Ndugu watembelea mtandao wangu kuna suala ambalo limeibuka linalohusiana na sakata la Fedha alizolipwa Father Rugemalila toka Account ya ESCROW, wengi wametoa tafsiri mbalimbali juu ya fedha ambayo ni mali halali ya Bw. Rugemalila, naomba tupeane ushauri hivi ni haki kuwawajibisha wale walipewa mgao wa fedha hiyo kama zawadi toka kwa RUGEMALILA? au mnaonaje sakata hilo lina mlengo wa masuala ya kisiasa hasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu 2015? kazi kwenu ndugu watembeleaji wa mtandao www.audax-kagera.blogspot.com.
Na mhariri
Tuesday, February 10, 2015
MKOA WA KAGERA WAJIZATITI KUTHIBITI VIFO VYA WAKINA MAMA WAJAWAZITO NA WATOTO
www.bukobawadau.blogspot.comwww.issamichuzi.blogspot.com
NA AUDAX MUTIGANZI
BUKOBA
Kamati ya huduma ya afya ya msingi katika mkoa wa KAGERA imefanya kikao cha
dharura kwa lengo la kujadili na kuweka mikakati mbalimbali yenye lengo la kupunguza
vifo vya watoto wachanga chini ya umri
wa miaka MITANO na wakina mama wajawazito.
Kikao hicho kimefanyika wilayani KARAGWE kwenye ukumbi wa hoteli ya kanisa la kiinjili la
KIRUTHERI diosisi ya KARAGWE iliyoko
katika mji wa mdogo wa KAYANGA chini ya
mkuu wa mkoa wa KAGERA, JOHN MONGELLA.
Katika kikao hicho kilichohudhuliwa na viongozi mbalimbali wa serikali katika ngazi zote, mkuu huyo wa mkoa amewaagiza wakuu wa wilaya mkoa humo katika kila vikao wanavyoviandaa vya kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo kuweka ajenda ya namna ya kudhibiti vya vifo vya watoto wachanga chini ya miaka MITANO na wakina mama wajawazito.
DKT THOMAS RUTACHUNZIBWA ni mganga mkuu wa mkoa wa KAGERA na
NEEMA KYAMBA mratibu wa huduma ya watoto na wakina mama wajawazito katika mkoa huo ni maofisa wa afya
wanaoeleza hali ya sasa ya vifo vya watoto na wakina mama.
Kwa upande wake GRANDIOSA
TIBAIJUKA ambaye ni meneja taaluma wa
mradi wa JHPIEGO unaofadhiliwa na seriikali ya MAREKANI anaishauri jamii kuchangia huduma ya afya ili
iweze kupata matibabu sahihi badala ya kutegemea sana misaada toka kwa serikalini
na wafadhili, DALI RWEGASIRA mkuu wa wilaya ya KARAGWE na DENIS
MBEO mkuu wa wa wilaya ya BIHARAMULO ni miongoni mwa wakuu wa wilaya wanaoeleza
mikakati yao ya namna ya kuthibiti vifo
vya wakina mama na watoto kwa kuwahamasisha wananchi wajiunge na mfuko wa afya ya jamii.
Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa michache hapa nchini
ambazo inafanya mikakati mikubwa ya kuhakikisha vifo vya wakina mama wajawazito
na watoto cinini ya miaka MITANO vinabaki kwenye vitabu vya historia, mkakati
wa mkoa huo ni kuihamasisha jamii namna ya kujiepusha na vifo hivyo kuanzia
ngazi ya vijiji, mtaa na vitongoji.
WAZIRI MKUU ATEMBELEA SHAMBA LAKE
waziri
Mkuu, Mizengo Pinda akiwaongoza viongozi wa Kanisa la Anglican
kutembelea malisho ya ng'ombe kwenye shamba lake lililopo Zuzu Dodoma
Februari 9, 2015. Baadhi ya viongozi hao ambao walikwenda kujifunza kwa
lengo la kuanzisha shamba linalofanana na hilo Dodoma ni Askofu Dickson
Chilongani wa Dayosisi ya Dodoma (wapili kushoto), Askofu Maimbo
Mndolwa wa Dayosisi ya Tanga (kulia kwake) na kulia ni Re. Canon,
Johnson Chinyongole ambaye ni Katibu Mkuu wa Kanisa hilo. (Picha na
Ofisi ya Waziri Mkuu)
DR KAMALA ATEMBELEA MAONYESHO YA UTALII BRUSELS
Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala akimshukuru
mwakilishi wa kampuni ya utalii ya Escape Bwana Nassri Chaouki baada ya
kutembelea banda la kampuni hiyo inayoshiriki Maonesho ya Utalii ya
Brussels. Balozi Kamala aliishukuru kampuni hiyo kwa kutangaza vivutio
vya utalii vya Tanzania.
Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala P AKIWA katika picha ya pamoja na Bwana Burt Munting Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Habari Travel ya Uganda inayoshiriki Maonesho ya Utalii ya Brussels. Balozi Kamala ameishukuru kampuni hiyo kwa kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania.
Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala P akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Masoko wa kampuni ya kutangaza utalii ya Travel Xenarjo ya Ubeligiji Bi. Dana Maes baada ya kutembelea Banda la kampuni hiyo inayoshiriki Maonesho ya Utalii ya Brussels. Kampuni hiyo imekubali kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania baada ya Balozi Kamala kuiomba kampuni hiyo kufanya hivyo.
Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala P AKIWA katika picha ya pamoja na Bwana Burt Munting Mkurugenzi wa kampuni ya utalii ya Habari Travel ya Uganda inayoshiriki Maonesho ya Utalii ya Brussels. Balozi Kamala ameishukuru kampuni hiyo kwa kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania.
Balozi wa Tanzania Ubeligiji Dr. Diodorus Buberwa Kamala P akiwa katika picha ya pamoja na Meneja wa Masoko wa kampuni ya kutangaza utalii ya Travel Xenarjo ya Ubeligiji Bi. Dana Maes baada ya kutembelea Banda la kampuni hiyo inayoshiriki Maonesho ya Utalii ya Brussels. Kampuni hiyo imekubali kutangaza vivutio vya utalii vinavyopatikana Tanzania baada ya Balozi Kamala kuiomba kampuni hiyo kufanya hivyo.
Monday, February 09, 2015
WAZIRI MKUU AZINDUA MPANGO WA KUKUZA STADI ZA KKK *Ataka AZISE zishirikishwe kikamilifu
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amezindua Mpango wa Kitaifa wa
Kukuza Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK) unaolenga kukuza viwango vya
uelewa kwa watoto wa darasa la kwanza na la pili kwa nchi nzima.
Mpango huo wa miaka mitatu ulioanza kutekelezwa 2014/2015
hadi 2016/2017 umelengwa kuwahusisha watoto wenye umri wa miaka mitano hadi 13
walio kwenye mfumo rasmi wa elimu na usio rasmi (MEMKWA).
Akizungumza na wadau wa elimu, walimu na wanafunzi
walioshiriki uzinduzi huo jana jioni (Jumamosi, Februari 7, 2015) Waziri
Mkuu Pinda alisema mpango huo ni mkubwa na umeandaliwa mahsusi kujibu
changamoto zilizojitokeza miaka ya nyuma.
Aliwataka watekelezaji wakuu wa mpango ambao ni Wizara ya
Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Ofisi ya Waziri Mkuu (TAMISEMI) pamoja na Wizara ya
Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kuhakikisha kuwa wanazishirikisha asasi
zisizo za Kiserikali ambazo zinajihusisha na masuala ya elimu.
“Kuna
mashirika mengi yasiyo za kiserikali ambayo ni chachu ya kuhimiza elimu
nchini... jaribuni kuwashirikisha sababu wao ni wadau wazuri sana wa suala hili.
Pangeni utaratibu wa kukaa na hawa wadau na kuwapa mrejesho wa mpango huu mzima,”
alisema Waziri Mkuu.
Hata
hivyo, Waziri Mkuu aliwataka wahusika wakuu wa mpango waangalie mgawanyo wa
mikoa iliyoingizwa kwenye mpango huo kwa kuzingatia kanda ili kuleta matokeo ya
mtawanyiko badala ya hali ilivyo sasa. “Nimeangalia jinsi mlivyogawa mikoa yenu,
inanipa taabu kidogo... kuna mikoa inahitaji msukumo wa pekee, mikoa ya
wadugaji, mikoa iliyoko pwani ya bahari na maziwa, yote inahitaji msukumo wa
tofauti,” alisema.
Katika
taarifa yao, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilisema mpango huo wa KKK au
LANES (Literacy and Numeracy Support Programme) unafadhiliwa na Ushirika wa Kimataifa wa
Maendeleo ya Elimu (Global Partnership for Education – GPE) na wahisani
wengine.
Wahisani hao ni pamoja na Shirika la Maendeleo la Uingereza (DFID)
kupitia mradi wa EQUIP-T unaotekelezwa katika mikoa saba ya Kigoma, Shinyanga,
Mara, Simiyu, Lindi, Dodoma na Tabora; Shirika la Umoja wa Mataifa la Maendeleo
ya Elimu kwa Mtoto (UNICEF) wanaofadhili utelekezaji wa Mpango wa LANES katika mikoa
ya Iringa, Mbeya na Njombe; na Shirika la Maendeleo la Marekani (USAID) kupitia
Mradi wa TZ-21 unaotekelezwa katika mkoa wa Mtwara.
Mapema, akisoma taarifa ya mpango huo mbele ya Waziri Mkuu, Kamishna
wa Elimu nchini, Prof. Eustella Bhalalusesa alisema mpango huo umelenga
kuongeza ufanisi katika stadi za KKK, kurahisisha kazi ya walimu wanaofundisha
watoto wa darasa la kwanza na la pili pamoja na kuongeza ushiriki wa jamii
katika kuboresha elimu na hasa ujifunzaji wa stadi za KKK.
Alisema
mpango huo utachangiwa sh. bilioni 150 ambazo zitaingizwa moja kwa moja kwenye
mfuko wa elimu kupitia Wizara ya Fedha.
Alisema maandalizi yote ya utekelezaji wa mpango huu yamekamilika ikiwa ni
pamoja na mtaala wa darasa la kwanza na darasa la pili, muhtasari wa KKK kwa
darasa la I & II, pamoja na Mwongozo wa Mwalimu wa kufundisha kusoma
kuandika na kuhesabu.
(mwisho)
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
DODOMA.
JUMAPILI, FEBRUARI 8, 2015.
Subscribe to:
Posts (Atom)