Saturday, August 10, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA WAZIRI WA UCHUMI,VIWANDA NA BIASHARA WA JAPAN

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na  Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Mheshimiwa Toshimistu Motegi alipokutana na kufanya mazungumzo naye  Ikulu, Dar Es Salaam.

PICHA NA IKULU
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete akimsindikiza   Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Mheshimiwa Toshimistu Motegi baada ya kukutana na kufanya mazungumzo naye  Ikulu, Dar Es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Waziri wa Uchumi, Biashara na Viwanda wa Japan, Mheshimiwa Toshimistu Motegi (wa tatu kushoto, mbele)  na ujumbe wake pamoja na Waziri wa Uchukuzi  Dkt.  Harrison Mwakyembe (wa kwanza kulia),  Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwezeshaji na Uwekezaji Dr Mary Nagu (wa pili kulia), Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Abdallah Kigoda (wa pili kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Japan Mhe Salome  Sijaona  (wa kwanza kushoto) alipokutana na kufanya mazungumzo naye  Ikulu, Dar Es Salaam.

KATIKA KUSHEHEREKEA SIKUU YA IDDI WATANZANIA WAMEOMBWA KUDUMISHA AMANI ILIYOPO HAPA NCHIN


Alhaji Yusufu Saidi Mfinanga wa kibaha Njuweni Pamoja na Mke wake Mama Mfinanga wamewaomba  Watanzania   kudumisha amani na upendo kwa kuondoa tofauti zetu za kidini kisiasa kwani kufanya hivyo mwenyezi mungu ataendelea kuijalia amani na baraka iliyo kuwepo  hapa nchini  kwani kupendana kutaleta maendeleo katika nchi tuswali na kuheshimu mamlaka za serekali zilizopo kwani mafundisho ya dini zote yafundisha amani upendo na utii.

MAMMBO YA SIKUKUU YA IDD

 Ma Ernestina Mwesiga akiwa na wajukuu zake, wa kwanza kulia ni Ayesiga Rugalabamu, kushoto Kalumuna Rugalabamu na Muumuliza.
 Margreth Abella akiwa na Ma Erenestina, hili ni eneo la kijiji cha Rushasha katika tarafa ya Bugabo.


 Mlima wa kutoka eneo la kijiji cha Rushasha kuelekea Barabara kuu ya kutokea Rubafu.
Ayesiga na Kalumuna wakiwa kwenye moja ya pango linalopatikana eneo la mlima wa Rushasha.

Friday, August 09, 2013

RAIS KIKWETE AKUTANA NA BUNGE LA AFRIKA MASHARIKI

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia jambo na baadhi ya wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2013. Kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki,  Dkt. Abdala Juma Abdulla Saadalla.
 


Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wabunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki waliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Agosti 7, 2013. Wa pili kushoto ni Naibu Waziri wa Wizara ya Ushirikiano ya Afrika Mashariki,  Dkt. Abdala Juma Abdulla Saadalla.

WAZIRI MKUU PINDA NCHINI UINGEREZA

 Waziri  Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakisalimiana na baadhi ya watumishi  wa ubalozi wa Tanzania nchini Uingereza  uliopo London baada ya kuwawsili kwenye ubalozi huo kuzungumza na watanzania waishio Uingereza Agosti 6, 2013. (Picha na Ofisi ya Wazire Mkuu)
 Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na Mkewe Tunu wakisalimiana na Watoto Tanzania nchini Uingereza uliopo London  kuzungumza na watanzania waishio Uingereza Agosti 6,2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)