANA NA MLIPUKO


NA AUDAX MUTIGANZ
BUKOBA

Halmashauri ya manispaa ya BUKOBA imeshauriwa  kufanya utaratibu wa kuliondoa  DAMPO liliko karibu kabisa na shule ya msingi  ya KASHAI ambalo ni makusanyo maalumu  ya taka zinazotoka ndani ya soko kuu la kata ya KASHAI ili wawaepushe wanafunzi katika shule hiyo na  magonjwa ya mlipuko pamoja na baadhi ya wanaofanyabiashara karibu na DAMPO hilo.

Baadhi  ya wananchi walioongea na  CLOUDS wamesema DAMPO kuwa DAMPO hilo linaharatisha uhai wa wananfunzi katika shule ya KASHAI na baadhi ya wananyabiashara wanaotumia maeneo yanayozunguka DAMPO hilo kuendesha shughuli mbalimbali za kuwaingizia kipato.

Wananchi hao wamesema  jambo linalohatarisha zaidi uhai wa wanafunzi ni maji ya machafu  yanayojichuja kwenye taka zinazorundikwa  kwenye  DAMPO hilo ambayo hutililika hadi kwenye maji  ya  mto ulioko karibu na eneo ya shule hiyo, maji ya  mto huo  wanafunzi katika shule hiyo huyatumia kwa matumizi  mbalimbali, hapa  baadhi ya wananchi  wanavyoeleza madhara ya uwepo na DAMPO hilo.


ERNEST BYANGWAMU ni mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya KASHAI anayekiri  kwamba  uwepo wa DAMPO hilo namna  unavyowaathiri wanafunzi katika shule hiyo hasa nyakati za mvua.


Kwa upande wake, CHIBUNU LUKIKO ambaye ni Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Manispaa ya BUKOBA,  amesema kuwa manispaa hiyo iko katika mchakato wa kuliondoa DAMPO hilo,  akizungumza kwa njia ya simu amesema  kwa sasa inatafuta eneo mbadala.


Friday, February 13, 2015

PINDA AAGANA BALOZI WA SAUDI ARABIA NCHINI

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiagana na balozi wa Saudi Arabia nchini Mhe. Hani Mominah baada ya mazungumzo yao.  Balozi huyo alikwenda ofisini kwa Waziri Mkuu  jijini Dar es salaam  Februari 13, 201 kuaga, (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akimkabidhi zawadi balozi wa Saudi Arabia Nchini, Mheshimiwa Hani Mominah  baada ya mazungumzo yao. Balozi huyo alikwenda Ofisini kwa Waziri Mkuu jijini Dar es salaam Februari 13, 2015 kuaga. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)

Tuesday, February 10, 2015

MAHAKAMA YA RUFANI NCHINI KUSIKILIZA MASHAURI ISHIRINI NA SITA KAGERA


NA MHARIRI
AUDAX MUTIGANZI +255 784 939 586/ 753 844 995





Mahakama kuu kanda ya BUKOBA imezindua kikao vya mahakama ya rufaa ambapo mashauri mbalimbali ISHIRINI na SITA   yatasikilizwa huku  mengine yakitolewa  maamuz na jopo la majaji wa mahakama hiyo, uzinduzi wa vikao hivyo umefanyika leo  kwenye viwanja vya mahakama hiyo iliyoko katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba.



Uzinduzi huo   ulienda sambamba  na gwaride maalumu lililoandaliwa na kikosi cha jeshi la polisi cha kutuliza ghasia lililokaguliwa  na jaji EDWARD RUTAKANGWA ambaye ni mwenyekiti wa  majaji watakaosikiliza mashauri yote yatakayoletwa  mbele ya mahakama ya rufaa uliudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali walioongozwa na mkuu wa mkoa wa KAGERA JOHN MONGELLA..



Akitoa  wakati wa uzinduzi huo ,CHARLES MAGESSA ambaye  msajili wa mahakama kuu kanda ya BUKOBA amesema  sambamba na kikao vya mahakama hiyo ya rufani pia mahakama  kuu kanda ya BUKOBA itakuwa  kikao kitakachoanza leo  katika vituo viwili ambavyo alivitaja kuwa ni pamoja na BUKOBA na BIHARAMULO ambapo  jumla ua mashauri ISHIRINI na SABA yatasikilizwa.





Aidha , msajili huyo  amesema mahakama hiyo imeandaa vikao hivyo kwa washirikisha wadau wakuu wa mahakama hiyo ambao aliwataja kuwa ni pamoja na jeshi la polisi na ofisi ya mwanasheria mkuu wa serikali, MAGESSA amesema  asilimia kubwa ya  wakaotoa ushahidi unaohusiana na mashauri yatakayosikilizwa kwamba wanaonyesha mwitikioa mzuri.





Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliohudhulia uzinduzi wa vikao hivyo wameshukuru hatua ya serikali ya kusogeza huduma mahakama ya rufani katika mkoa wa KAGERA, kwa nyakati tofauti wamesema kuwa uwepo wa Mahakama ya rufani katika mkoa wa KAGERA utawapa nafasi kubwa ya kutetea haki zao ambazo wakati mwingine walikuwa wakipokonywa walikuwa wakifuiata huduma ya mahakama ya rufani mkoani MWANZA.

Kabla  ya serikali kusogeza huduma ya  mahakama ya rufani mkoani KAGERA mwaka jana, wananchi walikuwa wakisafiri hadi mkoani  MWANZA kusikiliza mashauri yao, hali hiyo ilikuwa ikiwapa wakati mgumu  wananchi hao  hasa wenye kipato kidogo wakatii mwingine walikuwa wakilazimika kupoteza haki yao, wengi walikuwa wakishindwa kumudu gharama za usafiri na malazi.