Sunday, October 21, 2012

RAIS KIKWETE AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA KENYA IKULU DAR ES SALAAM

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa  Jakaya Mrisho Kikwete ametaka wananchi wa Kenya wapewe nafasi ya kuamua ni viongozi gani wanawataka katika Uchaguzi Mkuu uliopangwa kufanyika Machi mwakani.

Aidha, Rais Kikwete amesema kuwa wananchi wa Kenya wanayo haki ya msingi kabisa kuamua hatma ya taifa lao katika Uchaguzi Mkuu huo.

Mheshimiwa Rais aliyasema hayo leo Oktoba 21, 2012 alipokutana na kufanya mazungumzo na ujumbe wa wabunge wa vyama mbalimbali vya siasa vya nchini Kenya uliomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam.

Ujumbe huo uliongozwa na Naibu Waziri Mkuu wa Kenya na Waziri wa Fedha Mhe. Uhuru Kenyatta ambaye pia ni Mwenyekiti wa  chama cha TNA na Waziri wa Sheria wa Kenya Mhe Eugene Wamalwa wa chama cha New Ford Kenya. Wote wawili ni wagombea wa nafasi ya Urais katika uchaguzi ujao.
Wengine katika msafara huo walikuwa ni Naibu Waziri wa Afya na mbunge wa Mombasa Mhe. Kambi Kazungu, Mbunge wa kuteuliwa wa chama cha TNA  Bi Rachel Shebesh, na Mbunge wa Kajiado kwa tiketi ya TNA Moses ole Sakuda na mbunge wa zamani Mhe Abdullahi Alli.

Rais Kikwete aliwapongeza kwa kuamua kufanya kazi kwa pamoja licha ya kuwa watakuwa  washindani katika kinyang’anyiro cha uchaguzi mkuu huo.

Mheshimiwa Rais ameitakia heri nchi ya Kenya katika uchaguzi huo ujao, na kusisitiza kwamba nchi hiyo ya jirani ina umuhimu katika mustakabali wa kiuchumi kwa nchi  za Afrika Mashariki.

Rais Kikwete wakati huo akiwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika (AU) alikuwa miongoni mwa viongozi walioshughulika sana kutafuta ufumbuzi wa ghasia na vurugu zilizozuka kufuatia Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2007 nchini Kenya.

Rais Kikwete alikaa siku tatu nchini Kenya akitafuta usuluhishi wa vurugu hiyo ya kisiasa nchini humo, ambayo katika mazungumzo yake leo ameyataja kama ajali iliyolipata Taifa la Kenya, na ambayo majirani wake hawaitarajii kutokea katika uchaguzi ujao.
Mwisho

Imetolewa na:
KURUGENZI YA MAWASILIANO YA RAIS
DAR ES SALAAM,
21 Oktoba, 2012

Friday, October 19, 2012

RAIS KIKWETE AREJEA NCHINI

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Makamu wa Rais Dkt Mohamed Ghalib Bilal leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere mara alipowasili kutoka katika ziara rasmi ya siku nne nchini Oman.

MKUTANO WA KUJADILI SEKTA YA GESI ASILIA

  Meneja wa Sekta Kupunguza Umaskini na Kusimamia Maendeleo ukanda wa Afrika wa Benki ya Dunia Dkt Albert Zeufack, akongea wakati wa mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusu sekta ya Gesi asilia nchini, akiwa ameongozana na mabalozi wa nchi kadhaa pamoja na Timu ya wataalam walioletwa na washirika wa maendeleo na  inayowakilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa, Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za China, Uingereza na Ujerumani

 Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akitoa ufafanuzi kwa baadhi ya waandishi wa habari baada ya mkutano na wanahabari Ikulu jijini Dar es salaam leo kuhusu sekta ya Gesi asilia nchini.Mkutano huo ulihudhruiwa pia na  mabalozi wa nchi kadhaa pamoja na timu ya wataalam walioletwa na washirika wa maendeleo na  inayowakilisha Benki ya Maendeleo ya Afrika, Benki ya Dunia, Shirika la Fedha la Kimataifa, Jumuiya ya Nchi za Ulaya na Nchi za China, Uingereza na Ujerumani ilipotembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo. Wa pili kushoto ni Waziri wa Katiba na Sheria Bw. Mathias Chikawe, akifuatiwa na Naibu Katibu Mkuu Ikulu Mama Suzan Mlawi na maafisa waandamizi  wa Ofisi ya Rais, kamati hiyo


PICHA NA IKULU

KAMATI YA BUNGE INAYOSHUGHUKIA UUNDWAJI WA SHERIA NDOGO NDOGO YAMALIZA KAZI YAKE KAGERA

Mkuu wa mkoa wa kagera kanali mstaafu Fabian Massawe akipongezana na mwenyekiti wa kamati ya bunge inayoghulikia sheria ndodo ndogo baada ya kikao cha majumuisho za ziara ya kamati hiyo kilichofanyika kwenye ukumbi wa mkuu wa mkoa wa Kagera.
Baadhi ya watendaji wa halmashauri ya wilaya ya Bukoba.
 Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Muleba, Richard Katomero (kushoto).
Massawe akiongea na watendaji wa halmashauri za wilaya na manispaa.

Thursday, October 18, 2012

KAMATI YA BUNGE INAYOSHUGHULIKIA MASUALA YA TUNGAJI WA SHERIA NDOGO NDOGO

 Wabunge wanaounda kamati ya bunge inayoshughulikia sheria uundwaji wa sheria ndodo ndogo
 Mkuu wa mkoa wa Kagera kanali mstaafu Fabian Massawe akiongea na kamati ya bunge ofisini.