Sehemu ya zawadi iliyotolewa na mkuu wa mkoa wa Kagera Kanali Mstaafu Fabian Massawe kwa vikundi visivyojiweza kwa ajili ya kusherekea sikukuu ya Idd, hawa ni mbuzi.
Massawe akitoa zawadi kwa msimamizi wa kituo cha kulea watoto yatima cha Uyacho kilichoko Hamgembe, Kagera.
Msimamizi wa kituo cha kulelea yatima cha Nusuru yatima akipokea zawadi ya sikukuu ya Idd.
Massawe akimungalia mmoja wa yatima wanaolelewa katika kituo cha Nusuru yatima kilichoko Kashai, alichukizwa na hali aliyokuwa nayo mtoto huyo.
Msimamizi wa kituo cha kulea wazee cha Kiilima akipokea zawadi ya mbuzi toka kwa Massawe.
Baadhi ya viongozi mkoani Kagera walioudhuria tafrija fupi ya kukabiddhi zawadi ya Idd kwa wasiojiweza, ilifanyika kwenye viwanja vya Ikulu ndogo iliyoko katika manispaa ya Bukoba.
Friday, October 26, 2012
Wednesday, October 24, 2012
RAIS KIKWETE AFUNGUA MKUTANO MKUU WA NANE WA UVCCM MJINI DODOMA
Bendi ya muziki ya Vijana Jazz Orchestra 'Wana Pambamoto' ikitumbuiza
kwa wimbo maalumu katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma ikiwa
ni shamra ya kufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo ya vijana wa
chama tawala leo Oktoba 23, 2012
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Rais Jakaya Mrisho Kikwete akipokea zawadi toka kwa Mwenyekiti anayemaliza muda wake wa UVCCM Bw. Benno Malisa katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kabla ya kufungua Mkutano Mkuu wa nane wa Jumuiya hiyo ya vijana wa chama tawala leo Oktoba 23, 2012

Tuesday, October 23, 2012
MNYAUKO BACTERIA WATISHIA USALAMA WA NDIZI KAGERA
UGONJWA unaoshambulia migomba wa mnyauko bacteria umeanza kuathiri
upatikanaji wa ndizi kwenye maeneo mbalimbali yaliyoko mkoani Kagera.
Ugonjwa huo unasambaa kwa kasi hasa kwenye maeneo ya wilaya za Muleba na Karagwe ambayo uzalisha ndizi nyingi mkoani Kagera na maeneo mengine ya wilaya za Bukoba na Misenyi.
Hali ya ugonjwa huo unaoshambulia migomba wa mnyauko bacteria imechangbia kupunguza uzalishaji wa ndizi mkoani Kagera jambo ambalo limechangia kupanda kwa bei ya ndizi zinapopelekwa kwenye masoko.
Uchunguzi uliofanywa na gazeti hili umebaini kwamba kwenye soko kuu la Bukoba ndizi kubwa inauzwa kwa wastani wa kati shilingi 15,000 hadi 20,000 ambapo miaka iliyopita ndizi kubwa zilikuwa zinauzwa kwa wastani wa kati ya shilingi 6,000 hadi 8,000.
Kupanda kwa bei ya ndizi iliyochangiwa na ugonjwa wa mnyauko bacteria wa migomba kumewalazimisha baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kagera ambao hutegemea ndizi kama chakula chao kikuu kubadilika ambapo sasa wanalazimika kula ugali na wali.
Baadhi ya wakazi wa mkoa wa Kagera wamelazimika kubadili fikira zao za kudhani kuwa ndizi ndicho chakula kikuu baada ya kushindwa kumudu gharama za kununua ndizi kwenye masoko ambazo bei yake ni kubwa.
Baadhi ya wakulima bora wa migomba mkoani Kagera ambao mashamba yao yameathirika kutokana na ugonjwa wa mnyauko bacteria wa mogomba ni pamoja kamishina mstaafu wa jeshi la polisi Alfred Tibaigana.
Kamishina Tibaigana shamba lake liko katika kijiji cha Buganguzi wilayani Muleba limeathirika sana, Mkulima huyu kabla ya ugonjwa huu alikuwa na uwezo wa kuzalisha wastani tani 40 za ndizi kwa wiki ambapo sasa anazalisha wastani wa tani zisizozidi 10 kwa wiki.
Aidha, baadhi ya wakulima mkoani Kagera wameitahadharisha serikali kuchukua hatua za haraka za kuthibiti ugonjwa huu unaosambaa kwa kasi ili zao la ndizi mkoani Kagera lisibaki kwenye vitabu vya historia.

