Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi kutoka kwa Wabunge Samuel Sitta na mkewe Margareth baada ya kuzindua wodi ya wanawake wajawazito wanaosubiri kujifungua katiak hospitali ya wilaya ya Urambo, Oktoba 12, 2014. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Sunday, October 12, 2014
WAZIRI MKUU PINDA WILAYANI URAMBO
Mkuu wa mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa akizungumza katika mkutano uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, Uyui Tabora Oktoba 11, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mbunge wa Urambo Mashariki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta akizungumza katika sherhe za kuzindua wodi ya wanawake wajawazito wanaosubiri kujifungua katiak hospitali ya wilaya ya Urambo, Oktoba 12, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifungua wodi ya ya wanawake wajawazito wanaosubiri kujifungua katika hospitali ya wilaya ya Urambo, Oktoba 12, 2014. Kushoto ni Mbunge wa Viti Maalum, Margareth Sitta ,,watatu kulia ni Mbunge wa Urambo Mashariki na Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta na wapili kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwansa. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu M izengo Pinda na Mbunge wa Urambo Mashariki, ambaye pia ni Waziri wa Ushirikiano wa Afrika ya Mashariki, Samuel Sitta (mwenye miwani ya jua nyuma ya Waziri Mkuu) wakikagua wodi ya wanawake wajawazito wanaosubiri kujifungua katiak hospitali ya wilaya ya Urambo, Oktoba 12, 2014. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi kutoka kwa Wabunge Samuel Sitta na mkewe Margareth baada ya kuzindua wodi ya wanawake wajawazito wanaosubiri kujifungua katiak hospitali ya wilaya ya Urambo, Oktoba 12, 2014. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea zawadi kutoka kwa Wabunge Samuel Sitta na mkewe Margareth baada ya kuzindua wodi ya wanawake wajawazito wanaosubiri kujifungua katiak hospitali ya wilaya ya Urambo, Oktoba 12, 2014. Kushoto ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwasa.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Thursday, September 18, 2014
KIKWETE AWASILI WASHINGTON
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa ameongozana na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe. Liberata Mulamula mara baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa La Guardia jijini Washington DC tayari kwa kushiriki katika mikutano mbalimbali na pia katika hafla ya "USIKU WA JAKAYA" leo jioni
Rais Kikwete akilakiwa na maafisa wa ubalozi wa Tanzania nchini Marekani baada ya kuwasili hoteli aliyofikia
Karibu Washington DC Mheshimiwa
Rais akiendelea kusalimia na na wafanyakazi wa ubalozini
Mapokezi yakiendelea
Rais Kikwete akisalimiana na Bw. Lucas Mkama wa Vijimambo Blog
Karibu sana Mzee...
PICHA NA IKULU
Wednesday, September 17, 2014
RAIS KITWETE AELEKEA NCHINI MAREKANI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ameondoka nchini usiku wa jana, Jumatatu, Septemba 15, 2014, kuanza ziara ya wiki mbili katika Marekani ambapo atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (UN General Assembly) New York. Mbali na kuhutubia Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York, Rais Kikwete pia atahudhuria mikutano muhimu katika mji mkuu wa Marekani, Washington, D.C.
Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 15, 2014. Kushoto ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali
Rais Kikwete akiagana na viongozi mbalimbali wakiwemo wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama waliofika kumuaga katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Septemba 15, 2014. Kulia ni Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali
Rais Kikwete akisindikizwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Gharib Bilali wakati alipokuwa anaondoka katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam kuelekea Marekani Septemba 15, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakiwasili New York, Marekani. Kulia Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa Balozi Tuvako Manongi akifuatiwa na Mama Upendo Manongi Septemba 16, 2014
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Ubalozi wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete wakilakiwa na maofisa mbalimbali wa Tanzania baada ya kuwasili New York, Marekani, Septemba 16, 2014. PICHA NA IKULU
WAZIRI MKUU PINDA NA WAHISANI
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiteta na Bw. Lord Hollick ambaye ni Mjumbe wa Masuala ya Biashara wa Waziri Mkuu wa Uingereza nchini Tanzania katika majadiliano kuhusu ushirikiano baina ya serikali na Sekta Binafsi (PPP Dialogue) kwenye hoteli ya Hyatt Regency- Kilimanjaro jijini Dar es salaam.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa katika picha ya pamoja na ujumbe wa wa Kampuni ya Japani ya SUMITOMO baada ya kuzungumza nao ofisini kwake jijini Dar es salaam Kulia kwake ni Rais wa kampuni hiyo, Nakamura Kumharu.
Tuesday, September 09, 2014
RAIS KIKWETE NA WAJUMBE WA KITUO CHA DEMOKRASIA
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na ujumbe wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD) baada ya kumalizika kwa awamu ya pili ya mazungumzo nao Ikulu Ndogo mjini Dodoma.
PICHA NA IKULU
WAZIRI MKUU PINDA JIJINI ARUSHA
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akisalimiana na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Kibosho wakati alipokutana nao kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro wakiwa katika ziara ya kujifunza masuala ya usafiri wa anga. Mheshimiwa Pinda alikuwa akienda Dar es salaam akitoka Arusha.
Subscribe to:
Posts (Atom)
















