Tuesday, April 02, 2013
RAIS KIKWETE AKUTANA NA NAIBU RAIS MTEULE WA KENYA
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akipozi na familia ya Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika
hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete leo April 1, 2013 akisalimiana na Mama Rachel Chebet, mke wa Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto katika hoteli ya kitalii ye Seronera katika mbuga ya wanyama ya Serengeti mkoani Mara. Mhe Ruto alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho
Kikwete leo April 1, 2013 amekutana na Naibu Rais mteule wa Kenya Mhe William Kipchirchir Samoei arap Ruto ambaye alikuwa nchini kwa mapumziko ya Pasaka.
Akiongea na mgeni huyo katika hoteli ya Seronera iliyoko
katika mbuga ya wanyama ya Serengeti
mkoani Mara, Rais Kikwete amempongeza Mhe Ruto na Rais mteule wa Kenya
Mhe. Uhuru Kenyatta, kwa ushindi wao kwenye uchaguzi mkuu nchini Kenya.
Mhe Rais pia alimueleza Mhe Rutto furaha yake pamoja na
kuridhishwa na jinsi uchaguzi ulivyofanyika kwa amani katika nchi
hiyo.
Alielelezea matumaini
yake ya kuwa urafiki uliopo kati ya
Tanzania na Kenya utadumishwa pamoja na kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.
Mhe Rutto, ambaye aliwasili mkoani Mara wiki iliyopita akiwa na mke wake na
watoto, ameondoka leo baada ya chakula
cha mchana alichoandaliwa na mwenyeji wake.
Monday, April 01, 2013
WAJUKUU WAMTEMBELEA BIBI YAO
Ayesiga Rugalabamu kulia na Ivan Kalumuna kushoto wakiwa na bibi yao Ernestina Mwesiga baada ya kumtembelea anaishi katika kijiji cha Rushasha, Bugabo.
Ayesiga na Ivan wakipanda mlima wa Rushasha.
Ayesiga na Ivan wakipanda mlima wa Rushasha.
KAMANDA KALANGI AKIELEZEA MATUKIO YA UHARIFU
MTU mmoja anayetuhumiwa kwa
ujangili ameuwawa baada mapambano makali ya kurushiana risasi kati ya
askari jeshi la polisi mkoani Kagera lililoshirikiana
na askari wa idara ya wanyama pori na kundi la watuhumiwa wa ujangili ndani ya
pori la hifadhi ya taifa la Burigi lililoko wilayani Ngara.
Akizungumza na waandishi wa habari kamanda wa jeshi la
polisi mkoani Kagera, Philip Kalangi amesema mapambano hayo yalianza pale majangili
hayo yaliyokuwa na silaha mbalimbali za kivita yalipoanza kujiami kwa kwa
kuwarushia askari risasi ambao walikuwa wakiyaamulu majangili hayo
yajisalimishe.
Katika tukio jingine kamanda Kalangi amewaambia waandishi wa
habari kuwa jeshi la polisi linamshikilia Joshua Mlindwa (25) mhaya mkazi wa
kata kashai mhutumiwa wa kuvunja ofisi ya shule ya sekondari ya Bukoba kwa kutumia funguo bandia kuiba yeti vya taaluma 131.
Akisimulia tukio hilo amesema mtuhumiwa amekamatwa baada ya kuwekewa
mtego, Kalangi amesema kuwa mtuhumiwa
alikuwa akidai uongozi wa shule ya sekondari ya Bukoba impatie shilingi milioni
6 ambayo alitaka ilipwe kwa njia ya M pesa ili aweze kurejesha vyeti hivyo la
sivyo angeviaribu kwa kuvichoma moto.
Kamanda Kalangi akionyesha vyeti ambavyo vilikuwa vimeibiwa na mtuhumiwa anayeshikiliwa na jeshi la polisi n i vyeti vya taaluma vya wahitimu wa kidato cha nne wa shule ya sekondari ya Bukoba iliyoko katika manispaa ya Bukoba.Kamanda akionyesha funguo bandia.
RAIS KIKWETE ATEMBELEA MAJERUHI MOI
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mke wake Mama Salma Kikwete wakiwa katika wodi ya Sewa haji ya Taasisi ya Mifupa ya MOI katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es salaam leo Machi 31, 2013 wakimjulia hali na kumpa pole Bw. Selemani Saidi, mmoja wa majeruhi walionusurika katika jengo lililoporomoka katikati ya jiji Ijumaa iliyopita na kusababisha vifo vya watu 25 Kushoto mwenye suti nyeusi ni Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mhe. Raymond Mushi Kulia ni Daktari C.N. Mcharo wa taasisi ya Mifupa ya Moi.
Subscribe to:
Posts (Atom)