Monday, October 22, 2012
RAIS KIKWETE KATIKA KILELE CHA MKUTANO MKUU WA UWT DODOMA
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akihutubia katika ukumbi wa
Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake
Tanzania (UWT).
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT.
Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasili katika ukumbi wa Chuo cha Mipango mjini Dodoma kufunga mkutano mkuu wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT.
YAJUE MAENEO YA MANAYOPAMBA MJI WA BUKOBA
Barabara ya Kashozi iliyoko katika manispaa ya Bukoba.
Barabara ya kuelekea tarafa ya Bugabo.
Standi kuu ya mabasi yaendayo Bugabo iliyoko katika halmashauri ya manispaa ya Bukoba.
Mitaa ya manispaa ya Bukoba.
Mandhari ya mzunguko uliko karibu na standi kuu ya mabasi.
Eneo la standi kuu ya mabasi.
Sanamu ya mgomba iliyoko kwenye mzunguko mkuu wa manispaa ya Bukoba.
Mandhari ya maeneo ya uswahilini.

Sunday, October 21, 2012
JESHI LA POLISI KAGERA LINAVYOFANYA KAZI YA KUWAHAMASISHA WANANCHI KUPIMA AFYA ZAO
JESHI la polisi mkoani Kagera limeanza kutekeleza mkakati
wake mpya ambao limeubuni wa kuwahamasisha wananchi mkoani humo kupima afya zao.
Mkakati huo ulidhihirika mwishoni mwa wiki baada jeshi
hilo kuendesha zoezi la kuwapima wananchi wa manispaa ya Bukoba na maeneo
mengine virusi vinavyoambukiza ugonjwa wa UKIMWI.
Katika zoezi hilo lililofanyika kwenye maeneo ya standi kuu
ya mabasi zaidi ya wananchi zaidi 1,500 walijitokeza kupima virusi vya UKIMWI
kwa hiari.
Akiongea wakati wa zoezi hilo la upimaji mrakibu msaidizi wa
jeshi la polisi Dr Hussein Gamu ambayo aliendesha zoezi hilo kwa kushirikiana
na maofisa wengine wa jeshi hilo alisema mkakati wa jeshi hilo wa kuanzisha
utaratibu wa kupima wananchi afya zao unalinga kuimarisha mahusiano kati ya
jeshi hilo na wananchi.
Gamu alisema jeshi la polisi lina mkakati mkikati ya kuimarisha ustawi wa wananchi, alisema
wananchi wanapokuwa na ustawi wanakuwa na uwezo mkubwa wa kutekeleza majukumu
yao vizuri.
Afisa huyo alisema kuwa wananchi ndio nguzo kubwa ya jeshi la polisi, aliendelea kusema wananchi
ndio wanalipa nguvu jeshi hilo liweze kutekeleza majukumu yake vizuri.
Alisema taarifa zinazotolewa na wananchi zinazohusiana na
masuala ya uharifu kuwa ndizo zinazolisaidia
jeshi la polisi kukabiliana na matukio ya uharifu kwa kiasi kikubwa.
Gamu alisema jeshi hilo litaendelea kuwa karibu na wananchi
hasa kupitia kwenye dhana yake maalumu ya polisi jamii na ulinzi shirikishi,
alimaliza kwa kuwaomba wananchi waendelee kulipa ushirikiano jeshi hilo ili
waweze kunufaika nalo zaidi.
Subscribe to:
Posts (Atom)