Monday, November 05, 2012

EDIUS NJUNWA MWESIGA APATA MWENZA WAKE ELIDA NTUNGILWEGE.

 Maharusi Edius Njunwa na Elida Tungilwege wakiwa nje ya kanisa muda mfupi baada ya kufunga ndoa yao takatifu katika kanisa la kiinjili la kirutheri lililoko katika manispaa ya Bukoba.
 Bwana na Bibi, Jonas Lwezaura mashahidi wa ndoa wa Edius Mwesiga na Elida Ntugilwege.
 Wazazi wa Edius Njunwa Mwesiga wakiwa kwenye ukumbi wa Bukoba Club ambao harusi ilifanyika.
 Maharusi wakikata utepe.
 Mambo ya keki hayo.
 Maharusi wakilishana Keki.
Watoto waliosimamia harusi, kutoka kulia ni Benson Baina, Kalumuna Rugalabamu, Ayesiga Rugalabamu na Stella.

Saturday, November 03, 2012

Rais Kikwete azindua rasmi Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela - Arusha (NM-AIST)

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi  Hati ya Ardhi ya eneo la   Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela  jijini Arusha  Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilali ambaye ndiye Mkuu wa Chuo hicho katika sherehe za uzinduzi wake rasmi  Ijumaa Novemba 2, 2012. Kulia ni Makamu Mkuu wa Taasisi hiyo Profesa Burton Mwamila.

MASSAWE AZINDUA MNARA WA VODACOM KISIWA CHA GOZIBA


Wakazi wa Kisiwa cha Goziba Kilichoko Wilayani Muleba wamekombolewa na kampuni ya mawasIliano ya Vodacom Tanzania baada ya kampuni hiyo kuzindua mnara wake wa  mawasiliano katika kisiwa hicho ambapo  wananchi sasa wanaweza kuwasiliana popote Tanzania na duniani kwa kutumia mtandao wa mawasiliano wa Vodacom.

Mnara wa Vodacom Kisiwani Goziba ulizinduliwa jana tarehe 30/10/2012 na Mhe. Kanali Mstaafu Fabian I. Massawe aliyembatana na Mkuu wa Wilaya ya Muleba Mhe. Lembrisi Kipuyo. Pia Katika uzinduzi huo Kampuni ya Vodacom iliwakilishwa na Salum Mwalimu ambaye ni Meneja Mahusiano ya nje wa Kampuni hiyo.

Katika Uzinduzi huo Meneja Mahusiano ya nje wa Vodacom Salum Mwalimu aliwaomba wananchi wa kisiwa cha Goziba kuulinda na kuutunza mnara huo kwani alisema kuwa mnara huo umejengwa kwa gharama kubwa, ni zaidi ya mara mbili ya gharama ya kujenga mnara mmoja katika eneo la nchi kavu. Pia aliwahakikishia wananchi wa Goziba kuwa huduma nyingine mbalimbali  kama M- Pesa zitapelekwa kwao.

Wananchi wa Kisiwa cha Goziba ambao ni 6000  pamoja na kuchangia asilimia 25 ya pato la wilaya ya Muleba, walisema kuwa kabla ya mnara huo hawakuwa na aina yoyote ya mtandao wa simu, pia bado wanakabiliwa na changamoto katika huduma za kijamii kama shule, Zahanati, na maji safi na slaama. Vilevile usafiri wa kuaminika  na kukumbwa na ujambazi wa mara kwa mara na kunyanganywa mali zao.

Wananchi hao waliishukuru Kampuni ya Vodacom Tanzania kwa kuwakumbuka kupitia mbunge wao Charles Mwijage wa Jimbo la Muleba Kasikazini kuwawekea mnara huo ambao utawatatulia baadhi ya kero zao kama kero ya ulinzi kwani itakuwa rahisi kutoa taarifa za uharifu kwa haraka sana pale unapotokea.

Mkuu wa Mkoa alisistiza sana wananchi hao kuutumia mtandao huo kwa manufaa yao na taifa lakini siyo kutumia simu zao kwa mambo ya uhasherati kwani UKWIMWI bado unatisha sehemu za visiwani. Aliwasistiza wananchi hao kuwa waaminifu walioko kwenye ndoa, kutumia kinga na vijana kusubiri muda wao wa kuoa ndiyo waoane. Pia Mhe. Massawe alitumia muda huo kuwagawia kinga (kondomu) wananchi hao na kuwashauri kuzitumia ili kupanga uzazi na kujikinga na virusi vya UKWIMWI.

Vodacom Tanzania tayari pia imetoa Tshs. 4,200,000/= kwa ajili ya ujenzi wa zahanati, pia Mkuu wa Mkoa naye alitoa Tshs 500,000/= ili kuendeleza jengo la zahati ya Goziba ambalo limefikia hatua ya Msingi. Changamoto ni vifaa vyote vya ujenzi kupatika na nje ya kisiwa hicho hata matofari  ya kujengea yafyatuliwa Mwanza na kuletwa kisiwani humo isipokuwa mawe tu.

Mnara wa Vodacom siyo tu ni faida ya wakazi wa Goziba na visiwa vya jirani isipokuwa imekuwa mkombozi kwa Manahodha wa mitumbwi iliyokuwa inapotea mara kwa mara na kujikuta sehemu nyingine kwasababu ya kisiwa hicho kutoonekana kwa mbali. Mnara huo umekuwa ndiyo dira ya nahodha wanaokwenda huko kwasasa.

Wilaya ya Muleba inavyo visiwa 36 na 24 tu ndivyo vinakaliwa na wananchi. Pia serikali ianaendelea na juhudi za kuhakikisha huduma za kijamii zinapatikana katika kisiwa hicho ambapo inatarajia katika miaka miwili ijayo itakuwa tayari imeanzisha kituo cha Polisi kisiwani humo.

Imeandikwa na :               Sylvester Raphael
                                                Afisa Habari Mkoa
                                                KAGERA @2012

MASSAWE AFANYA MAAJABU ATEMBELEA KISIWA CHA GOZIBA

 Mandhari ya kisiwa cha Goziba.
 Salum Mwalim Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom Akiongea na Wananchi wa Kisiwa cha Goziba.
Mkuu wa Mkoa kanali mstaafu Fabian Massawe, Katibu wa CCM, Kagera na Salum Mwalim Meneja Mahusiano ya Nje wa Vodacom na RPC Kagera Philipo Karangi Wakiwasili Kisiwani Goziba, Massawe ni mkuu wa mkoa wa kwanza mkoani Kagera kutembelea kisiwa hicho tangu nchi ipate uhuru.

Friday, November 02, 2012

MAMLAKA YA MAPATO KAGERA YAZINDUA WIKI YA MLIPA KODI

Baadhi ya maoofisa wa mamlaka ya mapato mkoani Kagera wakisikiliza hotuba ya ufunguzi iliyokuwa inatolewa  na mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi Ziporah Pangani.

Mmoja wa maofisa wa TRA

Mkuu wa wilaya ya Bukoba Bi Ziporah Rion Pangani akitoa hotuba ya ufunguzi wa wiki ya mlipa kodi ulifanyika kwenye ukumbi wa chama cha msalaba mwekundu.

Mameneja wa TRA, kulia ni Bw. Mgimba na kushoto ni Magere.

KIKAO CHA MTANDAO UNAOYAUNGANISHA MASHIRIKA YASIYO YA KISERIKALI KAGERA

 Dr George Buberwa akiongea wakati wa kikao cha mtandao wa mashirika yasiyo ya kiserikali Kagera KANGONET  kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Kagera.
 Wajumbe halali wa KANGONET.
 Wajumbe wengine.

 Bw. Kiiza alikuwa mmoja wa walioudhuria kikao cha KANGONET, wajumbe wa mtandao huo walikuwa wakulalamikia uongozi ulioko madaraka ambao ni pamoja na Katibu Christan Byamungu na mwenyekiti Yusto Mchuruza, walisema viongozi hao hawana imani nao.
 Kimani na Michael.

Afisa maendeleo ya jamii mkoani Kagera Charles Mwafimbo ndiye aliyeongoza kikao hicho.